Washtakiwa wakiwa katika gari la polisi
Wakipanda gari baada ya kusomewa mashitaka
Wakitoka mahakamani baada ya kusomewa mashitaka
Washtakiwa wakisubiri kuingia mahakamani. Picha na Sultani Kipingo wa Globu ya Jamii
Mkurugenzi
wa Mashitaka Nchini (DPP), aliwapandisha kizimbani vigogo wanne wa Chuo
Kikuu cha Kimataifa cha Tiba (IMTU) na baadaye kuwaondolea mashitaka
kupitia hati ya Nole ya kuwaondolea mashtaka ya kushindwa kufukia viungo
vya binadamu na kupeleka hati ya kufukia viungo vilivyotumika
kufundishia kwa Kampuni Coroner.
Vigogo
hao ni, Venkat Subbaian (57), Appm Shankar (64), Prabhakar Rao (59) na
Dinesh Kumar (27) ambao walisomewa mashtaka yao katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo saa 8:07 mchana.
Washtakiwa hao walisimama kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi,
Kwey Lusemwa.
Mwendesha
Mashitaka wa Polisi, Magoma Magina alidai kuwa Julai 20, mwaka huu
washtakiwa wakiwa na nyadhifa tofauti, Profesa, Mtawala na wahadhiri,
kwa makusudi walishindwa kufukia mifuko 83 iliyokuwa na viungo vya
binadamu kinyume cha sheria ya 128 kifungu cha 8 na cha 9 cha Mwenendo
wa Makosa ya Jinai (CPA).
Magina
alidai kuwa katika shitaka la pili, washtakiwa wote kwa pamoja
walishindwa kupeleka hati ya kumtarifu kwamba wamefukia viungo hivyo
baada ya kutumika kufundishia kama sheria inavyowataka.
Hakimu Lusemwa alisema washtakiwa watakuwa nje kwa dhamana kwa kuwa na wadhamini wawili raia wa Tanzania kila mmoja.
Hakimu Lusemwa alisema washtakiwa watakuwa nje kwa dhamana kwa kuwa na wadhamini wawili raia wa Tanzania kila mmoja.
Hata
hivyo, kabla mahakama haijasikiliza kipengele cha dhamana, Wakili wa
Serikali Mwandamizi, Salum Ahmed aliwasilisha hati ya Nole kutoka kwa
DPP akidai kuwa anawaondolea vigogo hao mashtaka na kwamba hana nia ya
kuendelea kuwashitaki.
Ahmed
alidai kuwa DPP anawaondolea washtakiwa mashitaka hayo chini ya kifungu
cha 91 kidogo cha (1) cha CPA kwa kuwa hana nia ya kuendelea
kuwashitaka.
Wakili wa washtakiwa Gaudiosus Ishengoma alisema kwamba inaonekana kuna mbinu kubwa dhidi ya washtakiwa.
Alisema anavyofahamu kwamba hati ya mashitaka ingekuwa na kasoro wateja wake wangepata dhamana na baadaye ingewezekana kubadilishwa.
Alisema anavyofahamu kwamba hati ya mashitaka ingekuwa na kasoro wateja wake wangepata dhamana na baadaye ingewezekana kubadilishwa.
Alisema
kutokana na sababu hiyo, ana wasiwasi kwamba inawezekana DPP ana nia ya
kuwafungulia wateja wangu kesi yenye mashitaka yasiyokuwa na dhamana
ili wakasote mahabusu.
Viwanja
vya mahakama hiyo vilikuwa tulivu huku wanaodaiwa kuwa wafanyakazi wa
IMTU wakiwa wamesimama katika makundi makundi wakijadiliana hili na
lile.
Kupitia
magari ya Jeshi la Polisi, T 366 AVG aina ya Rav4 alipanda mshtakiwa wa
tatu kwa madai kuwa ni mgonjwa na washtakiwa wengine waliondoka
mahakamani hapo katika gari yenye namba za usajili KX06EFY aina ya
Toyota Landcruiser na kurudishwa mahabusu ya jeshi hilo.
No comments :
Post a Comment