Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Tuesday, July 8, 2014

TBL YATOA MSAADA WA SH. MIL. 25 ZA KUCHIMBA KISIMA CHA MAJI ZAHANATI YA MAKUBURI, DAR



 Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Kinondoni,Joseph Nicholous 9kushoto) akimkabidhi Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni,  ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Dk. Gunini Kamba mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 25 ikiwa ni msaada uliotolewa na TBL kwa ajili ya ujenzi wa kisima cha maji katika Zahanati ya Makuburi, Dar es Salaam. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika zahanati hiyo. Kulia ni Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo, Stella Kivugo na katikati ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mwongozo katika kata hiyo ya Makuburi.James Ngoitanile.
 Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni,  ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Dk. Gunini Kamba (wa pili kulia) akimkabidhi  mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 25 Mkurugenzi wa Kampuni ya Drima Drilling, Mhandisi Amiri Msangi msaada uliotolewa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa ajili ya ujenzi wa kisima cha maji katika Zahanati ya Makuburi, Dar es Salaam katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki  katika zahanati hiyo. Kulia ni Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo, Stella Kivugo na katikati ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mwongozo katika kata hiyo ya Makuburi.James Ngoitanile.
 Jengo la zahanati ya Makuburi
 Viongozi wa Manispaa ya Kinondoni,viongozi wa na wahudumu wa zahanati hiyo pamoja na Wajumbe wa kamati ya maji ya mtaa huo Mwongozo wakifurahia kupata msaada huo kutoka TBL.
Ofisa  Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu akielezea mikakati ya kampuni hiyo kutoa sehemu ya faida ya mauzo ya vinywaji vyao kuwapatia wananchi misaada ya maji nchini.
 Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Dk. Kamaba akitoa shukrani kwa TBL kwa msaada huo wa kisima cha maji.
 Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo, Kivugo akitoa shukrani kwa TBL kwa kuwapatia msaada wa kisima cha maji na kwamba kitendo hicho kitawapunguzia kwa asilimia kuwa tatizo la maji lililokuwa linaikumba zahanati hiyo.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

No comments :

Post a Comment