WASICHANA SABA WABAKWA KISHA KUNYONGWA NACHINGWEA-LINDI.
WASICHANA saba wamepoteza maisha
wilayani Nachingwea mkoani Lindi baada ya kubakwa na kunyongwa kisha
kuwekewa vijiti na chupa kwenye sehemu zao za siri.
Wasichana hao
wamepoteza maisha kwa nyakati tofauti katika kipindi cha miezi minne
iliyopita na wamekuwa wakipigiwa simu nyakati za usiku na kukutana na
waliwapigia simu ambapo hubakwa na kunyongwa na kisha katika sehemu za
siri kuwekewa vijiti au chupa.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick
Mwananzila amebainisha aina hiyo ya mauaji jana wakati alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari katika Hospitali ya Mkoa ya Sokoine.
Mwananzila
alikuwa amekwenda hospitalini hapo kuwatazama majeruhi ambapo
alifafanua kuwa mauaji hayo yanaendelea na juzi mtu mwingine aliuawa
katika mazingira hayo.
Alisema, "serikali ya wilaya ilishatoa
namba za simu kuwa unapopigiwa simu mtoto wa kike fanya juhudi
kumjulisha mwenzako au piga simu kituo cha polisi ili kuweza kukabiliana
na watu hao wanaotoa roho za watu".
Mwananzila alisema kuwa
binti mmoja aliweza kupigiwa simu na kundi hilo, aliamua kupiga simu
kituo cha polisi na kuweka mtego baada yeye kutoka nje, polisi walikuwa
wameshazingira maeneo hayo na wauaji wale walimfuata ndipo huyo binti
alianza kuvutana nao na hatimaye Polisi waliwatia mbaroni watu hao. Mkuu
huyo wa mkoa aliwaonya mabinti hao na kusema: “ni makosa kwa wasichana
kutoka nje baada ya kupigiwa …
"kinachotakiwa kwanza mjulishe mwenzako, lakini unafanya siri madhara yataweza kukutokea, hususani watoto wa kike".
Alisema
mauaji hayo yana ishara ya imani ya kishirikina. Hata hivyo uchunguzi
unaendelea kufanyika. Alisema suala hilo liko ndani ya uchunguzi hivyo
ni vizuri kufanyia kazi kwanza na kuwataka wananchi wawe na
subira.HABARILEO.
No comments :
Post a Comment