Watoto
wa shule ya Ojays Kiddies Zone iliyopo maeneo ya Kinondoni Block 41,
wakiwa kwenye chumba cha mapumziko kabla ya kuanza kwa mahafali ya Kaka
na Dada zao wa Laura Class kuanzia miaka 4-5 (T-shrits za kijani)
yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Regency Park jijini Dar
mwishoni mwa juma.
We are happy to Graduate....! Wanafunzi wa Laura Class wakipata Ukodak.
Mkurugenzi
wa Shule yaawali ya Ojays Kiddies Zone iliyopo Kinondoni -Block 41,
Bi. Debbie Ndulla akiwakaribisha walezi/wazazi na wageni waalikwa kwenye
mahafali ya pili ya shule hiyo yaliyofanyika mwishoni mwa juma jijini
Dar.
Baadhi ya walimu wa madarasa wakitambulishwa kwa wazazi kwenye mahafali hayo.
Walimu na wanafunzi wa Ojay Kiddies Zone wakitoa burudani kwa wazazi/walezi na waalikwa kwenye sherehe za mahafali hayo.
Wazazi/walezi wakichukua Ukodak wa watoto wao kwenye mahaali hayo.
Darasa
la awali la Lilies Class wa miaka 1-2 wakitoa burudani ya kuimba kwa
wazazi/walezi na wageni waalikwa kwenye mahafali ya kaka na dada zao.
Mwenyekiti
wa Bodi wa shule ya Ojays Kiddies Zone, Bi. Usia Nkhoma Ledama
akizungumza na wazazi/walezi kwenye mahafali ya pili ya shule hiyo
ambapo aliwashukuru wazazi kwa kuonyesha kuwaamini na kuwapa fursa
watoto wao kusoma kwenye shule hiyo yenye maadali bora na kuzingatia
ustawi wa mtoto pindi awapo katika mazingira ya shule.
Mwanaharakati
wa Haki za Watoto, Zubeida Masabo akitoa nasaha kwa wazazi/walezi juu
ya kuwalinda na haki za msingi ambapo aliwaasa kutenga muda wa
kufuatilia maendeleo ya mtoto kila siku, amewashauri wazazi kuwa na
taratibu za kutenga muda wa jioni kuzungumza na watoto wao kutokana
kukithiri vitendo vya ukatili dhidi ya watoto hali itakayosaidia kubaini
vitendo vya uovu.
Mmoja
wa wazazi Dr. Isaac Maro akifafanua jambo kwa wazazi/walezi likiwemo
suala la afya kwa watoto hasa magonjwa ambukizi kama Tetekuangua
(chicken pox) ambapo wazazi wengi wamekuwa na hofu endapo kunatokea
mlipuko wa ugonjwa huo kwenye mazingira ya shule wasihofu na kushauri
watoto kuendelea kuhudhuria masomo kwani wakiumwa utotoni ni nafuu zaidi
kutibika kuliko kuugua ukubwani.
Watoto
wa Lantana Class kuanzia miaka 3-4 wa shule ya awali ya Ojays Kiddies
Zone wakijitambulisha mbele ya wazazi/walezi kwenye mahafali hayo.
Kwa picha zaidi bofya hapa
No comments :
Post a Comment