Makamu
Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimkaribisha Balozi wa Oman nchini Tanzania, Saoud Ali Mohammed
Al-Ruqaish, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam,
leo Julai 3, 2014 kwa mazungumzo.
Makamu
Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na Balozi wa Oman nchini Tanzania, Saoud Ali Mohammed
Al-Ruqaish, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam,
leo kwa mazungumzo.
Makamu
Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimkaribisha Balozi wa Syria nchini Tanzania, Abdulmonem Annan, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo kwa mazungumzo.
Makamu
Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na Balozi wa Syria nchini Tanzania, Abdulmonem Annan,
wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo kwa
mazungumzo.
********************************************
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AKUTANA NA MABALOZI WA OMAN NA SYRIA
Ikulu jijini Dar es Salaam, Julai 03, 2014
Makamu
wa Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal
leo Alhamisi Julai 03, 2014 amekutana na Waheshimiwa Mabalozi wa nchi za
Oman na Syria wanaowakilisha nchi zao hapa Tanzania. Mheshimiwa Makamu
wa Rais amekutana na Mabalozi hao ofisini kwake Ikulu jijini Dar es
Salaam.
Awali
alikuwa ni Balozi wa Oman, Mheshimiwa Saoud Ali Mohammed Al-Ruqaish
aliyefika kukutana na Mheshimiwa Makamu na kufafanua kuwa uhusiano baina
ya Tanzania na Oman unazidi kuimarika na kwamba wawekezaji kutoka Oman
wamekuwa wakija kwa wingi kuwekeza Tanzania tofauti na siku za nyuma
huku pia Tanzania ikionesha kufungua milango yake kwa uwekezaji mkubwa
wa kati nchini Tanzania.
Kwa
upande wa Balozi wa Syria Mheshimiwa Abdulmonem Annan yeye alimueleza
Mheshimiwa Makamu wa Rais kuwa Syria iko katika kipindi kigumu na kwamba
nchi hiyo kwa sasa inatafuta kila linalowezekana kurejesha amani.
Balozi huyo alifafanua kuwa nchi yake inahitaji msaada wa nchi za
Kimataifa ili kusaidia kuweka pande zote zinazokinzana mezani kwa lengo
la kufikia maazimio yatakayoifanya nchi hiyo isiparanganyike.
Mheshimiwa
Makamu wa Rais alimueleza Balozi za Syria kuwa, Tanzania inatamani sana
kuona hali ya utulivu inarejea Syria na kwamba nchi hiyo inaendelea
kujenga uchumi uliobomoka tayari. Pia alisema kuwa msimamo wa Tanzania
unabakia katika kutaka pande zinazohusika katika mgogoro huo zinafuikia
suluhu kwa amani ili wananchi wengi wasipoteze maisha.
Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
Ikulu Dar es Salaam
No comments :
Post a Comment