Lionel Messi amepewa tuzo ya mchezaji bora wa mashindano .
Imechapishwa Julai 14, 2014, saa 8:32 usiku
LICHA ya kupoteza mechi ya fainali na
kukosa kombe la dunia mwaka 2014, mshambuliaji wa Argentina na
Barcelona, Lionel Messi ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa michuano ya
kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
Tuzo hii imekuja kaka ya kustaajabisha kwa watu wengi, lakini kwa kiasi kikubwa alistahili kupewa.
Messi alionesha kiwango kikubwa katika
hatua ya makundi akifunga mabao 4 katika michezo mitatu dhidi ya
Bosnia, Iran na Nigeria, lakini nyota yake ilififia baada ya kushindwa
kufunga katika mechi za mtoano dhidi ya Switzerland, Ubelgiji, Uholanzi
na Ujerumani.
Katika mchezo wa fainali dhidi ya
Ujerumani, Messi alipoteza nafasi moja muhimu, lakini muda mwingi
alifanya jitihada za kutafuta upenyo bila mafanikio.
Lionel Messi alipiga shuti, lakini alikosa bao katika mchezo wa fainali Maracana.
Baada ya kipyenga cha mwisho, Messi alipokea tuzo yake ya mchezaji bora akiwashinda nyota wa Colombia James
Rodriguez, winga wa Uholanzi, Arjen Robben na wachezaji watatu wa
Ujerumani, Manuel Neuer, Bastian Schweinsteiger na Thomas Muller.
Ndoto zimezima: Lionel Messi akiangalia chini baada ya kupoteza mechi ya fainali dhidi ya Ujerumani.
No comments :
Post a Comment