Taarifa kwa vyombo vya habari
Wakazi wa Mtwara na Lindi kushuhudia fursa za Utalii na Uchumi kupitia Tamasha la Utamaduni la Mtwara.
10 Julai, 2014. Mtwara.
Tamasha la Mkoa wa Mtwara, ‘Mtwara Festival’, linatarajia kufungua
milango ya fursa kwa wakazi wa mikoa ya Mtwara na Lindi katika kuziona
fursa kadhaa kwenye sekta ya Utalii na Uchumi.Tamasha hilo linatarajiwa
kufanyika kwa siku mbili kuanzia mwezi Agosti 16 na 17 mwaka huu kwenye
uwanja wa Nangwanda Sijaona ulipo Mtwara mjini. Mgeni
rasmi katika Tamasha hilo anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
huku likiwa na kauli mbiu isemayo ‘Fursa Zimefunguka, Tuzitambue,
Tujiandae, Tuzichangamkie.
Tamasha
hilo limeandaliwa kwa ushirikiano wa Tanzania Creative Industries
Network (TACIN) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) huku
likisaidiwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB). Akizungumzia Tamasha hilo
Mwenyekiti Mtendaji wa TACIN, Anic Kashasha alisema kuwa mikoa hiyo
inautajiri mkubwa katika utalii, uchumi na vivutio vingi mbalimbali.
"Mikoa
hiyo ina utajiri mkubwa tena sana katika rasilimai zake mbalimbali kama
vile fukwe nzuri na za kuvutia, utajiri mkubwa wa historia yake
utamaduni na hata ubunifu wa aina mbalimbali hivyo matamasha kama haya
yanasaidia kwa kiasi kikubwa kutangaza utajiri huo," alisema Kashasha.
Aliongeza kuwa, "Kwa sasa mikoa hiyo imeghunduliwa kuwa ina utajiri
mkubwa wa gesi na hivyo kuna watu mbalimbali wameshaajiliwa ikiwa pamoja
na kupatikana kwa fedha nyingi tayari kwa ajili ya maendeleo ya
wananchi wake na taifa zima kwa ujumla."
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu ya
TTB, Devota Mdachi alisema kuwa utalii umekuwa kwa kiasi kikubwa
ukisaidia maendeleo ya uchumi wa nchi. Anasema kuwa katika tamasha hilo
ambapo kutakuwa na shughuli mbalimbali za kiutamaduni, sanaa na
nyinginezo ni nafasi kubwa ya kukuza utalii pia hasa utalii wa ndani au
utalii wa kiutamadunia. "Ni nafasi kwao katika kutangaza mengi kuhusiana
na masuala ya Utalii, hapa nchini au hata utai wa shughuli za
kiutamaduni pia ni muhimu na hii ndio nafasi ya kipekee kwao na kwa
wadhamini mbalimbali kujitokeza kuunga mkono Tamasha hili la aina yake,"
alisema Mdachi.
Tamasha
hilo limedhaminiwa na Ofisa ya Mkuu wa Mkoa Mtwara, Mkuu wa Wilaya wa
Mtwara na Mikindani Baraza la Wilaya la Mtwara Vijijini, Baraza la
Biashara, KIlimo na Viwanda (TCCIA). Wengine ni Kampuni ya Magazeti ya
Serikali (TSN) Pride FM, Radio of Mtwara pamoja na Kampuni ya
Mawasiliano ya Strictly Communications.
Kuhusu TACIN:
TACIN ni
shirika lenye usajiri nchini lisilofungamana na upande wowote na lisilo
la kiserikari, au la kibiashara, lenye makao yake jijini Dar es salaam. Shilika hili huleta pamoja watanzania wenye uzalendo na nchi yao na wenye fani mbalimbali na uzowefu ambawo wamejiridhisha na Creative Industries kama muendelezo muhimu unaohitaji uangalizo makini.
No comments :
Post a Comment