Viongozi
na maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na wale wa NDC
wakipata maelezo kuhusu mradi wa makaa ya mawe Ngaka kutoka kwa Mtaalam
wa Kudhibiti Ubora (Quality Control Superintendent) Bw. Boscow R.
Mabena.
Timu
kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na NDC wakipata maelezo kutoka kwa
Meneja wa Kikundi cha Wanawake cha Mbalawala, Bi. Joyce Haule juu ya
matumizi ya makaa ya mawe majumbani. Makaa hayo hutumika majumbani kwa
kutumia majiko maalum baada ya kubadilishwa kitaalam na kuwa rafiki kwa
matumizi ya majumbani. Mbalawala kinajihusisha na shughuli mbalimbali za
maendeleo ikiwa ni jitihada za kumkwamua mwanamke kiuchumi.
Majiko maalum yanayotumia mkaa uliotokana na makaa ya mawe kwa ajili ya kupikia majumbani.
Mtaalam
wa Kudhibiti Ubora, Bw. Boscow R. Mabena akitoa maelezo namna ambavyo
Coal Briquett Machine (Pichani) hutumika kubadili makaa ya mawe kutoka
hali yake ya mwanzo baada ya kuchimbwa na kutengenezwa kwa ajili ya
matumizi ya nyumbani.
Katibu
Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango (ORTM), Dkt. Philip I. Mpango,
(wa tano kutoka kushoto) akikagua Mradi wa Makaa ya Mawe Ngaka. Wengine
ni viongozi na maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na Shirika
la Maendeleo la Taifa – NDC pamoja na wataalam wa kampuni ya TANCOAL
inayojishughulisha na uchimbaji wa makaa ya mawe.
Viongozi
na Maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na NDC wakiwa katika
picha ya pamoja na wataalam wa Kampuni ya TANCOAL ndani ya mgodi wa
makaa ya mawe. Kampuni ya TANCOAL ndiyo inayohusika nauchimbaji wa makaa
ya mawe katika Mradi wa Mkaa ya Mawe Ngaka. Picha na: Thomas Nyindo, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
No comments :
Post a Comment