Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Sunday, July 13, 2014

JK AVUKA MTO PANGANI


 —Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakiangalia mandhari ya mji wa Pangani wakati wa ziara ya kikazi wilayani humo.Sehemu kubwa ya mji huo imo katika hatari ya kumezwa na bahari kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na serikali imeahidi kujenga ukuta pembezoni mwa mto Pangani ili kuzuia athari za kimazingira kutokana na kuongezeka kwa kina cha maji.

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipitia moja ya hotuba zake akiwa ndani ya kivuko kipya cha MV Pangani II wakati akivuka mto Pangani kutoka Tarafa ya Bweni kuelekea Pangani mjini wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani Pangani jana(Jumamosi).Rais Kikwete ambaye alikuwa mkoani Tanga kwa ziara ya kikazi ya wiki moja alihitimisha ziara hiyo jana ambapo pamoja na mambo mengine alisema kuwa serikali itajenga kivuko kingine kwenye mto huo chenye uwezo mkubwa zaidi ili kuboresha shughuli za kiuchumi na kijamii wilayani humo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya majumuisho wakati akihitisha ziara yake ya kikazi ya wiki moja mkoani Tanga ambapo alizindua na kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo(picha na Freddy Maro)

No comments :

Post a Comment