Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Saturday, July 5, 2014

UZINDUZI WA ATM ZA SELCOM ZAFANA KATIKA VIWANJA VYA SABASABA


Meneja miradi wa kampuni ya Selcom Wireless, Gallus Runyela kulia akiwaelekeza kina mama waliotembelea kutoa pesa wakati wa uzinduzi wa mashine ya ATM ya kampuni hiyo ambazo zinatoa  pesa kwa kutumia mitandao mbalimbali ya simu kama M-pesa,tigo pesa,Airtel Money, walipo tembelea katika maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu JK Nyerere  kushoto ni Ester Kariwa na Joyce Mtema picha na mpiga picha wetu
Mmoja ya wateja waliotembelea banda la kampuni ya Selcom Wireless, Bi,Joriet Benjamin akichukuwa fedha zake katika ATM mashine mpya za kampuni hiyo wakati wa
maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu JK Nyerere
Wafanyakazi wa Selcom kampuni ya Wireless, wakiwa katika banda lao wakati wa
maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu JK Nyerere kutoka kushoto ni Juma Mgori Meneja ukuzaji biashara na masoko,Ofisa Mauzo Ally Mbaga na Meneja miradi wa kampuni hiyo Gallus Runyela

ATM mpya na za kisasa za selcom zawa kivutio kikubwa kwa kampuni ya selcom ambayo imekuwa ikijihusisha na utoaji wa malipo mbalimbali kama vile ving'amuzi na luku mwaka huu imezindua huduma yake mpya ya ATM ambazo zitakuwa zinatoa pesa kwa kutumia mitandao kama Mpesa,Tigo pesa,Airtel Money, na Easy pesa ATM hizo zimevuta hisia nyingi kwa watanzania baada ya kuziona kwa mara ya kwanza katika banda la Selcom na kushudia ATM hizo mpya na za kwanza nchini kutumika kutoa pesa kwa njia ya simu za mkononi
Meneja miradi wa kampuni ya Selcom Wireless, Gallus Runyela kulia akiwaelekeza Goerge Vupembe jinsi ya mashine zinavyofanya kazi
Ofisa Mauzo wa Kampuni ya Selcom Wireless  Ally Mbaga  kushoto akifurahia jambo na mteja, Bi, Rose Mombo aliyekuja kutoa pesa katika mashine ya ATM ya kampuni hiyo




Mtaalamu wa ufundi wa mashine za ATM za Selcom, Maful Awadhakitoa maherekezo ya jinsi ya kutumia mashine hizo
Meneja ukuzaji biashara na masoko  kampuni ya Selcom Wireless Juma Mgori akionesha mashine hiyo

Mtaalamu wa ufundi wa mashine za ATM za Selcom, Maful Awadh akiwa katika moja ya mashine hizo zilizozinduliwa katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es salaam
Meneja ukuzaji biashara na masoko
Juma Mgori akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mashine za ATM za kampuni hiyo kwa ajili ya kutolea fedha
kutumia mitandao kama Mpesa,Tigo pesa,Airtel Money, na Easy pesa ATM hizo zimevuta hisia nyingi kwa watanzania baada ya kuziona kwa mara ya kwanza katika banda la Selcom na kushudia ATM hizo mpya na za kwanza nchini kutumika kutoa pesa kwa njia ya simu za mkononi
Meneja miradi wa kampuni ya Selcom Wireless, Gallus Runyela kulia akihojiwa na waandishi wa habari kuhusu mashine hizo za ATM
wakati wa
maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu JK Nyerere

JK Atembelea Banda la Mambo ya Nje, Sabasaba


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Kikwete akiwasili kwenye Banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwenye viwanja vya Sabasaba

Rais Dkt. Kikwete akiweka saini kwenye kitabu cha wageni katika banda la Wizara ya Mambo ya Nje
Rais Kikwete (Mwenye Koti la Blue) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Taasisi zake.
Mtumishi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mbwana Msingwa akiweka saini katika kitabu cha wageni alipokuja na familia yake kwenye banda la Mambo ya nje lililopo kwenye viwanja vya sabasaba
Ankal akisalimiana na Afisa Mawasiliano Ally kondo, alitembelea Banda la Mambo ya Nje katika Viwanja vya Sabasaba. Picha na Reginald Philip

WAZIRI MEMBE AMTEMBELEA KADINALI PENGO NYUMBANI KWAKE KURASINI DAR LEO


 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard K. Membe, akizungumza na Polycarp Cardinal Pengo, wakati alipokwenda kumtembelea nyumbani kwake Kurasini jijini Dar es Salaam leo. 
Membe akiagana na Pengo, baada ya mazungumzo.

KIKWETE ATEMBELEA BANDA LA PSPF KATIKA MAONESHO YA SABASABA LEO


Rais Jakaya Kikwete, akipatiwa maelezo na Meneja Mawasiliano, Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Costantina Martin, alipotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu JK Nyerere jijini leo.
Rais Jakaya Kikwete, akipokewa na Meneja Mawasiliano, Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Costantina Martin, alipotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu JK Nyerere jijini leo.
 Rais Jakaya Kikwete, akisaini kitabu cha wageni, huku akipatiwa maelezo na Meneja Mawasiliano, Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Costantina Martin, alipotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu JK Nyerere jijini leo.

Friday, July 4, 2014

RAIS MSTAAFU ALI HASSAN MWINYI AZINDUA MSIKITI WA MASJIDIL HUDA CHAMAZI MBAGALA JIJINI DAR LEO


001
Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, akikata utepe kuzindua rasmi Msikiti wa ‘Masjidil Huda’ uliojengwa na mfanyabiashara maarufu nchini, Said Salim Bakhresa  katika eneo la Uwanja wa Chamazi, Mbagala jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti huyo wa Makampuni ya SSB, Said Salim Bakhresa, ambapo pia uzinduzi huo uliofanyika leo Julai 4, 2014, ulihudhuriwa na baadhi ya Viongozi wa Kiserikali akiwemo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na wengineo. 

02 (3) 4 (3)Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wa tatu kulia) Rais Mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi (wa pili kushoto) Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana ( wa pili kuli) Mwenyekiti wa Makampuni ya SSB, Said Salim Bakhresa (katikati) na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kushoto) wakijumuika na waumini wa dini ya Kiislam, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mkititi wa ‘Masjidil Huda’ na Swala ya Ijumaa uliofanyika leo Julai 4, 2014, Chamaz jijini Dar es Salaam. 
2 (4)Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na wenyeji wake wakati alipowasili Msikiti wa ‘Masjidil Huda’ uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuhudhuria uzinduzi wa msikiti huo uliofanyika leo Julai 4, 2014. 
1 (4)Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokelewa na Mwenyeji wake Mwenyekiti wa Makampuni ya SSB, Said Salim Bakhresa, wakati alipowasili Msikiti wa ‘Masjidil Huda’ uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuhudhuria uzinduzi wa msikiti huo uliofanyika leo Julai 4, 2014. Picha na OMR

TTCL YAFURAHIA KUIBUKA NA TUZO YA USHINDI KATIKA SEKTA YA MAWASILIANO


 Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Peter Ngota akionesha tuzo ya ushindi katika sekta ya mawasiliano.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya TTCL wanaoshiriki Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa wakipiga picha ya pamoja na tuzo yao mara baada ya kutwaa tuzo hiyo.Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya TTCL wanaoshiriki Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa wakipiga picha ya pamoja na tuzo yao mara baada ya kutwaa tuzo hiyo.
Muonekano wa Banda la TTCL kwenye Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba. Muonekano wa Banda la TTCL kwenye Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba.Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya TTCL wanaoshiriki Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa wakipiga picha ya pamoja na tuzo yao mara baada ya kutwaa tuzo hiyo.Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya TTCL wanaoshiriki Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa wakipiga picha ya pamoja na tuzo yao mara baada ya kutwaa tuzo hiyo katika sekta ya Mawasiliano.Banda la TTCL kwenye Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba. Banda la TTCL kwenye Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba.

KAMPUNI ya Simu Tanzania, TTCL imeshinda tuzo katika kundi la kampuni zinazotoa huduma za mawasiliano, kwenye Maonesho ya 38 ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam. 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi ndiye aliyemkabidhi tuzo hiyo,  Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Peter Ngota katika uzinduzi rasmi wa Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa jijini Dar es Salaam yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere. 

Ushindi wa TTCL unatokana na ubora wa huduma zinazotolewa na kampuni hiyo katika upande wa mawasiliano ya simu na pia mawasiliano ya intaneti "DATA". TTCL imesema ushindi huo umeipa hamasa ya kuendelea kubuni bidhaa ambazo zitakuwa chachu ya ukuaji uchumi nchini.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL, ABDULRAHMAN KINANA NA RAIS MSTAAFU, ALI HASSAN MWINYI WATEMBELEA GYM YA MAZOEZI YA TIMU YA AZAM FC, CHAMAZI



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana wakijaribu kufanya mazoezi katika mashine zilizo ndani ya Gym ya mazoezi ya timu ya Azam Fc, wakati walipotembelea Gym hiyo kujionea leo baada ya hafla ya uzinduzi wa Msikiti wa ‘Masjidil Huda’, kwenye Uwanja wa Chamazi, jijini Dar es Salaam, leo.
 Mkurugenzi wa Makampuni ya SSB, Said Mohamed, (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa viongozi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Mwenyekiti wa Makampuni ya SSB, Said Salim Bakhresa, wakati walipokuwa wakitembelea kujionea Uwanja wa Azam Complex, unaomilikiwa na timu ya Azam Fc, leo Chamazi.
 Wakitembelea Uwanja wa Chamazi, kujionea maendeleo ya timu ya Azam Fc , leo.
 Mkurugenzi wa Makampuni ya SSB, Said Mohamed, (kulia) akitoa maelezo kwa viongozi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi,  wakati walipokuwa wakitembelea kujionea Uwanja Gym ya mazoezi ya timu ya Azam Fc iliyopo kwenye Uwanja wa Azam Complex, unaomilikiwa na timu ya hiyo, leo Chamazi.
 Mkurugenzi wa Makampuni ya SSB, Said Mohamed, (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa viongozi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi,  wakati walipokuwa wakitembelea kujionea Uwanja Gym ya mazoezi ya timu ya Azam Fc iliyopo kwenye Uwanja wa Azam Complex, unaomilikiwa na timu ya hiyo, leo Chamazi.
''2015 DKT SLAA ATANIKOMA'' Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akijaribu kufanya zoezi katika moja ya mashine zilizo ndani ya Gym ya mazoezi ya timu ya Aazam Fc, kwenye Uwanja wa Chamazi Complex, wakati walipotembelea Gym hiyo leo. 

WAZIRI WA ULINZI WA CHINA AWASILI NCHINI



Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Watu wa China, Jenerali Chang Wanquan (Kulia) na waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk. Hussein Mwinyi wakikagua gwaride rasmi lililoandaliwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika viwanja vya Wizara ya Ulinzi na JKT, Dar es Salaam leo.(PICHA KWA HISANI YA JWTZ)

Thursday, July 3, 2014

Mambo yameiva ndani ya banda la MeTL Group kwenye maonyesho ya Sabasaba!



DSC_0004
Muonekano wa lango kuu la kuingia ndani ya banda la Makampuni ya MeTL Group kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yaliyozinduliwa rasmi jana kwa kupewa baraka na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Sefu Iddi katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
DSC_0008
Utajiuliza kwani LG wapo ndani ya Banda la MeTL Group kwenye maonyesho ya Sabasaba kwa sababu MeTL Group wamekuwa Mawakala waliothibitishwa Tanzania nzima (Authorized Dealers) kuuza vifaa vya LG nchini. USISAHAU KUJINADIKISHA KWA AJILI YA DROO YA BAHATI NASIBU ITAKAYOCHEZESHWA TAREHE 7 MWEZI HUU NDANI YA BANDA LETU…!
DSC_0120
Kampuni ya MeTL Group inahusika pia na masuala ya Vitenge, Khanga, Mashuka na n.k Njoo upendeze mwanamke na vitenge bora na imara kutoka MeTL Group…..Sikukuu ya Eid ilee na maandalizi yawe mapema kabisa…!
DSC_0125
Wakazi wa jiji la Dar wakivinjari ndani ya Banda la Mohammed Enterprises Tanzania Ltd. (MeTL Group) kujipatia mahitaji mbalimbali za bidhaa bora kabisa kwa bei nafuu msimu huu wa Sabasaba.
DSC_0151
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar wakiangalia na kupata maelezo ya  bidhaa mbalimbali kama  TV, Music System, Simu za mkononi za nyingine nyingi kutoka kampuni ya LG ambapo MeTL Group ndio Authorized Dealers pekee nchini Tanzania.
DSC_0124
Muonekano wa ndani wa Banda letu la MeTL Group ukiwa umenakshiwa kwa mabango pamoja na TV za LG zinazoonyesha matangazo mbalimbali ya bidhaa zetu.
DSC_0136
Mmoja wa wateja akipata maelezo kutoka kwa wataalamu wetu waliobobea wa vipozi kwenye banda letu la MeTL Group.

OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO YAKAGUA MRADI WA MAKAA YA MAWE NGAKA




Viongozi na maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na wale wa NDC wakipata maelezo kuhusu mradi wa makaa ya mawe Ngaka kutoka kwa Mtaalam wa Kudhibiti Ubora (Quality Control Superintendent) Bw. Boscow R. Mabena.
Timu kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na NDC wakipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kikundi cha Wanawake cha Mbalawala, Bi. Joyce Haule juu ya matumizi ya makaa ya mawe majumbani. Makaa hayo hutumika majumbani kwa kutumia majiko maalum baada ya kubadilishwa kitaalam na kuwa rafiki kwa matumizi ya majumbani. Mbalawala kinajihusisha na shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwa ni jitihada za kumkwamua mwanamke kiuchumi.
Majiko maalum yanayotumia mkaa uliotokana na makaa ya mawe kwa ajili ya kupikia majumbani.
Mtaalam wa Kudhibiti Ubora, Bw. Boscow R. Mabena akitoa maelezo namna ambavyo Coal Briquett Machine (Pichani) hutumika kubadili makaa ya mawe kutoka hali yake ya mwanzo baada ya kuchimbwa na kutengenezwa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.
Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango (ORTM), Dkt. Philip I. Mpango, (wa tano kutoka kushoto) akikagua Mradi wa Makaa ya Mawe Ngaka. Wengine ni viongozi na maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na Shirika la Maendeleo la Taifa – NDC pamoja na wataalam wa kampuni ya TANCOAL inayojishughulisha na uchimbaji wa makaa ya mawe. 
Viongozi na Maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na NDC wakiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa Kampuni ya TANCOAL ndani ya mgodi wa makaa ya mawe. Kampuni ya TANCOAL ndiyo inayohusika nauchimbaji wa makaa ya mawe katika Mradi wa Mkaa ya Mawe Ngaka. Picha na: Thomas Nyindo, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.