Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari Tigo yawazawadia washindi wa promosheni ya “ZAMU YAKO KUSHINDA” 20 Desemba, 2011, Dar es Salaam. Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imewazawadia washindi watano, kila mmoja shilingi milioni nne, (Tsh. 4,000,000/-) kama washindi wa kwanza wa kila siku ambao wamepatikana ndani ya muda wa siku tano, katika promosheni ya inayoendelea ya Zamu yako Kushinda. Halikadhalika washindi wengine kumi wamezawadiwa kompyuta aina ya laptop Washindi hawa wote wamepatikana ndani ya kipindi cha muda wa siku tano.promosheni hii bado inaendelea hadi Feb. 19, 2011. Utaratibu wa kupata washindi ulifayika kwa kufanya droo inayofanywa na kampuni ya Tigo chini ya usimamizi wa wa Bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha. Afisa Uhusiano wa wa Tigo Alice Maro alisema kuwa promosheni hii ni kubwa na kuwa bado kuna washindi wengine ambao watazawadiwa wiki ijayo. Washindi wa Tsh. 4,000,000/- ni Issa Juma (Dar es Salaam), Sultani Mohammed (Songea), Idrissa Ally (Dar es Salaam), Ally Hassan (Dodoma), na Kusena Nicodemus Sospeter kutoka Iringa. Washindi wa lap top ni Pilly Bwela (Dar es Salaam), Mwakatage Sunday John (Dar es Salaam), Juma Lyimo (Dar es Salaam), Saugo Mwachengula Ndemo (Iringa), Rajab Abdul (Dar es Salaam), Furaha John Mahui (Dar es Salaam) Deogratius John (Dodoma), Felix Frank (Dodoma), Emmanuel Dodoma (Kilimanjaro) na Viren Ehijha (Dar es Salaam). Ili kushiriki mtumiaji wa Tigo anatakiwa kutuma neno “TIGO” kwenda 15571. Gharama kwa kila ujumbe ni Tsh 450. Washiriki wanatakiwa kujikusanyia pointi nyingi ili kujiwekea mazingira mazuri ya kujishindia zawadi. Washiriki pia watazawadiwa zawadi za kutuma ujumbe wa bure kutoka Tigo kwenda Tigo. Watumiaji wa mtandao wa Tigo wenye umri chini ya miaka 18, hawaruhusiwi kushiriki. Promosheni hii ni kwa ajili watumiaji wa Tigo walioko nchini Tanzania tu.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
9 hours ago
No comments :
Post a Comment