Rais wa tff tenga kulia akiwa na mkurugenzi wa ufundi sunday kayuni.
Shirikisho la soka nchini TFF limemsimamisha kazi Afisa habari wake FLORIAN KAIJAGE kutokana na tuhuma za uzembe uliochangia kushindwa kukamilishwa kwa itifaki ya kupigwa kwa nyimbo za taifa katika mchezo kati ya TAIFA STARS dhidi ya MOROCCO uliofanyika siku ya Jumamosi.
Rais wa shirikisho la soka hapa nchini-TFF- LEODGAR TENGA amemwomba radhi rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, JAKAYA MRISHO KIKWETE,serikali ya MOROCCO, mashabiki waliokuja uwanjani siku ile na WATANZANIA kwa ujumla kwa tukio hilo.
Aidha TENGA anasema hatua ya kumsimamisha kazi KAIJAGE imechukuliwa ili kutafuta chanzo cha sababu zilizopelekea kushindwa kupigwa kwa nyimbo za TAIFA siku hiyo na TFF imeunda tume maalumu kuchunguza suala hilo.
Kufuatia kutokea kwa tatizo la kugoma kwa wimbo wa taifa mara kwa mara TFF imeamua kuanzia sasa kutumia bendi ya polisi -‘BRASS BAND’ kama njia mbadala ya kucheza nyimbo za taifa pindi timu ya taifa inapocheza na timu ya taifa jingine.
Wakati huohuo TFF imeahidi kukaa meza moja na vyombo vya habari kutatua
kasoro zilizojitokeza katika mechi iliyopita ambapo waandishi wa habari walilazimika kuingia uwanjani kwa kutumia tiketi badala ya utaratibu uliozoeleka wa kutumuia kadi maalumu.
ALIYEKUWA MSEMAJI WA TFF KAIJAGE.
No comments :
Post a Comment