TASWA YAIJIA JUU TFF JUU YA UINGIAJI WA WANAHABARI KATIKA MECHI
Katika hatua nyingine CHAMA cha waandishi wa habari za michezo TASWA na kinakusudia kuvunja uhusiano wake na shirikisho la soka nchini TFF endapo halitafuata maelekezo ya mapendekezo yao ya waandishi wa habari kuingia uwanjani bila kuwa na utaratibu wenye kikwanzo.
Taarifa ya TASWA iliyosambazwa na katibu mkuu wa chama hicho, AMIR MHANDO ametaja mapendekezo ya makubaliano ya kikao chao na baadhi ya wahariri wa habari nchini na kubainisha kuwa endapo TFF itapuuza mapendekezo yao.
Miongoni mwa mapendekezo waliyotaka kutekelezwa ni pamoja na TFF itenge tiketi 120 kwa ajili ya wanahabari kuanzia mchezo wa kesho kati ya TAIFA STARS na MOROCCO na si tiketi SABINI ambazo TFF ilibainisha kuzitoa katika mchezo huo.
BALOZI WA JAPAN AKABIDHI MIPIRA OFISI YA TAMISEMI
Balozi wa japan akitoa mipira
naibu katibu mkuu tamisemi akikabidhi mipira kwa mmoja wa viongozi kutoka namtumbo.
BALOZI wa JAPAN nchini TANZANIA, HIROSHI NAKAGAWA amekabidhi mipira MIA MBILI ya soka kwaajili ya watoto wa shule za wilaya ya NAMTUMBO mipira ambayo ilitolewa na wananchi WANNE wa JAPAN kuunga mkono maendeleo ya mchezo huo nchini.
Wakati akikabidhi mipira hiyo, Naibu katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Jumanne Sagini na kutaka mipira hiyo iwafikie walengwa
SAGINI, ameonyesha imani ya kuwa na wachezaji wa baadae wenye vipaji na hakusita kumweleza balozi HIROSHI NAKAGAWA kuwa mchezo wa soka ni moja kati ya michezo inayotoa ajira kwa vijana wengi nchini ndo mana serikali imeamua kurudisha michezo ya UMISETA na UMITASHUMTA kwani vipaji huanza kuonekana tangu utotoni.
MOROCCO WAINGIA DSM KWA KASI YA AJABU
mazoezi kama kawaida
mazoezi kama kawa
morocco wakiwa mazoezini
No comments :
Post a Comment