Watoto 14 kutoka mjini Mombasa, Kenya, wenye umri wa chini ya miaka 13, wamekuwa nchini Uingereza kushiriki katika mechi kadhaa za kandanda.
Kundi hilo la watoto likifahamika kwa jina la Coastal Kings, yaani Wafalme wa Pwani, liliweza kupambana katika soka na watoto wa shule ya Uingereza ya Elstree.
Katika kipindi cha wiki moja, watoto hao waliweza kupata jumla ya magoli tisa, na muhimu zaidi, kupata marafiki watakaodumu katika maisha yao yote.
Vijana hao waliweza kutoka sare katika mechi tatu, na kupata ushindi katika moja.
Mwalimu mkuu wa shule ya Elstree, Mark Sayer, alisema alipendezwa mno na namna vijana hao kwa upesi walivyoweza kujumuika katika jamii ya Elstree.
Mara tu walipofika walishangazwa na maisha ya Elstree, lakini baada ya muda mfupi tu, waliweza kwa ujasiri mkubwa kuyazoea masiha ya Elstree.
Safari ya vijana hao nchini Uingereza ilipangwa na shirika linalofahamika kama Touraid.
No comments :
Post a Comment