Afisa
Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde akimkabithi mshindi wa Airtel
Mkwanjika Diana Samwel na mkazi wa Dar es Saalam pesa taslimu mara baada
ya kujinyakulia shilingi 480,000 kupitia boksi la Airtel Mkwanjika.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
· Zaidi ya wateja 212 wajishindia pesa taslimi
Dar es Salaam
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel leo imechezesha droo ya mwisho ya
promosheni ya Airtel Mkwanjika nakupata washindi 40 ambapo kila mmoja
atajishindia pesa taslimu hadi shilingi milioni 1 kupitia boksi la
Airtel Mkwanjika
Promosheni
ya Airtel Mkwanjika ilizinduliwa mwishoni mwa mwezi Disemba na
kuwazawadia wateja wanne watakaojiunga na vifurushi vya yatosha au
kuongeza muda wa maongezi kupitia vocha au Airtel Money kila siku.
Jumla ya washindi 28 walipatikana kupitia droo kila wiki na kuzawadiwa
pesa taslimu.
Akiongea
wakati wa kuchezesha droo ya mwisho, Afisa Uhusiano wa Airtel, Bi Jane
Matinde alisema” Leo tumefikia mwisho wa promosheni yetu ya Airtel
Mkwanjika , promosheni ambayo imeweza kuwazawadia wateja zaidi ya 212.
nchi
nzima. Tunajisikia furaha kuona mwitikio mkubwa kutoka kwa wateja
wetu na tunapenda kuwahakikishia kuwa Airtel itaendelea kutoa huduma
bora za kibunifu zinazokidhi mahitaji ya wateja wetu yanayoendelea
kubadilika na kukua kila siku na huku tukiendelea kuwazawadia kupitia
promosheni kama hii ya Airtel Mkwanjika”
“Tunaamini
kupitia Airtel Mkwanjika tumetoa zawadi ambazo zimewawezesha wateja
wetu kukabiliana na changamoto walizonazo na kuwasaidia kuongeza mitaji
ya biashara zao na kuongeza ufanisi katika shughuli zao mbalimbali za
kiuchumi na za kijamii. Tunaamini washindi wetu watakuwa ni ushuhuda
tosha wa namna gani Airtel kupitia promosheni hii imeweza kubadili
maisha yao na ya jamii zao kwa ujumla. Aliongeza Matinde
Promosheni
ya Airtel Mkwanjika imefikia mwisho, Airtel bado itaendelea kuwawezesha
washindi kutoka katika mikoa mbalimbali nchini ambao bado hawajaingia
kwenye boksi la Airtel Mkwanjika kupata nafasi ya kufanya hivyo ili
kuweza kujiokotea pesa na kukabithiwa zawadi zao.
No comments :
Post a Comment