Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu ya
Tigo, Diego Gutierrez akizungumza na waandishi wa habari na wageni
waalikwa mbalimbali wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo uliofanyika jana
Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam .
Wafanyakazi wa Tigo na wanahabari
kutoka vyombo mbalimbali wakifurahia jambo wa uzinduzi wa huduma ya
whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt
Regency Jijini Dar es salaam
Hapa kila mgeni mualikwa akiwa busy na simu yake kwenye uzinduzi huo.
Ni kama wanasema ‘tumependeza
sana ngoja tujipige picha’ wakati wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure
kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency
Jijini Dar es salaam.
Wageni waaalikwa wakiwa katika
maski za ” Emojis ” wakifurahia jambo kwenye uzinduzi huduma ya whatsapp
bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency
Jijini Dar es salaam
Hapa ni furaha tupu kwa wanahabari.
Washereheshaji katika uzinduzi
huo,Mc Taji Liundi na Mc Abby wakitoa maelezo jinsi gani wateja wa Tigo
watakavyofurahia huduma ya whatsapp bure.
Burudani ikiendelea kutoka kwa
wasanii wa kikundi maalum cha maonesho ya jukwaa wakati wa uzinduzi wa
huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika
hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez (katikati),
akiwa na viongozi wenzake kutoka tigo katika maski za “Emojis ” wakati
wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika
jana katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu ya
Tigo, Diego Gutierrez (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na
washereheshaji MC Taji Liundi na MC Abby wakati wa uzinduzi wa huduma ya
whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya
Hyatt Regency Jijini Dar es salaam.
Ofisa
Mkuu wa Biashara wa Tigo, Shavkat Berdiev (kushoto ) Meneja wa gharama
wa Tigo Jakhangic Tulaganov na Meneja masoko Olivier prentout
wakifurahia jambo wakati wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa
wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency
Bloggers
wakiwa katika picha ya pamoja na msanii Lucas Muhuvile ‘Joti’ wakati wa
uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika
jana katika hotel ya Hyatt Regency.
………………………………………………………………….
Dar es Salaam, Februari 2, 2016- Kampuni ya Tigo Tanzania ambayo inaongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali imetangaza huduma ya bure ya WhatsApp kwa watumiaji wa huduma hiyo ikiwa ni mara ya kwanza kwa kampuni ya simu kutoa ofa ya bure ya mtandao huo wa jamii nchini.
Dar es Salaam, Februari 2, 2016- Kampuni ya Tigo Tanzania ambayo inaongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali imetangaza huduma ya bure ya WhatsApp kwa watumiaji wa huduma hiyo ikiwa ni mara ya kwanza kwa kampuni ya simu kutoa ofa ya bure ya mtandao huo wa jamii nchini.
Akitangaza
upatikanaji bure wa huduma hiyo kwa vyombo vya habarijijini Dar es
Salaam, Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez amesema kuwa wateja wote wa
Tigo wanaotumia vifurushi vya intaneti vya kampuni hiyo kwa wiki na
mwezi watapata huduma ya WhatsApp bure. Tigo ina wateja zaidi ya milioni
10.
Huduma
ya WhatsApp ambayo ni maarufu kwenye kutuma ujumbe kwa njia ya simu,
ina watumiaji zaidi ya milioni nane nchini Tanzania na duniani inatumiwa
na watu wapatao milioni 900. WhatsApp inawezesha watumiaji
kubadilishana habari, ujumbe, video na miito ya sauti.
“Kuanzia
sasa na kuendelea wateja wote wa Tigo wanaonunua vifurushi vyetu vya
wiki au mwezi watakuwa na fursa ya kufurahia WhatsApp BURE. Hili
linawezekana kama mteja ana smartphone. Huduma ya bure ya WhatsApp kwa
wateja wetu inaonesha jinsi tulivyojikita katika kuboresha mabadiliko
kwenye maisha ya kidijitali na hivyo kuongoza kwenye kutoa teknolojia ya
hali ya juu pamoja na ubunifu”, alisema Gutierrez.
Kwa
Mujibu wa Gutierrez, ili kufurahia huduma hii, jambo analohitaji mteja
wa Tigo ni kuwa na kifurushi cha intaneti cha wiki au mwezi ambacho
anaweza kukipata kupitia *148*00# à Tigo-Tigo Xtreme/MiniKabangà Wiki au
Mwezi + WHATSAPP YA BURE. Huduma hii inapatikana kwa wanaomiliki simu
za aina ya Blackberry, Android na Nokia Symbian60.
WhatsApp ni huduma dada na huduma huduma Facebook ambayo iliingia makubaliano na Tigo mwaka 2014 na kuwapa fursa wateja wa Tigo huduma ya Facebook bure na kwa lugha ya Kiswahili kupitia simu zao.
WhatsApp ni huduma dada na huduma huduma Facebook ambayo iliingia makubaliano na Tigo mwaka 2014 na kuwapa fursa wateja wa Tigo huduma ya Facebook bure na kwa lugha ya Kiswahili kupitia simu zao.
No comments :
Post a Comment