Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, February 19, 2016

Tigo yatoa msaada wa millioni 10/- kwa waathirika wa mafuriko mjini Iringa


Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kusini, Jackson Kiswaga, akikabidhi msaada wa mabati kwa Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh Amina Masenza (katikati) , ikiwa pamoja  na msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye thamani ya millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika kata za Pawaga na Idodi,  mkoani Iringa,wanaoshuhudia pembeni ni viongozi kutoka serikalini  makabidhiano hayo yalifanyika jana . 
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kusini, Jackson Kiswaga, akikabidhi msaada wa magodoro  kwa Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh Amina Masenza (katikati) ikiwa pamoja  na msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye thamani ya millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika kata za Pawaga na Idodi,  mkoani Iringa,wanaoshuhudia pembeni ni viongozi kutoka serikalini  makabidhiano hayo yalifanyika jana .

Magodoro waliyokabidhi tigo ikiwa ni ikiwa pamoja  na msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye thamani ya millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika kata za Pawaga na Idodi,  mkoani Iringa, makabidhiano hayo yalifanyika jana .

Wafanyakazi wa Tigo wakisaidia kushusha mabati yaliyotolewa na Tigo ikiwa pamoja  na msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye thamani ya millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika kata za Pawaga na Idodi,  mkoani Iringa, makabidhiano hayo yalifanyika jana
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kusini, Jackson Kiswaga, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi misaada kwa  Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh Amina Masenza (kushoto) , ikiwa pamoja  na msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye thamani ya millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika kata za Pawaga na Idodi,  mkoani Iringa, makabidhiano hayo yalifanyika jana .

XXXXXXXXXXXXXXXXX

Iringa, Februari 17, 2016:  Tigo imetoa msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye thamani ya millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika wodi za Pawaga na Idodi, iliyosababisha watu wengi kukosa sehemu za kulala, mkoani Iringa.

Vifaa hivyo vilikabidhiwa leo kwa waathirika wa mafuriko na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kusini Jackson Kiswaga, aliesisitiza ahadi ya kampuni kusimama kidete na wananchi katika wakati wa faraja na shida.
“Tupo hapa kujumuika na wasamaria wema wengine katika kuwapa pole walioathirika na maafa hayo, na tunawaombea kila la kheri waweze kurudi katika hali tulivu baada ya kupoteza wapenzi wao na mali zao,” Alisema Kiswaga

Vifaa vilivyo tolewa na Tigo ni mabati 350, magodoro 30 na mashuka 35.

Mvua zilizonyesha katika wodi hizo, iliripotiwa kwamba zilisababisha watu 1,155 kukosa sehemu za kulala, na pia mimea na makazi ya watu yaliharibika au kubebwa na mafuriko, taarifa hii ni kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa Iringa mhe.Amina Masenza.

Msaada kutoka Tigo, kulingana na Kiswaga, ni katika mpango wake wa uwajibikaji kwa jamii, sera hii ni ahadi kwa ajili ya kuwekeza baadhi ya rasilimali za kampuni katika miradi ya kuendeleza na pia katika kusaidia jamii majanga yanapo ibuka.

No comments :

Post a Comment