Mkurugenzi wa
Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya akimpongeza Mpigapicha
za habari wa The Guardian Ltd na Media Solutions , John Badi baada
ya kuibuka mshindi wa tiketi ya bure ya fastjet wakati wa uzinduzi wa
ubia wa kampuni ya Airtel na Fastjet utakaowawezesha wateja kulipia tiketi zao
za ndege kupitia huduma ya Airtel Money
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
· Lipa
tiketi ya Fastjet kwa Airtel Money upate tiketi ya bure
Dar es Salaam Machi 01, 2016- Kampuni ya ndege ya
ki-Afrika yenye gharama nafuu Fastjet, imekuwa ya kwanza kuingia kwenye
makubaliano na kampuni ya simu ya Airtel Tanzania ambapo wateja wa Fastjet
wataanza kununua tiketi na hata kufanya miamala mingine kupitia Airtel Money.
Kutokana na makubaliano hayo,
wateja wa fastjet watakaoununua tiketi kupitia Airtel Money, watapata nafasi ya
kushinda tiketi ya kusafiri wa ndani na nje ya nchi kupitia droo ambayo
itafanywa kwa miezi miwili.
Akitangaza kusainiwa kwa
makubaliano hayo, Meneja Mkuu wa Fastjet Tanzania, John Corse alisema: “ukweli
kwamba wateja wetu watamudu kupata tiketi zao kupitia Airtel Money kunaimarisha
kujituma kwetu katika kuhakikisha kuwa Fastjet inaishi kulingana na
ahadi yake ya kuwa shirika lisilo na usumbufu linalofanya safari za wateja wake
kuwa ni rahisi.
Alisema kuwa huduma hiyo ambayo
inampa mteja uhakika wa kupata tiketi za Fastjet kutoka mahali alipo kwa
kutumia simu za mkononi, itaanza Machi 03, 2016 na kuongeza kuwa
mpango huo mpya wa kushirikiana na Airtel sio tu kwamba utahakikisha
kuwa huduma inakuwa ya kasi na ya ufanisi bali pia itaondoa kabisa kadhia ya
kupoteza muda miongoni mwa wateja walipokuwa wanakwenda kununua tiketi kutoka
kwa mawakala wa Fastjet waliopo mbali na makazi yao.
“Tunajivunia mno na tunawashukuru
wateja wetu ambao wamekuwa wakituunga mkono na tunaahidi kuendelea kuwapa
huduma zetu zenye ubora wa hali ya juu pamoja na kusikiliza mahitaji ya wateja
wetu,” alisema Corse.
Akizungumza kuhusu makubaliano
hayo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice
Singano Mallya alisema: “ushirikiano huu umekuwa ni njia sahihi kwa wateja
wetu ya kulipia tiketi kwa safari zao za ndani na za kimataifa wakati wowote,
mahali popote kwa utulivu wakiwa majumbani kwa kutumia simu ya
mkononi.
“Tunaamini wateja wetu wa
Airtel Money kote nchini hivi sasa
watafurahia njia hii ya haraka na rahisi kulipia na
hali kadhalika kupanga safari zao na Fastjet katika mazingira ya
utulivu.”
Aliongeza kusema, “Airtel
itaendelea kuonesha kujituma kwake katika kutoa bidhaa na huduma
zilizojikita kwenye ubunifu, kuanzisha ushirikiano ambao ni muhimu na
utakaokidhi mahitaji ya wateja kupitia huduma za Airtel
Money wakati wowote.”
Akiongelea promosheni hiyo, Meneja
wa Airtel Money, Asupya Naligingwa alisema, “tutakuwa tunatoa zawadi kwa wateja
watakaonunua tiketi za fastjet kupitia Airtel Money kila baada ya wiki mbili
kwa miezi miwili. Tiketi hizi zitatolewa kupitia droo ambapo kumi na sita
zitakuwa za safari za ndani ya nchi na nne zitakuwa za safari za nje ya nchi.
Tunawaomba wateja kununua tiketi kupitia Airtel Money ili wapate nafasi ya
kushinda tiketi za safari wazipendazo”, alisema Nalingiwa.
Nalingiwa alibainisha: “Ili
kulipia tiketi, mteja anatakiwa kupiga: *150*60*#, halafu chagua, ‘lipia bili’,
halafu, ‘chagua kwenye orodha’, halafu chagua, ‘Usafiri wa anga’, kisha ufuate
maagizo”.
Kuhusu Bharti Airtel
Bharti Airtel Limited ni kampuni
ya mawasiliano ya simu inayoongoza duniani ikiwa inafanya
shughuli zake miongoni mwa nchi 20 barani Asia na Afrika.
Makao yake makuu ni New Delhi, India, ikiwa ni kampuni inayoshika nafasi ya
tatu miongoni mwa makapauni yanayotoa huduma ya simu duniani. Nchini
India, kampuni inatoa bidhaa mbalimbali zikiwemo huduma za intaneti
bila nyaya za 2G, 3G na 4G, biashara kwa njia ya simu, huduma za njia ya simu,
huduma ya kasi ya DSL broadband, IPTV, DTH, huduma za
ujasiriamali zikiwemo huduma ya usafirishaji masafa
marefu kitaifa na kimataifa. Kwenye maeneo mengine ya kijiografia inatoa
huduma za intaneti bila nyaya na biashara kwa njia ya simu. Bharti Airtel
ilikuwa na wateja zaidi ya milioni 335 kwenye maeneo inakoendesha shughuli
zake hadi kufikia mwishoni mwa Agosti 2015. Ili kufahamu zaidi tembelea wavuti
wake, www.airtel.com
Kuhusu Fastjet Tanzania
Fastjet Tanzania ni kampuni ya
ndege yenye gharama nafuu iliyoanza safari zake nchi Tanznaia November 2012.
Kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya usalama, ubora, ulinzi na uhakika ,
Fastjet imeleta uzoefu mpya wa kusafiri kwenye soko la Afrika katika kiwango
cha bei ya chini. Kwa kutumia ndege zake za Airbus A319
Fastjet imekuwa inatumia bei ya chini Afrika na mikakati yake ya
muda mrefu ni kuwa kampuni ya kwanza ya ndege Afrika ya gharama nafuu.
Matokeo ya utafiti kuhusu
kuridhika kwa wateja yanaonesha kuwa asilimia 100 ya wateja wanaweza kusema
kuwa wanapendezeshwa na huduma za Fastjet. Katika kuendeleza nembo na
utambulisho wake, Fastjet imeshateuliwa kwa ajili ya tuzo kadhaa, ukiwemo
ushindi wa tuzo tatu za ‘kujisuka upya ki-biashara’ (re-branding) na uzinduzi
wa Fastjet ambayo unafahamika kama "Brand Strategy of the
Year" uliyopatikana kwenye Tuzo za Masoko za Drum jijini London
na Tuzo ya Mbunifu wa Usafiri kwenye Tuzo za Nane za Usafiri Afrika
2015 Johannesburg.
No comments :
Post a Comment