Na Elizabeth John
MKALI wa muziki wa kizazi kipya
nchini, Juma Awadhi ‘Blad Key’, amewataka wapenzi wa kazi zake kukaa mkao wa
kula kwa ajili ya burudani ambazo amewaandalia na kwamba anakuja na staili mpya.
Licha ya kuwa na vibao vingi, Blad
Key alishawahi kutamba na kibao chake cha ‘Vimepanda Bei’ ambacho
kilimtambulisha na kufanya vizuri katika soko la muziki huo.
Akizungumza Dar es Salaam,
Blad Key alisema ana nyimbo tatu ambazo tayari amezitengeneza na yuko katika
mchakato wa kuchagua ipi itangulie na ipi ifuate.
“Nimetengeneza nyimbo tatu kwa
mpigo zenye ujumbe tofauti, sijajua ni ipi itangulie kutoka na bado sijazipatia
majina; nafikiri wiki ijayo nitakuwa nishazitafutia majina,” alisema Abdukiba.
Aliwaomba mashabiki wake wakae
mkao wa kula kwa ajili ya kuzipokea kazi hizo, ambazo ana uhakika zitafanya
vizuri kutokana na ujumbe ulioko ndani yake.
No comments :
Post a Comment