Washindi waliokabidhiwa zawadi zao za pesa taslimu ambazo ni sh. 500,000/- kwa kila mmoja ni wale ambao ni wakazi wa jijini la Dar es Salaam wakati washindi wa kutoka nje ya Dar es Salaam taratibu za kuwakabidhi zawadi zao zinafanyika kuhakikisha kuwa nao pia wanakabidhiwa zawadi zao.
Washindi waliokabidhiwa zawadi ni Mashimba Mashimba, Chemu Hassani, Philip Masonda, Osole David Gilina, Godwin Joseph na Enock Dodan. Washindi hawa ni kati ya washindi 19 waliojishindia fedha taslimu ambazo jumla yake ni sh. Milioni 9.5 kutoka Zain.
Tangu kuanza kwa promosheni , Jumla ya washindi 26 kutoka mikoa mbalimbali wamejishindia zawadi mbalimbali zikiwemo Bajaj, baiskeli, na tiketi ya kushuhudia kombe la Dunia.
Meneja Masoko wa Zain Tanzania Costantine Magavilla alisema kuwa promosheni hiyo inaendelea kuchezeshwa ambapo washindi wataendelea kujishindia Zawadi mbalimbali kutoka Kampuni ya Simu za mkononi ya Zain Tanzania.
“Na leo hii kwa mara ya kwanza pia mtaweza kushuhudia tukimpa mshindi mwingine ambaye anajishindia tiketi ya kwenda kushuhudia kombe la Dunia, akiwa amelipiwa gharama zote yeye na mtu mwingine atakayemchagua kwenda naye, Kabla na baada kuisha kwa mwezi huu wa sita, tukiwa tumepata watanzania 12 watakaokwenda kushuhudia kombe la dunia nchini Afrika ya Kusini,”alisema Magavilla
Katika Promosheni ya JIVUNIE SMS kampuni ya Zain itatoa bajaj 10, baiskeli Toyota Corola 5, tiketi 12 za kushuhudia fainali za kombe la Dunia pamoja na fedha Taslimu 500,000/- kwa mshindi mmoja kwa kila siku. Zawadi kubwa katika promosheni hii itakuwa ni gari aina ya RAV 4 SUV.
Ili kushiriki katika promosheni hii ambayo inaendeshwa katika stahili ambayo mshiriki anajikusanyia pointi kutokana na maswali aliyoyajibu, mteja wa Zain anatakiwa kujisajili kwa kutuma neno JIVUNIE kwenda namba 15656.
Baada ya hapo mteja atapata ujumbe wa kumtaarifu kuwa sasa amesajiliwa na swali la kwanza litafuatia na maswali mengine pia yataendelea kuulizwa ambapo mshindi atapata pointi kutokana na kujibu majibu kwa usahihi.
Pointi za upendeleo zinatolewa endapo mshiriki atakuwa amefikia kiwango cha pointi ambazo zinatakiwa, na hii inaweza kumpa nafasi ya ushindi zaidi mshiriki na kujinyakulia zawadi za kila siku na zile za mwisho wa wiki.
No comments :
Post a Comment