Airtel Yaunganika na Afrika – Yakamilisha makubaliano ya kibiashara ya kuvuka mipaka makubwa kuliko yote katika masoko yanayoendelea
Imeingia Ligi ya simu tano za mkononi zinazoongoza duniani
Nembo ya Airtel sasa yaenda kimataifa ikiwafikia watu bilioni 1.8
Yasisitiza nia yake kwa Afrika na Yaahidi huduma za bei nafuu, kusambaza mtandao na kutoa huduma kabambe
Yazishukuru serikali za nchi 15 Afrika kwa kuiunga mkono
New Delhi, Juni 8, 2010: Bharti Airtel Limited (“Bharti”) leo imechukua hatua kubwa ya kuelekea kuwa kampuni ya simu za mkononi ya kimataifa baada ya kukamilisha ununuzi wa shughuli za biashara ya Zain Group (Zain) katika nchi 15 Afrika kwa gharama ya dola za Marekani bilioni 10.7. Kwa ununuzi huu, chapa ya Airtel sasa itakuwa ya kimataifa ikiwa inawafikia zaidi ya watu 1.8 bilion barani Asia na Afrika na wateja wakiwa zaidi ya milioni 180.Makubaliano haya ya kibiashara ya kuvuka mipaka ni makubwa kuliko yote katika masoko yanayoendelea na yatapelekea kupatikana kwa mapato ya zaidi ya dola za Marekani bilioni 12.4 na mapato kabla ya riba, kodi, uchakavu (EBITDA) ya zaidi ya dola za Marekani bilioni 4.7, kwa kuzingatia mahesabu ya mwisho. Bharti sasa ni miongoni mwa makampuni matano makubwa ya simu za mkononi duniani.
Bw. Sunil Bharti Mittal, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Bharti amesema, “Tumefurahi kukamilisha makubaliano haya kwa ajili ya India na Bharti. Tunapenda kuzishukuru kwa dhati serikali za nchi zote 15 pamoja na serikali ya India kwa kutuunga mkono katika hatua hii muhimu. Na hii itakuza zaidi uhusiano wa kihistoria baina ya India na Afrika katika masuala ya kiuchumi na kijamii na kupelekea kuboresha ushirikiano kati ya Kusini na Kusini.Bharti, ambayo imekuwa ikijizatiti kufikia dira yake ya kusambaa Afrika, imedhamiria kuchangia kukua kwa mawasiliano ya simu katika bara kwa kusambaza huduma ndani ya nchi hizo na kutoa huduma zenye bei nafuu ambazo zinawagusa watu wa kawaida. Pia tunawaadhidi wateja wetu wa Afrika mambo kabambe na bidhaa na huduma kadhaa zenye ubunifu wa hali ya juu.
Tunapenda kuwakaribisha zaidi ya wafanyakazi 6500 wenye vipaji na taaluma ya hali ya juu kwenye familia ya Bharti na tunasubiri kwa hamu kufanya kazi nao kupeleka kampuni zao kwenye hatua nyingine ya mafanikio. Tunapenda kuishukuru timu ya Zain kwa utaalamu wao, ambao umetuwezesha kukamilisha makubaliano haya katika muda unaoweka rekodi.’’
Bw. Asaad Al-Banwan, Mwenyekiti, Zain, said “Tunawatakia mafanikio makubwa Bharti Airtel katika kuendeleza kukua kwa mawasiliano ya simu katika bara la Afrika na tunauhakika watu wa Afrika wataipokea kampuni yenye nia dhabiti na inayotambulika duniani.’’Ununuzi wa Bharti wa shughuli za Zain unahusisha nchi 15 zenye wateja 42 milioni. Idadi ya watu wanaoishi ni zaidi ya milioni 450 na mwingiliano wa simu ni takriban asilimia 32. Nchi ambazo Bharti imenunua shughuli zake ni; - Burkina Faso, Chad, Congo Brazzaville, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Gabon, Ghana, Kenya, Madagascar, Malawi, Niger, Nigeria, Sierra Leone, Tanzania, Uganda, na Zambia. Zain inaongoza katika nchi 10 kati ya hizo nchi 15, na ni ya pili katika nchi zilizosalia nne.
Bharti ilishauriwa kuhusu makubaliano haya ya kibiashara na Standard Chartered Bank ambao walikuwa washauri wakuu, Barclays Capital kama mshauri mkuu mbia na SBI Group kama mshauri mkuu wa biashara (Onshore Advisor). Global Investment House , Kuwait walikuwa washauri wa kanda ( Regional Advisor).Standard Chartered Bank, Barclays, SBI Group, ANZ , BNP , Bank of America Merrill Lynch, Credit Agricole CIB , DBS, HSBC, Bank of Tokyo Mitsubishi UFJ na Sumitomo Mitsui Banking Corporation ni wafadhili wa Bharti katika makubaliano haya.
Herbert Smith LLP walikuwa Washauri wa Kimataifa wa masuala ya Sheria, Milbank Tweed Hadley & McCloy LLP walikuwa washauri wa masuala ya Fedha na Sheria na AZB & Partners walikuwa washauri wa Sheria wa India, wakati Ernst & Young walikuwa washauri wa Mahesabu.
Kuhusu Bharti Airtel Limited
Bharti Airtel Limited, ni kundi la makampuni ya Bharti, na inaongoza katika masoko yanayoendelea ya simu za mkononi katika nchi 18 Asia na Afrika. Kampuni ina zaidi ya wateja milioni 180.
Bharti Airtel imewekwa katika nafasi ya makampuni sita ya teknolojia yanayoongoza duniani na Business Week. Bharti Airtel inamuundo wa vitengo vinne vya biashara, simu za mkononi, (mobile), Telemedia, Kitengo cha Biashara ( Enterprise ) na TV za Digital,
Biashara ya simu za mkononi inatoa huduma katika nchi 18 Asia na Afrika. Biashara ya Telemedia inatoa huduma za data (broadband), IPTV na huduma za simu katika miji 89 India . Kitengo cha Biashara (Enterprise business) hutoa suluhisho kwa wateja wa makampuni, na huduma kwa makampuni yanayojihusisha na usafirishaji wa ndani na wa kimataifa. Huduma ya TV ya digital inatoa huduma nchini India . Huduma zote hizi zinapatikana chini ya chapa ya Airtel, (bila kuhusiha Bangaladesh na Africa ).
Miundombinu ya kimataifa ya mtandao wa Airtel inajumuisha umiliki wa mfumo wa mkongo wa baharini wa i2i na ushirika pamoja na umiliki katika mfumo wa mikongo mitano ya kimataifa ya baharini, SEA -ME-WE 4, EIG, I-ME-WE, AAG na UNITY. Kwa maelezo zaidi. Tembelea; www.airtel.in.
No comments :
Post a Comment