“Tunayofuraha
kubwa kwa mara nyingine tena kuona tumeweza kuungana na wenzetu wa
kabila la wasukuma katika kipindi cha wiki moja sasa na kusherehekea
furaha yao baada ya mavuno huku wakiendelea kuzienzi tamaduni zao. Ni
kwa mara ya nane sasa tumekuwa tukidhamini sherehe hizi za bulabo na
tunaahidi kuendelea kudhamini kwani sherehe hizi zina mchango mkubwa kwa
wasukuma na taifa kwa ujumla”. Alisema jaji Mark Bomani mwenyekiti wa
kampuni ya bia ya serengeti.
Kampuni
ya bia ya Serengeti imekuwa ikidhamini tamasha hilo kwa takribani mwaka
wa nane sasa,ambapo waandaaji wameishukuru kampuni hiyo kwa kuwezesha
na kufanikisha tamasha hilo, ”Napenda kutoa shukrani zetu kwa kampuni
ya bia ya Serengeti ambayo imekuwa mdhamini wetu kwa muda mrefu sasa
inafika miaka minane, tumekuwa nao bega kwa bega na hasa Mwenyekiti wa
Bodi ya Kampuni hiyo Mheshimiwa Mark Bomani ambae pia ni mlezi wetu hapa
Bujora” alisema Padri Mhoja, muandaaji wa tamasha hilo.
Naye
mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Magu Mheshimiwa Jacquieline Liana,
ameipongeza kampuni ya bia ya Serengeti kwa kudhamini tamasha hilo na
kuomba wadau wengine kujitokeza kudhamini kama wenzao wa kampuni ya bia
ya Serengeti wanavyofanya, pia aliwaasa vijana kuacha tabia za kunywa
pombe wakati wa kazi na badala yake wafanye kazi kwa bidii ili waje
kusheherekea sherehe hizi za Bulabo mwakani.
Katika sherehe hizo za Bulabo
vikundi vilivyoshiriki vilishindana kwa mtindo wa mtoano ambapo vikundi
viwili vikiwa katika pande mbili tofauti za uwanja vikitenganishwa na
bendera nyekundu, huku majaji wakiangalia ni kundi lipi lenye umati
mkubwa hivyo ni kuashiria kuwa mwenye watu wengi zaidi ndiye mwenye
mvuto zaidi na hapo kutangazwa mshindi. Kigezo kingine kichokuwa
kikiwafanya washiriki waongeze jitihada katika kucheza na kujikuta
wakiwapa raha zaidi watazamaji ni kile cha kundi linaloshindwa kutakiwa
kutoa elfu thelathini katika laki mbili ambazo zilikuwa zikitolewa kwa
kila kundi na kumpa mshindi.
Washindi
katika ngoma hizo zilizodumu kwa takribani wiki moja ni Nghomi Lukala,
Kanigini Hindiya, Kibola Shitungulu, Bagehu Lukala, Mayokagose, Kinasa
Ncheye, Nyamuitabungagwa Mnkoti, Mabeshi Lukwaja, Nyeyewaza, Shigulu
Dema, Bulolo Shokolo, Seleleko na Basesilia Bujora aliyemalizia siku ya
Jumapili baada ya mpinzani wake kuingia mitini.
No comments :
Post a Comment