Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Monday, October 19, 2009

MSONDO WIKIENDI HII WALIKUWA AFRI CENTER

Waimbaji wa bendi ya msondo music wakiwajibika wakati wa onesho lao lililofanyika katika ukumbi wa Afri center Dar es salaam kushoto ni Eddo Sanga na Juma Katundu.(picha na Rajabu Mhamila Super D Mnyamwezi)Wanamuziki wa bendi ya msondo music band wakiwajibika wakati wa onesho lao kushoto ni Zahoro Bagwe na Uluka Uvuruge( Super D Mnyamwezi)SADI ALLY Mashine akikaanga Chipsi

TWANGA PEPETA WAFANYA VITU VYAO LEADERS CLUB

Waimbaji wa bendi ya Afrikan stars twanga pepeta wakiwajibika katika viwanja vya lidaz club dar es salaam kushoto ni Chalez Gabrier Chals baba na Alex Fagason.(Picha na Rajabu Mhamila Super d Mnyamwezi) Wanenguaji wa bendi ya twanga pepeta wakiwajibika wakati wa onesho lao dar es salaam

FIVE STAR WASHIKA JIJI LA DAR

waimbaji wa kundi la five star wakiwajibika wakati wa onesho lao lililofanyika katika ukumbi wa max bar ilala Dar es salaam kutoka kushoto ni Hadija Yusufu Zainabu Said na Mariamu Mramari.(Picha na Rajabu Mhamila Super D Mnyamwezi)

ZANZIBAR STAR WAFANYA KWELI MANGO GARDEN

Waimbaji wa kundi la Zanzibar Modern Taarab Mwanamkuu Zayumba kushoto na Salma Kassim wakiimba moja ya nyimbo zilizoko kwenye albam mpya ya poa Mpenzi ya kundi hilo kwenye ukumbi wa Mango Garden Dar es Salaam juzi usiku (Super D Mnyamwezi)Wanamuziki wa Zanzibar Star wakiwajibika wikiendi hiiMwanamkuu Zayumba akiimba katika moja ya maonyesho yao wikiendi hiiMashabiki wakirusha roho

MENEJA WA UWANJA WA UHURU AFARIKI DUNIA

Kaimu katibu mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Bw. Gasper Mwombezi akizungumza na wandishi wa habari asubuhi ya leo kwenye ukumbi wa Idara ya Habari maelezo alipotangaza kifo cha Ghafla cha Meneja wa viwanja vya Uhuru na uwanja mpya wa Taifa kilichotokea usiku wa kuamkia leo baada ya kuangukiwa na ukuta.
Masanja alikimbizwa katika Hospitali ya Muhimbili ambapo baadae alifariki Dunia Bw. Gasper amesema habari zaidi zitatolewa baadae lakini Serikali kupitia Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo imeunda kamati ili kushughulikia masuala yote kuhusiana na msiba huo.
Selestin Masanja alizaliwa Urambo Mkoani Tabora Januari 20 mwaka 1957 na kusoma katia elimu ya msingi hapo baadae alijiunga na shule ya Sekonsari ya Itagana 1972-1975 baadae shule ya Sekondari Minaki 1975-1977.
Mwaka 1988 alienda nchini Cuba katika jiji la Havana na kuchukua shahada ya Uzamili wa Physical Education.
Akiwa mfanyakazi wa Serikali katika idara yaMichezo Marehemu Massanja aliwahi kuwa Afisa michezo mkuu daraja la I, Meneja wa uwanja wa Taifa, Mjumbe wa kamati ya Ufundi ya TFF, Katibu mkuu wa FAT Msaidizi, Afisa michezo idara ya Michezo, Katibu mkuu msaidizi wa FAT tena Kocha Mkuu wa African Sport ya Tanga

Sunday, October 18, 2009

SIMBA SPIDI 120 SHAAAAAAAAAAAAAA....

LIGI kuu Tanzania bara imeendelea tena leo katika dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam Wekundu wa msimbazi Simba wameichapa JKT Ruvu kwa magoli 4 - 1.
Kipigo hicho kikali kimeashiria timu ya Simba kuwa vitani Zaidi na kuwatumia ujumbe Dar es Salaam Young African kwamba wakae sawa watakapokutana nao.
Akielezea hali ya mchezo msemaji wa Simba Cliford Ndimbo amesema kuwa mchezo ulikuwa mzuri na ushindi huo walisitahili kupata, kutokana na mchezo mzuri walionyesha uwanjani wachezaji waKlabu ya Simba sasa inaongoza ligi ikiwa inajumla ya Pointi 24 katika msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara.

WACHEZAJI WA SOKA JIUNGENI SPUTANZA

Amry Massare mtangazaji wa kipindi cha Michezo na kipindi cha Viwanjani kinachorushwa siku ya Jumapili (12:00pm - 13:00pm) na mdau nambari moja wa viwanjani.blogspot.com akimuelekeza jambo katibu wa SPUTANZA Abeid Kasabalala mara baada ya mahojiano ya moja kwa moja katika kipindi cha viwanjani Radio Times FM.
Wachezaji wa soka nchini Tanzania wametakiwa kujiandikisha na kuwa wanachama katika chama cha wachezaji nchini Tanzania SPUTANZA chombo ambacho kimeundwa kupigania maslahi ya wachezaji.Hayo yamesemwa na katibu msaidizi wa SPUTANZA Abeid Kasabalala wakati akihojiwa katika kipindi cha VIWANJANI kinachorushwa na Radio Times fm Dar es Salaam kila siku ya Jumapili kuanzia saa sita kamili hadi sasa saba.
Kasabalala amesema anawashangaa wachezaji wa Tanzania hulalamika na kuhitaji msaada wakati tayari wakiwa na matatizo au mambo yanapowawia vigumu na wasijue wapi pa kukimbilia.
Amesema chombo hicho ni chao na ili waweze kukitumia wanalazimika kujiunga na kuwa wanachama.Miongoni mwa faida kubwa ambazo wachezaji wanaweza kufaidia na SPUTANZA ni pamoja na mikataba ambayo wanaingia na klabu zao lakini pia kuwasaidia kudai maslahi yao pindi wanapotimuliwa na klabu ama kusitishwa kwa mkataba wa mchezaji.
Amesema kwa sasa wameanza kutoa mafunzo maalumu kwa wachezaji ili kuwaelimisha na kuwafahamisha faida za SPUTANZA lakini pia kuwafundisha sheria mbali mbali za soka pamoja na taratibu za mikataba na wajibu wao kama wachezaji.Katibu wa chama cha wachezaji wa soka nchini Tanzania SPUTANZA Abeid Kasabalala akijibu jambo katika kipindi cha viwanjani Radio Times FM.

WASILIANA NA SPUTANZA (SOCCER PLAYERS UNION OF TANZANIA)
P.o.Box 13162, Dar es Salaam - POSTA HSE. - GHANA/OHIO AVENUE 4th FLOOR ROOM #403
SIMU - +255754270815, EMAIL: soccertanz@yahoo.com

SHIMIWI MOROGORO YAFANA, TIMU ZAONYESHA USHINDANI

Mchezaji wa netbol wa timu ya uhamiaji, Zena Naziri akifikiria jinsi ya kumtoka mchezaji wa kilimo, Asma Hamis wakati wa ufunguzi wa michezo ya SHIMIWI iliyofanyika Morogoro mwishoni mwa wiki iliyopita na kudhaminiwa na kampuni ya Vodacom, Uhamiaji ilishinda 35.21.(Picha na Rajabu Mhamila)CHANETA mnaona mambo yako huku...???Ukitaka kujua uhondo wa ngoma ni uingie uchezeBaadhi ya wachezaji wa timu ya kilimo wakivuta kamba wakati wa mashindano ya SHIMIWI yaliyodhinduliwa mwishoni mwa wiki iliyopita Morogoro na kudhaminiwa na Kampuni ya Vodacom kilimo iliwashinda lindi kwa kuwavuta mara mbili.(Picha na Rajabu Mhamila)Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Mwantumu Maiza akihojiwa na Mwandishi wa TBC Jeni John mara baada ya timu yake ya kuibuka na ushindi katika mashindano ya SHIMIWINaibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mwantumu Maiza (wapili Kushoto) akishangilia na wachezaji wa timu ya Wizara ya Elimu baada ya kubwagiza timu ya waziri mkuu wa goli 2-0Mchezaji wa timu ya waziri mkuu William Benjamin (kushoto) akimtoka mchezaji wa timu ya elimu Gunda Azizi wakati wa ufunguzi wa michezo ya SHIMIWI iliyozinduliwamjini Morogoro na kudhaminiwa na Vodacom ambapo Elimu iliibuka kidedea kwa magoli 2-0Mwakilishi wa Vodacom Tanzania MACFADYNE MINJA (kulia)akimkabidhi mipira na vifaa vya michezo mbali mbali mwenyekiti wa shimiwi Leonard Kikuli mjini Morogoro, vifaa hivyo ambavyo vitagawiwa kwa washindi wa mashindano hayo.Anayeshuhudia katikati ni muweka hazina wa SHIMIWI Wiliam Mkombozi.

MSINDI WA KWANZA WA ZAP APATIKANA - ZAIN

Ofisa wa Kampuni ya Zain Bi.Eleanora Maruma (kushoto) akibonyeza kitufe kwa ajili ya kutafuta mshindi wa kwanza wa Promosheni ya 'Shinda na Zap' iliyofanyika Dar es salaam mwishoni mwa wiki anaeshughudia wapili kushoto ni Msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha Bw.Emanuel Ndaki na Ofisa wa Mawasiliano ya Ndani wa Kampuni ya Zain Bi. Dangio Kaniki.(Picha na Rajabu Mhamila)

Saturday, October 17, 2009

MATOKEO YA LIGI KUU TANZANIA BARA OCT 17, 2009

YANGA 1 - 1 AZAM FC

MAJIMAJI 0 - 0 MANYEMA RANGERS

TANZANIA PRISON 1 - 1 TOTO AFRICAN

UCHAGUZI MKUU YANGA JANUARI 2010

Mwenyekiti wa timu ya Dar es Salaam Yang African Bw. Imani Madega (kulia)akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam kuhusu uchaguzi wa timu hiyo utakaofanyika Januari 3 mwakani, kushoto ni Katibu Mkuu wa timu hiyo Lawrence Mwalusako.
Akizungumza na kipindi cha michezo na burudani cha Radio Times FM Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Imani Mahugira Madega amesema sababu kubwa za kurudishwa nyuma kwa uchaguzi huokufanyika may mwakani ni kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge ambao unatarajiwa kufanyika Oktoba mwakani hivyo wameona bora warudishe nyuma uchaguzi wa Yanga kwa maslahi ya Taifa.

TANZANIA YAPOROMOKA KATIKA VIWANGO VYA FIFA

Tanzania imeshuka kwa nafasi tano katika viwangi vya Fifa Dunia katika msimamo uliyotolewa mapema leo.
Tanzania ambayo katika msimamo wa mwezi uliyopita ilikuwa ikishika nafasi ya 94 hivyo imeshuka hadi nafasi ya 99.
Hata hivyo kwa Ukanda wa Afrika Tanzania imeonekana kama imepanda kwa nafasi moja kwani wakati ikishika nafasi ya 94 Duniani Afrika ilikuwa ikishika nafasi ya 23, lakini kwa sasa Afrika inashika nafasi ya 22.
Kuporomoka kwa Tanzania kumetokana na kutoshiriki katika mashindano ya mbali mbali ya kimataifa ambayo hutumiwa na shirikisho la kandanda Dunia kupandisha nchi ama kushuka katika viwango vya kandanda.
Mataifa yamepanda katika viwango vya kandanda Duniani kutokana na kucheza michezo mingi ya kusaka nafasi ya kufuzu fainali za kombe la Dunia.
Ukanda wa Afrika mwezi uliyopita Ivory Cost ilikuwa juu lakini sasa licha ya kupanda kwa nafasi ya moja lakini imeshuka hadi nafasi ya pili na nafasi ya kwanza ikishikiliwa na Cameroon ambayo imepanda kwa nafasi 15.
Wakati nambari moja Duniani inaendelea kushikiliwa na Brazili ikifuatiwa na Hispania.

KOSTA PAPIC ASAINI MKTABA KUIFUNDISHA YANGA

Siku ya Alhamisi kocha Mserbia Kosta Papic alitiliana saini na klabu ya Yanga kwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja, kocha huyo ameanza rasmi kazi Ijumaa, Yanga imefikia hatua hiyo kufuatia kumalizika mkataba kwa kocha Dusan Kondic, mkataba ambao utamalizika Novemba 15 mwaka huu.katikati pichani ni Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Imani Mdega

GHANA MABINGWA WA DUNIA U-20

Vijana kumi wa Ghana wamefanikiwa kulitwa kombe la Dunia vijana chini ya umri wa miaka 20 kwa mikwaju ya penati katika mhcezo wa fainali dhidi ya Brazili.
Ghana, ambayo mchezaji wake Daniel Addo alitolewa kwa kadi nyekundu, baada ya kutolewa ilijiimarisha zaidi katika safu ya ulinzi na kukataa kufungwa na vijana toka Amerika ya Kkusini.
Walimaliza dakika tisini pamoja na muda wa nyongeza wakiwa zare ya bila kufungana, ingawa Brazili wanapaswa kujutia kwa makosa yaliyofanywa na Alex Teixeira kwa kushindwa kumalizia mpira uliyokufa.Emmanuel Agyemang-Badu ndiyo alikuwa shujaa wa Ghana na kuifanya kuwa taifa la kwanza toka bara la Afrika kwa kuitwaa uchampion wa michuano hiyo.
pande zote mbili zilikosa mkwaju mmoja wa penati katika mikwaju mitanop ya kwanza na kuzidisha wasi wasi kwa mashabiki wa pande zote mbili.

Thursday, October 15, 2009

SAFARI LAGER KUZAWADIA WATEJA PESA NA MATREKTA

Meneja wa bia ya Safari Lager Bw.Fimbo Butallah na Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Bw.David Minja wakionesha vipeperushi baada ya uzinduzi wa 'Chagua Zawadi yako' uliofanyika Dar es Salaam.(Picha na Rajabu Mhamila)

VODACOM WAJIKITA SWAHILI FASHION

Mbunifu wa Mavazi, Mustafa hassanali (kulia)akizungumza na waandishi wa habari dhidi ya tamasha la SWAHILI FASHION, kushoto ni meneja udhamini wa kampuni ya Vodacom George RwehimbizaMeneja udhamini wa kampuni ya Vodacom George Rwehimbiza akimpongeza mwanahabari Dina Zuberi baada ya kuibuka mshindi katika bahati nasibu ya papo hapo iliyofanyika leo wakati wa utambulisho wa swahili fashio. picha na Rajabu Mhamila a.k.a Super D Mnyamwezi

TWANGA PEPETA, WAIGIZAJI WAFANYA USAFI NYUMBANI KWA NYERERE

Baadhi ya wasanii mbalimbali nchini wakihitolea kufanya usafi nyumbani kwa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere Dar es salaam juzi.(Picha na Rajabu Mhamola)

Wednesday, October 14, 2009

PASCHAL CASSIAN MSHINDI BONGO STAR SEARCH

Hapo vipi wangwana huyu ndiyo mshindi wa BSS toka mwalimu wa kwaya hadi Muziki wa Kizazi kipyaPaschal Kasian akkiwajibika na wimbo wa pili katika Shindano la BSSMshindi wa Mashindano ya kuinuwa vipaji vya uimbaji BSS Paschal Kasian akiwajibika wakati wa mashindano hayo yaliyofanyika Dar es salaam.(Picha na Rajabu MHamila)Brother AY kama kawa aliwakilisha vema kwa burudani katika fainali za BSSShaa naye hakuwa nyuma alipiga shoo ya ukweli, unajua huyu kadhamiria kuja kuwashikaSHAA akidance na wachezaji show wakeHuyu ndiye mshindi wa pili Peter Msechu akiwakilisha mkoa wa Kigoma katika Shindano la BSS, jamaa huyu naye si haba anavipaji kibao, Mapromota na wamiliki wa Bendi changamkieni Dili kabla hajarudi kwao kujipanga ohoo!Huyu ni Kelvin Mbati alishika nafasi ya tatu katika fainali ya BSS akiwakilisha DSM.Huyu ni Jackson George moja ya washiriki wa shindano la BSS ambaye alishika nafasi ya NneHuyu ni Betrice William alichukua nafasi ya tano katika BSS Final.

Tuesday, October 13, 2009

YANGA NA SIMBA KUKIPIGA UWANJA MPYA WA TAIFA

katibu mkuu wa wekundu wa msimbazi Mwina Seif Kaduguda akiteta jambo na waandishi wa habari.
Na Rajabu Mhamila
KAMPUNI ya Simu za Mkononi ya Vodacom inataka mchezo wa watani wa jadi nchini Simba na Yanga uliopangwa kufanyika Oktoba 31 ufanyike katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) mchezo huo umepangwa kufanyika katika uwanja Uhuru, Dar es Salaam.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Emilian Rwejuna alisema mchezo huo utafanyika katika uwanja wa Taifa ambapo utatoa fulsa kwa washindi wa shindano la M-Pesa watashuhudia mchezo katika uwanja huo.
"Tumeandaa shindano kwa mashabiki wa klabu hizo kongwe kuwa watakaposhinda watapata nafasi ya kushuhudia mchezo huo katika uwanja wa Taifa kutokana na ukubwa wa mchezo huo," alisema Rwejuna.Kushoto ni katibu mkuu wa kuajiriwa wa klabu ya Yanga Laurence Mwalusako.
Alisema wamependekeza mchezo huo ufanyike katika uwanja huo kutokana na kutoa fulsa kwa washindi hao ambao baadhi yao inawezekana kuwa hawakupata nafasi ya kuingia katika uwanja huo ambao haujaanza kutumika rasmi.
"Ukiacha wapenzi wa timu hizo wanaoishi jijini Dar es Salaam ambao wanaweza kuwa wamewahi kuuona uwanja huo lakini shindano hilo litajumuisha wapenzi wa timu hizo wa nchi nzima hivyo uwanja huo utakuwa mnoja ya kivutio kwa mashabiki hao," alisema Rwejuna.
Uwanja huo ambao umezinduliwa rasmi hivi karibuni lakini umekuwa ukitumika kwa michezo ya timu ya Taifa pamoja na baadhi ya michuano mikubwa na michezo kati ya miamba hiyo ya soka Tanzania.
Timu hizo zilikutana katika uwanja huo wakati wa michezo yao yote miwili katika msimu uliopita ambapo katika mchezo wa kwanza Yanga ulishinda bao 1-0 na mzunguko wa pili zilitoka sare ya mabao 2-2.

TWANGA PEPETA KUCHEZA NETBAL NA TASWA

Majuto Omari akipokea jezi toka kwa meneja udhamini wa Vodacom Emilian Rwejuna
Na Rajabu Mhamila Super d Mnyamwezi
TIMU ya Mpira wa miguu na Netiboli ya bendi ya muziki wa dansi ya African Star 'Twanga Pepeta' kesho itachuana na timu ya waandishi wa habari za michezo (TASWA FC) katika viwanja vya leaders, Dar es Salaam.
Mashindano hayo ni maalum kwa ajili ya kumuenzi na kumbukumbu za hayati Mwalimu Julius Nyerere ambazo hufanyika Oktoba 14 ya kila mwaka tangu aage Dunia.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa African Star Entertainment (ASET), Asha Baraka alisema, Twanga pepeta wao wapo tayari kwa kucheza na timu hiyo ambapo timu yake imejiandaa kwa ajili ya shamra shamra hizo.
Alisema, sambamba na timu za pande hizo mbili pia wasanii mbalimbali wa filamu hapa nchini watashiriki kwa pamoja katika kuadhimisha siku hiyo.
Asha alisema, baada ya bonanza hilo, wataelekea katika makazi ya Mwl. Nyerere, Msasani kwa ajili ya kufanya usafi katika makazi hayo ikiwa ni pamoja na kupanda maua katika maeneo ya makazi hayo.
Alisema,wanamuziki na wasanii wengine ikiwa pamoja na waandishi watajifunza mambo mbalimbali aliyokuwa akiyafanya Mwl. Nyerere enzi za uhai wake ikiwa ni pamoja na kufahamu makazi yake.
" Nadhani hii ni njia pekee ya kuwafanya vijana hawa kufahamu historia fupi ya Mwalimu ikiwa ni pamoja kufahamu mambo mbalimbali aliyokuwa akiyakemea na kuyapinga kama Rushwa, Udini na Ukabila ili kuepuka machafuko", alisema Asha.
Asha alisema kumbukumbu hizo zitamaliziwa na burudani ya uhakika kutoka kwa bendi hiyo linalofanyika kila siku ya jumatano katika ukumbi wa Klab Billcanas, Posta, Dar es Salaam.

KITABU CHA UJASIRIAMALI CHAZINDULIWA

Mwandishi wa Vitabu vya Ujasiriamali na Muhazili Chuo Kikuu cha Elimu ya Biashara Bi.Mariam Tambwe (kulia) akizindua vitabu vinne vya ujasiria mali katika ukumbi wa Idara ya Habari na Maelezo Dar es salaam, kushoto ni Ofisa Uhusiano wake na Mtangazaji wa Kipindi cha Siesta Maisha Radio Times FM, Bi. Hawa Hassani.(Picha na Rajabu Mhamila)