Mchezaji mashuhuri wa timu ya Taifa ya Ufaransa na Barcelona Thierry Henry ametangaza kustaafu soka ya kimataifa na timu ya Taifa.
Henry mwenye umri wa miaka 32 ametangaza uamuzi huo wakati wa mahojiano na shirika la habari AP kabla ya kufikia uamuzi wa kujiunga na klabu ya mpira wa miguu ya New York Red Bulls.
Amesema kuwa anajiunga na klabu ya Red Bulls nchini Marekani, siyo kwa kutaka kumuiga David Beckham kwa kusafiri mara kwa mara baina ya Ulaya na Marekani.
Amesema huu ndiyo mwisho kwake kushiriki timu ya Taifa.
Tangu ajiunge na timu ya Taifa, Henry amefunga magoli 51 mara 123 alizoshiriki michuano ya kimataifa kwa niaba ya Ufaransa kuanzia mwaka 1997.
Alitia fora wakati akichezea klabu ya Arsenal ambako alikuwa nahodha na anatazamiwa kushiriki pambano la Red Bulls dhidi ya mahasimu wakuu wa klabu yake ya zamani, Tottenham hotspurs hapo tarehe 22 Julai.
Alipohama kutoka Arsenal mnamo mwaka 2007, Henry alijiunga na Barcelona ya Uhispania na alikuwa na mwaka mmoja uliosalia kwenye mkataba wake aliporuhusiwa na Barcelona kuweza kuihama.
No comments :
Post a Comment