Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, January 29, 2010

AZANIA WALAMBA DUME VIFAA VYA MICHEZO


Baadhi ya WAnafunzi wa shule ya SEkondari ya Azania wakikusanya vifaa mbalimbali baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti Mtenmdaji wa Kampuni ya IPP, Renginar Mengi Dar es Salaam jana.(Picha na Rjabu Mhamila)MWENYEKITI mtendaji wa Kampuni za IPP, Regnald Mengi jana, alikabidhi vifaa vya michezo kwa shule ya Sekondari ya Azania kwa ajili ya maashindano mbalimbali yakiwemo mashindano ya Shule za Sekondari ya UMISETA.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa mkuu wa shule hiyo Benald Ngozye, alisema anatambua umuhimu wa michezo katika mashule kwani humsaidia mwanafunzi kujijenga kiakili na afya na kwamba vifaa hivyo vitaifanya shule hiyo kufanya vizuri katika mashindano ya
UMISETA.
"Vifaa hivi vitumieni vizuri kwani vitawasaidia kunyanyua viwango vya michezo mkiwa hapa shuleni ambapo mnaweza kuwa wachezaji wa kutegemewa na Taifa hapo baadaye,"alisema mengi.Vifaa alivyoikabidhi shule hiyo ni pamoja na mipira 10 ya soka, mipira ya mchezo wa kikapu mitatu na mipira miwili ya mchezo wa wavu.
Vifaa vingine ni jezi seti 10 za mpira wa miguu, jezi za mpira wa kikapu, jezi za mpira wa wavu na jezi za mchezo wa riadha zote zikiwa ni seti tatu kwa kila mchezo na trakisuti 16 kwa ajili ya waamuzi na makocha wa shule hiyo.

Friday, January 22, 2010

DJ JD SASA KUSIKIKA RADIO TIMES FM 100.5 KATIKA BLUST 100.5

John Dilinga (DJ JD) akisani mkataba wa kuitumikia Radio Times FM katika kipindi cha BLUST 100.5, anayemtazama ni Meneja vipindi wa Radio Times FM Scholastica Mazula.
DJ mkongwe nchini John Dilinga maarufu DJ JD amesaini leo mkataba na Radio Times FM tayari kuanza kuunguruma kupitia masafa ya 100.5.
DJ JD ambaye inasadikia ndiye mkali na mtundu nchini Tanzania katika kuichezea Dj mashine na uchangaji wa muziki atakuwa akiendesha kipindi cha BLUST 100.5 kila siku kuanzia saa 10:00 jioni hadi saa 1:00 jioni, akitangaza na kumix mziki mwenyewe.
Akizungumza na viwanjani DJ JD amesema kwamba wapenzi wa aina ya uchangaji muziki wake na wasikilizaji wa RAdio Times FM wajiandae kupata burudani ambayo wameikosa kwa muda mrefu.
DJ JD amesema wanaodhani kwamba uwezo wake umeshuka, wafute kabisa mawazo hayo na wakitaka kuthibitisha basi wasikilize Radio Times FM 100.5 na watathibisha kile ambacho wanakifikiria.
DJ JD ni moja ya ma DJ na Watangazaji waliyotoa mchango mkubwa katika kuunyanyua muziki wa kizazi kipya yaani Bongofleva.Hapa John Dilinga (DJ JD) akijadiliana jambo na Meneja Vipindi wa Radio Times FM Scholastica Mazula wakati akisaini mkataba wa kuitumiki Radio Times FM.

MABONDIA WAZICHAPA KUSAKA NAFASI TIMU YA TAIFA

Bondia Denis Mwaisarage (kulia) akijaribu kutupa konde kwa mpinzani wake, Said Mtubukwa, wakati wa mazoezi ya kuchagua timu ya Taifa ya ngumi yaliyofanyika Dar es salaam jana (Picha na Rajabu Mhamila)Bondia Sanday Elias (kulia) akijaribu kutupa konde kwa mpinzani wake, Noel Akwilini, wakati wa mazoezi ya kuchagua timu ya Taifa ya ngumi yaliyofanyika Dar es salaam jana (Picha na Rajabu Mhamila)

KARATE KUENZI MUUNGANO KWA MASHINDANO

Mashindano ya karate ya kuwania kombe la Muungano yataanza kuvurumishwa April 24 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Phlip Chikoko ni Mwenyekiti wa Chama cha mchezo wa karate Taifa, TASHOKA, amesema mashindano hayo yanafanyika kila mwaka na yanashirikisha wachezaji kutoka mikoa yote inayoshiriki mchezo huo.
Maandalizi ya mashindano hayo yamekamilika ambapo washindi watajinyakulia zawadi mbali mbali vikombe medali.
Aidha amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kama wanavyojitokeza katika mashindano ya mpira wa miguu.

MPIRA WA MIKONO WAHITAJI MILIONI 14

Kiasi cha Shilingi million kumi na nne kinahitajika kuendeshea mashindano ya klabu bigwa ya mpira wa mikono yatakayoanza February 22 hadi 27 mwaka huu jijini Dodoma
Nicolaus Mihayo Katibu Mkuu wa chama cha Mpira wa Mikono Taifa TAHA, amesema mashindano hayo yanafanyika kila mwaka ambapo mwaka jana yalifanyika mwezi Februari katika jiji la Mwanza na timu ya Magereza Kiwira iliibuka kinara.

MTIBWA YAINYUKA MANYEMA 5-2

Mabingwa wa michuano ya kombe la Mapinduzi na Ngao ya Hisani Mtibwa Suger leo wamewaadhibu vikali vijana wa Manyema Rangers kwa kuwachabanga jumla ya magoli 5-2.
Alikuwa mchezaji Zuberi Katwila aliyefungua milango ya magoli kwa mtibwa kunako dakika ya saba ya mchezo akiunganisha pasi iliyopigwa na Shaaban Nditi.
Dakika 21 baadae Musa Kipao wa Manyema Rangers alikosa goli la wazi baada ya kipa kuhama golini na kubaki peke yake.
Mnamo dakika ya 35 mchezaji Masoud Ally aliipatia goli la pili Mtibwa Suger akiunganisha mpira wa adhabu ndogo uliyopigwa na Zuberi Katwila.
Kama haitoshi baada ya kurejea kutoka mapumziko ikiwa ni dakika ya 54 Saidi mkopi alifunga goli la tatu akiunganisha mpira uliyopigwa na Omari Matuta huku goli la nne likifungwa na MAsoud Ally kwa shuti la Mbali.
Katika dakika ya 71 Manyema walizinduka toka usingizi na kupata goli la kwanza toka Julias Mrope na kisha dakika ya 79 Mrope tena alifunga, lakini katika dakika ya 84 Yusuph Mrope alipigilia msumari wa tano katika lango la Manyema Rangers.

Thursday, January 21, 2010

CHEKA NA MBWANA WAPATA MENEJA

Mabondia Francis Cheka kushoto na Mbwana Matumla kulia wakiwa na Meneja wao Juma Ndabile mara baada ya meneja huyo kuongea na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa idara ya habari maelezo juu ya mkataba wa mwaka mmoja aliosaini na mabondia hao ili kufanya nao kazi, meneja huyo atakuwa na jukumu la kuwatafutia mabondia walimu kwa ajili ya mafunzo na kuwatafutia mapambano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi pamoja na kuingia mikataba mbalimbali ya mapambano na udhamini.

ZAP KUMUZESHA MTEJA KUNUNUA MAFUTA OILCOM

Meneja Huduma za Zap wa Kampuni ya Zain Bw. Deo Talimo (kulia) akitoa maelekezo ya jinsi ya kununuwa mafuta katika vituo vya OILCOM wakati wa uzinduzi wa kutumia huduma za Zap kununulia mafuta Dar es Salaam anaeshughudia kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni hiyo Bw.Costantino Magavilla na Ofisa.Bw. Abdi Adam.(Picha na Rajabu Mhamila)

JKT RUVU YATAMBA MBELE YA TANZANIA PRISON

Timu ya JKT Ruvu imeendeleza wimbi la ushindi katika ligi kuu Tanzania bara baada ya kuichapa Tanzania Prison 2-0 katika mchezo uliyopigwa uwanja wa Uhuru.
Mshambuliaji Sostenes Manyasi ndiyo alikuwa wa kwanza kuchungulia nyavu za Tanzania Prison baada ya kuunganisha pasi iliyopigwa na Hussein Bunu.Goli la pili na la ushindi lilifungwa na Stanley Nkomola (mwenye jezi nambari tano pichani) katika dakika ya 43 ya mchezo na kuwafanya kumaliza dakika tisini wakiwa na uhakika wa kuondoka na jumla ya pointi 3.
Kufuatia ushindi huo sasa JKT Ruvu wanafikisha jumla ya pointi 18 sawa na majimaji ya Songea, wakati Tanzania Prison wakiendelea kubaki nafasi ya kumi wakiwa na jumla ya pointi 8.

GAZETI LA MAJIRA LA MFANYA MBATIA KUMSAIDIA MOHAMED ALBANI

Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, Bw. James Mbatia akimkabiddhi sh. mil. 1.2 kwa ajili ya kununulia viungo bandia Mohamed Albani (12),na kuahidi kumsomesha baada ya kupata ajali ya kugongwa na treni mwaka 2005.Picha na maelezo ya mtoto huyo ilichapishwa na gazeti la Majira mwaka jana.(Picha na Rajabu Mhamila)Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, Bw. James Mbatia akimfunga mkanda Mohamed Albani (12),baada ya kumkabidhi Baiskeri ya kutembelea Dar es salaam jana, na kuahidi kumsomesha baada ya kupata ajali ya kugongwa na treni mwaka 2005.Picha na maelezo ya mtoto huyo ilichapishwa na gazeti la Majira mwaka jana.(Picha na Rajabu Mhamila)

MAJEMBE KAZINI

Kulia, Mkurugenzi wa Kampuni ya Udalali ya Majembe Action Mart Bw. Seth Motto akikata bomba la mdaiwa sugu wakati wa operesheni hiyo iliyoanza Dar es salaam jana baada ya kupewa uwakala na Kampuni ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASCO).
Kushoto ni Ofisa wa Kampuni ya udalali ya Majembe Action Mart akimwandikia makosa mmoja ya madereva wa daladala baada ya kupitisha gari katika njia isiyo halali Dar es salaam jana.(Picha na Rajabu Mhamila)

Monday, January 18, 2010

AZAM FC YABANWA MBAVU NA KAGERA SUGER

Mlinzi wa klabu ya Azam akiondosha moja ya hatari langoni mwao.
Timu ya Azam Fc imelazimisha sare ya goli 1-1 na timu ya Kagera Suger katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara uliyochezwa katika uwanja wa Uhuru.
Timu ya Azam ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata goli katika dakika ya 48 kipindi cha pili kupitia kwa mchezaji Saidi Sued, wkati goli la kusawazisha kwa Kagera Suger lilifungwa na Saidi Dilunga katika dakika 87 ya mchezo huo.
Kufuatia sare hiyo sasa Azam Fc wanafikisha pointi 22 wakiwa na fasi ya tatu wkati Kagera Suger wanafikisha pointi 13 wakiwa nafasi ya nane katika msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara.Golikipa wa Kagera Suger akiokoa moja ya hatari langoni mwake.
Kiujumla mchezo ulikuwa wa kuvutia kwani walikuwa wakishambuliana kwa zamu, nilimsikkia moja ya mdau akisema ukitaka kulifaidi soka Tanzania usiangalie mechi wakicheza Simba au Yanga mchezo unakuwa wa upande mmoja, uli ufaidi soka inabidi uangalie hizi timu zingine za ligi kuu.
Je wadau kunaukweli wa kauli hii? na kama upo ni kwanini? hebu tusaidieni mawazo hapo!!!

TFF - UCHAGUZI BAADA YA LIGI RUKSA

Shirikisho la kandanda Tanzania TFF limewaomba watanzania wote kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali ikiwemo ya makamu wa pili wa Rais wa Shirikisho hilo.
Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo Fredrick Mwakalebela amesema kwamba fomu za kuwania nafasi hizo zimeanza kutolewa mapema mwezi huu na mwisho utakuwa kesho.
Aidha baada ya wanachama wa klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba kupitisha rasmu ya katiba January 16 na kukubaliana Uchaguzi wa viongozi utafanyika baada ya Ligi Kuu Tanzania Bara Mwakalebela amesema TFF haina shida na hilo chamsingi ni katiba.
wakati huo huo Kamati ya mashindano ya TFF itakutana Jumanne ya tarehe 19 kijadili mambo mbambali ikiwemo ligi daraja la kwanza.
Kamati hiyo ilikutana ijumaa ya wiki iliyopita lakini hawakutoa maamuzi hadi hapo kesho.
Mwakalebela amesema vilabu tisa ndio vitakavyoshiriki ligi hiyo ambapo timu tatu ndizo zitazopanda daraja ambapo mwezi wa tatu ndio ligi hiyo inatakiwa ianze.

KUOGELEA KUTIMIZA KAULI YA RAISI - WAJIPANGA KURUDI NA MEDALI

Chama cha mchezo wa kuogelea hapa nchini kimeandaa mikakati kabambe ya kuhakikisha wanaandaa timu ya taifa ya mchezo huo itakayorudi na ushindi katika mashindano ya Jumia ya Madola yatakayoanza Oktoba mwaka huu mjini Delh nchini India.
Akizungumza na kipindi cha michezo cha radio Times Fm Katibu Mkuu wa chama cha mchezo huo Noel Kiunsi amesema wameamua kupanga mikakati hiyo ili kuinga mkono kauli ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete alipokuwa anapokea kifumbo cha malkia Burton kwamba anataka ushindi na si kushindana.

MICHUANO YA WAZI TENIS KUANZA FEBRUARI

Mashindano ya wazi ya mchezo wa tenisi yataanza kuvurumishwa mwanzoni mwa February mwaka huu katika viwanja vya klabu ya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
Nahodha wa mchezo huo Inger Njau amefahamisha kwamba mashindano hayo ni utaratibu wa mashindano ya kila mwaka na yanasimamiwa na chama cha tenisi Tanzania.
Aidha ameongeza kwamba washiriki wa mashindano hayo wanatoka kila pembe ya Tanzania pamoja na majirani zao Kenya na Uganda.
amesema maandalizi ya mashindano hayo yapo tayari ikiwemo zawadi kabambe kutoka kwa mdhamini wa mashindano hayo.

SIMBA YAENDELEZA UBABE KWA MAJIMAJI KATIKA LIGI KUU TANZANIA BARA

Mchezaji wa Simba Ramadhani Chombo akijiandaa kupiga mpira katika mchezo dhidi ya Majimaji uliyochezwa katika uwanja wa Uhuru, Simba ilishinda 2-0.
Timu ya Simba ya jijini Dar es salaam imeichapa timu ya Majimaji kutoka Songea Mkoani Ruvuma magoli 2 kwa Nunge katika mchezo mkali na uliokuwa wa upande mmoja uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru maarufu kama shamba la bibi.
Katika mchezo huo timu ya Simba ndiyo iliyotwala sana mchezo huku wachezaji wake wakikaa na mpira kwa muda mrefu na kufanya mashambulizi ya mara kwamara kwenye lango la timu ya Majimaji, amabpo magoli ya simba yamefungwa na mshambuliaji wake hatari Mussa Hassan Mgosi aliyefunga katika dakika ya 37 kipindi cha kwanza na 72 katika kipindi cha pili hivyo kuifa simba kuibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya majimaji.
Majimaji walifanya mashabulizi machache katika lango la timu ya Simba ambayo hayakuwa na madhara yoyote langoni mwa Simba hivyo kuwafanya wekundu hao wa msimbazi kuusogelea zaidi ubingwa wa Ligi kuu ya Vodacom 2010 ambao kwa sasa unashikiliwa na timu ya Yanga ya Jijini Dar es salaam.
Simba yenye pointi 36 baada ya ushindi mnono wa leo inahitaji kushinda michezo minne ili iweze kutangaza ubingwa kwa msimu huu wa 2010-2011 kazi ambayo kocha mkuu wa timu hiyo mzambia Patrick Phiri amesema atahakikisha anashinda michezo hiyo ili aweze kutangaza ubingwa mapema zaidi

Sunday, January 17, 2010

MATUMLA KUZIPIGA UJERUMANI FEBRUARI 6

Bondia wa Ngumi za kulipwa Rashidi "Snake Boy" Matumla anatarajiwa kupanda ulingoni huko Trabrennbahn Hypodrom, Karlshorst, Berlin, nchini Ujerumani Februari 6 dhidi ya bondia Simon kuwania mkanda wa Dunia wa IBF.
Akizungumza na Viwanjani Rashidi Matumla amesema anaamini atafanya vizuri katika pambano hilo kwani kwasasa akliwa chini ya Mwalimu Ally Bakari Champion anaona anamabadiliko makubwa katika uchezaji ikiwa ni pamoja na wepesi wa kurusha ngumi na kukwepa tofauti na awali.Katikati ni mdau wa viwanjani akiwa na rashidi Matumla aliyevalia kapelo na kocha wake Ally Bakari Champion.
Matumla amesema anamfahamu vema Bondia Benjamin Simon kuwa ni mzuri na anareko nzuri lakini anaamini atakuwa wa pili kumsimamisha ulingoni tena katika uwanja wa nyumbani.
Nilipomuuliza kocha na wakala aliyemtafutia pambano hilo Ally Bakari Champion amesema aliombwa kupeleka mikanda ya mabondia wa ngumi za kulipwa Tanzania ili wachague ni bondia gani mwenyesifa ili acheze na Benjamini.
Amesema baada ya kuangalia mikanda hiyo na kumkubali Matumla kutokana na umahiri wake ulingoni.
Rashidi Matumla amecheza jumla ya mapambano 47 ameshinda mapambano 39 na kupoteza mapambano 8.
wakati Mpinzani wake Benjamin Simon anaumri wa miaka 26 amecheza mapambano 17 amepoteza pambano moja tu.
HUU HAPA NI WASIFU WAKE

boxer: Benjamin Simon

Jinsia - Mwanaume

Tarehe ya kuzaliwa - 1983-01-28

Umri - 26

Meneja/Wakala - Robert Rolle

Uzito - middleweight

Urefu - 5′ 10″ / 178cm

Utaifa - Ujerumani

Anaishi - Berlin, Germany

Ameshinda 16 (KO 16) amepoteza 1 (KO 0) ametoka sare 0 = 17
Benjamin Simon katikati akiwa na Meneja wake kulia na kushoto ni Mlinzi wake

JUMBE ARUDI MSONDO

Waimbaji wa bendi ya Msondo music wakiwajibika wakati wa onesho lao lililofanyika Dar es salaam Kushoto ni Juma Katundu na Huseni Jumbe.(Picha na msondo)
BENDI kongwe ya muziki wa Dansi nchini ya Msondo Music imemludisha kundini mwimbaji wake maili, Huseni Jumbe 'Mzee wa Dodo' baada ya kukaa nje ya bendi hiyo kwa mwaka mzima
Akizungumza Dar es Salaam, Msemaji wa kundi hilo, Rajabu Mhamila 'Super D'
Alisema, wameamua kumrudisha kundini mwimbaji huyo baada ya kukaa viongozi na kukubariana nae na sasa ameshaanza kupanda katika jukwaa la bendi hiyo ambapo mpaka sasa tunajipanga kutoa nyimbo mpya za mwaka uhu baada ya mwaka jana kutambulisha albamu yetu ya huna shukrani na kuwa ipo mtaani kwa sasa inauzwa,Wakati huohuo, bendi hiyo kwa sasa imekuwa ikitoa burudani za wazi katika kuwaweka karibu wapenzi wake ambapo kila jumamosi tunakuwa katika viwanja vya TCC Chan'gombe na jumapiri uwa tupo Leaders Club jijini Dar es Salaam
Alisema, sambamba na burudani hizo pia wamejipanga kutoa nyimbo mpya kila baada ya wiki tatu ili kukamilisha albamu ya mwaka uhu mapema kadri iwezekanavyo alisema Mhamila,
Akitoa wito kwa wapenzi wa bendi hiyo kuhudhulia kuona maonesho yao popote yafanyikapo kwani kuna burudani ambazo azihitaji kuadithiwa

GOFU LUGALO WALAMBA ZAWADI ZA ZAIN

Luteni Burure Magige(Kushoto) akimkabidhi simu mshindi wa wiki katika mchezo wa gofu uliodhaminiwa na kampuni ya Zain Ofisa masoko wa Benki ya biashara ya Akiba Moses Namuisa baada ya kuibuka mshindi Lugalo,Dar es Salaam juzi.(Picha na Rajabu Mhamila)Mcheza gofu Sophia Mathias akijitayarisha kupiga mpira wakati wa mashindano ya mchezo huo ya kila wiki yaliyofanyika Lugalo Dar es Salaam juzi, mashindano hayo yalidhaminiwa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Zain.(Picha na Rajabu Mhamila)

KICKBOXING LIGI SASA KUPIGWA FEBRUARI 27

Wachezaji nane wamejitokeza kushiriki ligi ya ngumi na mateke kickboxing ligi itakayoanza feb 27 hadi marchi sita mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na kipindi cha michezo na burudani Mwandaji wa ligi hiyo ambaye pia ni bigwa wa dunia wa mchezo huo Japhet Kaseba amesema wachezaji hao wanatoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani.
Amewataja ambao wamejitokeza hadi sasa ni Kanda Kabongo kutoka Dar es Salaam, Emanuel Shija Musoma, Chaz Angaya Shinyanga, Michael Aren Mwanza, ally Mrisho Vandame na Masud Mkalambati.
amefahamisha kwamba wachezaji wanaohitajika kushiriki ni nane na aliwatangazia wale watakaofika mapema ndio Watakaopata nafasi ya kushiriki.

Friday, January 15, 2010

MATHARE UNITED FC IMELAMBA DUME KATIKA UDHAMINI

Klabu ya Mathare United FC ya nchini Kenya imefanikiwa kulamba udhamini wa miaka mitatu na kampuni ya Kenya Data Networks (KDN) kwa dau la Shilingi ya Kenya milioni 15 ikiwa ni pamoja na nyongeza ya Shilingi ya Kenya milioni 5 kwa ajili ya vifaa.
Mkataba huo mpya umetangazwa wakati wa hafala iliyofanyika Nairobi hotel Alhamisi usiku.
Akizungumza wakati akiwakilisha cheki ya Shilingi milioni 15 za Kenya, Meneja masoko wa KDN Mr. Vincent Wangombe, amesema wamefikia hatua hiyo ili kuzidisha kuimarisha uhusiano mzuri wa kusaidia soka ikiwa ni pamoja na kuwanyanyua wachezaji wa Mathare United nikimnukuu kwa kimombo to "provide role models we can believe in."
Mr. Wang'ombe anasema udhamini huo ni moja ya maswala ya kijamii ambayo kampuni ya KDN imejiwekea kutimiza mwaka huu.
Prof Hellen Sambili, waziri wa michezo wa Kenya ambaye alikuwa mgeni rasmi, ameishukuru KDN kwa kutoa udhamini huo wa nguvu katika historia ya soka la Kenya.
Sambili ameyataka makampuni mengine kuiga mfano huo mzuri kwa maendeleo ya jamii kupitia soka.
Anthony Kimani, kapteni wa klabu ya Mathare alipewa vifaa vipya wakati Mr. Wang'ombe alizawadiwa mpira.
Titus Mulama aliondoka na tuzo ya tatu kwa kuwa mwanasoka bora, kiungo bora na mfungaji bora wa pili.
Joseph Nyagah naye aliondoka na tuzo na tatu ya kuwa mchezaji bora wa pili, mfungaji bora na tuzo ya mchezaji aliyejitokeza michezo mingi.
Duncan Ochieng amekabidhiwa tuzo ya golikipa bora wa mwaka.
Andrew Tolowa, Edgar Ochieng, Anthony Khadudu, Anthony Kimani na Paul Ambembo wote wamepata tuzo ya wachezaji wanaochipukia, kujitokeza katika michezo mingi, na mfungaji.

BENITEZ HAONDOKI LIVERPOOL

Nafasi ya kocha Rafael Benitez siyo swala la kujadili licha klabu ya Liverpool kuondoshwa katika FA Cup baada ya kuchapwa na Reading, taarifa hiyo ni kwa mujibu wa kiongozi wa michezo wa klabu hiyo Christian Purslow.
Benitez anakabiliwa na msukumo mkubwa toka kwa mashabiki hasa baada ya kupteza nafasi kwa klabu hiyo iliyoshuka daraja, kuondolewa mapema katika ligi ya mabingwa na kufanya vibaya katika ligi kuu ya England.
Licha ya matatizo yake, Mhispania huyo bado anaendelea kupambana kubaki katika dimba la Anfield.
hata hvyo katika mahojiano Purslow amesema Benitez anaungwa mkono na uongozi wa bodi ya klabu hiyo.
Kapteni wa zamani wa Liverpoll, Ronnie Whelan jana alikaririwa akisema anaamini kocha Benitez sasa nafasi yake inalazimika kuchukuliwa na kocha mwingine.

HAWA WANAPASWA KUENDELEZWA

Hawa wanapaswa kuendelezwa, kwani naamini wanaweza kuchangia kuongeza soko la ajira kwa vijana, lakini wanaweza kurahisisha kupatikana kwa huduma nafuu kwa wakazi wa maeneo mbalimbali nchini na kuliongezea taifa kipato.Hii ni Dar es Salaam, gari hili lilotengezwa kwa mbao likiwa linatembea kufanya safari zake kama kawaida huku likitumia mafuta ya Taa na Disell.Hii ni Musoma, gari limetengenezwa kwa makuti

Thursday, January 14, 2010

SERENGETI - SISI WADHAMINI WA TAIFA STARS JUKUMU LA KULETA TIMU NI TFF

Katibu mkuu wa shirikisho la mpira Tanzania TFF Fredrick Mwakalebela akizungumza na wanahabari kwenye makao makuu ya kiwanda cha bia cha Serengeti Chang'ombe Temeke jijini Dar es salaam, anayefuatia katika picha ni Meneja uhusiano wa kamuni hiyo Teddy Mapunda na mwisho ni Msemaji wa TFF Frolian Kaijage.
Gazeti la New Vision la Uganda toleo la Januari 6/ 2010 lilichapisha habari likieleza kuwa Kampuni ya Bia ya Serengeti ndiyo iliyokataa maombi ya Uganda ya kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki na timu ya Taifa ya Ivory Coast wakati timu hiyo ilipokuwa Tanzania kujiandaa na fainali za mataifa ya Afrika zinazoendelea huko nchini Angola. Gazeti hilo liliendelea kudai kuwa uamuzi wa Ivory Coast kucheza na Rwanda ulikuwa baadaye kwani Serengeti ilitaka Ivory Coast icheze michezo miwili na Taifa Stars kwa madai kuwa Serengeti ilitaka kurejesha fedha ambazo ziliwekezwa kwenye ziara hiyo.
Habari hiyo ambayo kwa hakika haina ukweli wa aina yoyote ilimnukuu afisa wa Shirikisho la mpira wa miguu la Uganda FUFA aitwaye Moses Magogo akitoa madai hayo. Hata hiyo habari haikueleza Magogo ana cheo gani ndani ya FUFA.Serengeti Breweries inapenda kuufahamisha umma kuwa majukumu yake katika mpira yanafahamika vizuri kulingana na Mkataba ambao inao na Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF.
Kazi ya SBL ni kutoa fedha kwa ajili ya kulipia gharama kama zilivyoainishwa kimkataba.Si kazi ya SBL kualika timu za kucheza wala kuamua ni timu gani icheze na Taifa Stars au timu nyingie yoyote ile. Hiyo ni kazi ya TFF.Kwa mantiki hiyo tunapenda kuufahamisha umma kuwa habari nzima iliyoadikwa na gazeti hilo ni ya uongo na haina chembe ya ukweli.
Hata hivyo SBL inafahamu vema kwamba Uganda kupitia FUFA walialikwa na TFF na walijibu kwa maandishi kuwa hawawezi kuleta timu yao kwa sababu wanazozijua. Sasa hatuelewi maneno mengine yanatoka wapi. Ni wakati wa kupuuza uzushi wa namna hii wenye lengo la kuleta mtafuruku na kuvuruga uhusiano baina ya vyama vya mpira na wadhamini.

VYAMA VYA SOKA MIKOA - RAMADHANI NASIBU BADO TUNAKUHITAJI

Kutoka kushoto Shaibu Nampunde(Lindi) AMin Bkhresa (DRFA) Juma Muruwa (Mtwara) na Joseph Mapunda (Ruvuma).
Mikoa mitano wanachama wa shirikisho la soka Tanzania waemchukulia fomu ya kutetea nafasi ya makamu wa pili wa raisi wa TFF, Ramadhani Nasib.
Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Dar es Salaam DRFA, AMini Bakhresa amesema wamefikia maamuzi hayo ya kumchukulia fomu kwa mapenzi yao kutokana na mchango wa kiongozi huyo tangu achaguliwe kushika nafasi hiyo mwezi Desemba 2008.
Ramadhani Nasibu alilazimika kuacha nafasi hiyo wazi kufuatia, nafasi ya makamu wa pili wa Raisi ambayo huwakilisha vilabu huongozwa na mtu ambaye ni kiongozi wa moja ya klabu zinazoshiriki ligi kuu Tanzania Bara.Mapema Shirikisho la kandanda Tanzania TFF lilitangaza mchakato wa kuziba nafasi zilizoachwa wazi ikiwa ni pamoja na makamu wa pili wa Raisi iliyokuwa ikiongozwa na ramadhani Nasibu ambaye alikuwa kiongozi wa klabu ya Villa Squad ambayo imeshuka daraja, ambapo kwa mujibu wa katiba alilazimika kufanya hivyo.
Wanachama waliyoungana kumchukulia fomu Ramadhani Nasibu ni Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Dar es Salaam, Amini Bakhresa, Mwenyekiti wa Chama cha soka Ruvuma Joseph Mapunda, Mwenyekiti wa chama cha soka Lindi Shaibu Nampunde, Mwenyekiti wa chama cha soka Tanga Saidi Sudi na Mwenyekiti wa chama cha soka Mtwara Juma Muruwa.
wagombea wengine ambao tayari wamekwishachukua fomu hadi sasa ni pamoja na Mwenyekiti na mkurugenzi wa klabu ya Manyema Abeid Abeid maarufu Falcon.

Wednesday, January 13, 2010

TBL WAKABIDHI VIFAA VYA TAHAMANI YA MILIONI 62 KWA SIMBA NA YANGA


Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) David Minja (kushoto) akimkabidhi jezi Katibu Mkuu wa Clubu ya Yanga, Lawlence Mwalusako, Dar es Salaam jana kwa ajili ya msimu wa ligi kuu ya Tanzania bara inayotarajia kuendelea hivi karibuni anaeshughudia katikati ni Meneja wa bia ya KIlimanjaro George Kavishe.(Picha na Rajabu Mhamila)Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) David Minja (kulia) akimkabidhi jezi Katibu Msaidizi wa Clabu ya Simba, Mohamed Mjenga,Dar es Salaam jana kwa ajili ya msimu wa ligi kuu ya Tanzania bara inayotarajia kuendelea hivi karibuni anaeshughudia katikati ni Mkurugenzi wa Utawara na Uwanachama kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)Mtemi Ramadhani.(Picha na Rajabu Mhamila)

Tuesday, January 12, 2010

TANZANIA YATWAA MEDALI TISA KUOGELEA - KENYA

Timu ya mchezo wa kuogelea imewasili nchini ikitokea jijini Nairobi nchini Kenya ikiwa na ushindi mnono katika mashindano ya kanda ya tatu na ya nne iliyomalizika Jumapili.
Akizungumza na viwanjani.blogspot.com katibu mkuu wa chama cha kuogelea Tanzania TSA, Noel Kiunsi amesema timu hiyo imefanya vizuri na kufanikiwa kurejea na medali tisa katika michuano hiyo.
Lakini wadau sasa hapa najiuliza huko katika mashindano hivi hawa walikuwa wanasema wanatoka wapi? Tanzania kweli? mbona wote wanaonekana ni wazungu! inamaana kweli hakuna mzawa kabisa anayeweza kuogelea? ni kwanini wazawa wenyewe hatushiriki na badala yake nafasi inachukuliwa na wenzetu ambao wengi ukiwauliza utasikia ni watoto wa mabalozi ama wazungu wanaofanya kazi nchini na baada ya muda wanaondoka.Au ndiyo kusema wazazi hawatoi fursa kwa watoto kuogelea? naomba wadau hapo tusemezane.
Hatukatai kuwa wazungu kuwakilisha Tanzania lakini sasa ndiyo timu nzima jamani?

GOFU YA FANA

Mchezaji wa mchezo wa Gofu, Moses Namuhisa, akijiandaa kupiga mpira wakati wa mashindano ya mwishoni mwa wiki yanayohandaliwa na kampuni ya Zain yaliyofanyika katika viwanja vya Lugalo Dar es salaami.(Picha na Rajabu Mhamila)Mchezaji wa mchezo wa Gofu,
Mohamed Lwehimamu, akijiandaa kupiga mpira wakati wa mashindano ya mwishoni mwa wiki yanayohandaliwa na kampuni ya Zain yaliyofanyika katika viwanja vya Lugalo Dar es salaam.(Picha na Rajabu MhamilaSayore akiwajibika katika gofu

MWEZINGO KURUDI TENA MSONDO

Wasanii wa Msondo Music band wakiwajibika wakati wa onesho lao lililofanyika Dar es salaam juzi kushoto ni mpiga kinanda Abdul Ridhiwani 'pangamawe' na mpiga gita la Solo Saidi Mabela.(PIcha na Rajabu Mhamila)
moses namuhisa,
Wakati huo huo MWIMBAJI nyota wa muziki wa dansi nchini,Rashidi Mwezingo 'Silver Boy' amesema anaipenda sana bendi ya msondo music hivyo kuwa yupo mbioni kurejea katika kundi la msondo ikiwa ni baada ya wiki kadhaa za kuwa nje kutokana na matatizo ya kiutawala
'Mwezingo amesema mda mchache ujao atalejea kundini na kuanza kuonekana kama mwanzo baada ya kuweka sawa mambo yaliyokuwa yakimkabili ikiwemo ukweli juu ya jukumu walilonalo viongozi wa bendi ya msondo katika kulipa deni analodaiwa na benki ambapo alikopa kupitia udhamini wa TOT.Plus
Lakini nilipohamia Msondo uongozi wa TOT ukauandikia barua uongozi wa msondo kueleza kuwepo kwa deni hilo ambalo napaswa kulipa sh.67,000 kila kila mwezi alisema.
Alifafanua kuwa barua hiyo kwa kiasi flani iliwachanganya viongozi wa Msondo ambapo walidhani jukumu la kulipa deni hilo ni lao, wakati ukweli ni kwamba ninapaswa kulipa mimi kupitia mshahara ninaolipwa kila mwezi.
Alisema badala yake viongozi hawo walisema awawezi kumudu kulipa deni hilo hivyo kuamua kuachana nae, lakini baada ya kuwaelewesha bila shaka wameelewa na sasa yupo mbioni kulejea kundini na kuendelea kutoa burudani jukwaani na nimeshatunga kibaa kitakachokwenda kwa jina la 'heshima ya ndoa' tutakachofanyia mazoezi baada ya kukaa pamoja hivyo kuwataka wapenzi wa Msondo kukaa mkao wa kula

Friday, January 8, 2010

TBF YALIPONGEZA JESHI LA POLISI YATOA ZAWADI KWA ASKARI JASIRI

Kamanda wa Polisi Mkoa
Kanda Maalum ya Polisi
DAR-ES-SALAAM

KUMPONGEZA NA KUMZAWADIA ASKARI WAKO WP……………. KWA UJASIRI

Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) linayo heshima kutambua na kuenzi ujasiri wa kiwango cha juu uliooneshwa na askari wako wote walioshiriki katika operesheni ya kukamata majambazi juzi jijini Dar Aidha tunampongeza binafsi na kumzawadia askari wa kike Constebo Mwachumu Haji kwa ujasiri wake unaostahiki kuigwa na wanawake wengine nchini. Kitendo kilichooneshwa na askari huyu ni cha kupongezwa na wanajamii wote, lakini ujasiri wake akiwa kama mwanamke ni wa kupigiwa mfano.
Taifa letu limekumbwa na vitendo vya ujambazi na mauaji kwa muda mrefu, jambo ambalo ni la kusikitisha na linalotakiwa kulaaniwa. TBF kama taasisi katika jamii, kwanza inakerwa sana na kuwepo kwa vitendo hivi, lakini pia tunaunga mkono na kupongeza juhudi zozote toka kwa jeshi la Polisi pamoja na wananchi kwa ujumla katika kupambana na kuutokomeza ujambazi na mauaji nchini.
TBF imeona ni vyema kupongeza ujasiri wa askari Polisi wote waliohusika katika operesheni ile lakini hasa ushupavu wa askari yule wa kike na kuwataka wanawake wengine nchini waige mfano ule katika nyanja zote, ikiwa ni pamoja na MICHEZONI.
Majeshi nchini, hasa jeshi la POLISI, ULINZI na JKT ni wadau wakubwa wa MCHEZO WA MPIRA WA KIKAPU, kwani wamekuwa wakishiriki vizuri katika ngazi zote tangu mikoa hadi taifa. Ni kwa heshima hii basi ndio nasi Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) tumeona tushiriki kuenzi na kupongeza juhudi hizo za wenzetu katika kutekeleza wajibu wao kwa jamii.
TBF inamzawadia Constebo Mwachumu Haji fedha taslimu Sh. 100,000.00 ikiwa kama ni kichocheo cha kuongeza bidii katika majukumu yake.

HEKO JESHI LA POLISI, HEKO MAJESHI.

UDUMU ULINZI SHIRIKISHI, TUDUMISHE MICHEZO


Mussa Mziya
RAIS
SHIRIKISHO LA MPIRA WA KIKAPU TANZANIA (TBF)
7 JANUARI, 2010


Nakala:
- Mhe. Jaji Augustino Ramadhani - Jaji Mkuu (Mlezi wa Shirikisho)
- Mkuu wa Jeshi la Polisi
- Vyombo vya Habari