Klabu ya Mathare United FC ya nchini Kenya imefanikiwa kulamba udhamini wa miaka mitatu na kampuni ya Kenya Data Networks (KDN) kwa dau la Shilingi ya Kenya milioni 15 ikiwa ni pamoja na nyongeza ya Shilingi ya Kenya milioni 5 kwa ajili ya vifaa.
Mkataba huo mpya umetangazwa wakati wa hafala iliyofanyika Nairobi hotel Alhamisi usiku.
Akizungumza wakati akiwakilisha cheki ya Shilingi milioni 15 za Kenya, Meneja masoko wa KDN Mr. Vincent Wangombe, amesema wamefikia hatua hiyo ili kuzidisha kuimarisha uhusiano mzuri wa kusaidia soka ikiwa ni pamoja na kuwanyanyua wachezaji wa Mathare United nikimnukuu kwa kimombo to "provide role models we can believe in."
Mr. Wang'ombe anasema udhamini huo ni moja ya maswala ya kijamii ambayo kampuni ya KDN imejiwekea kutimiza mwaka huu.
Prof Hellen Sambili, waziri wa michezo wa Kenya ambaye alikuwa mgeni rasmi, ameishukuru KDN kwa kutoa udhamini huo wa nguvu katika historia ya soka la Kenya.
Sambili ameyataka makampuni mengine kuiga mfano huo mzuri kwa maendeleo ya jamii kupitia soka.
Anthony Kimani, kapteni wa klabu ya Mathare alipewa vifaa vipya wakati Mr. Wang'ombe alizawadiwa mpira.
Titus Mulama aliondoka na tuzo ya tatu kwa kuwa mwanasoka bora, kiungo bora na mfungaji bora wa pili.
Joseph Nyagah naye aliondoka na tuzo na tatu ya kuwa mchezaji bora wa pili, mfungaji bora na tuzo ya mchezaji aliyejitokeza michezo mingi.
Duncan Ochieng amekabidhiwa tuzo ya golikipa bora wa mwaka.
Andrew Tolowa, Edgar Ochieng, Anthony Khadudu, Anthony Kimani na Paul Ambembo wote wamepata tuzo ya wachezaji wanaochipukia, kujitokeza katika michezo mingi, na mfungaji.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment