Baadhi ya WAnafunzi wa shule ya SEkondari ya Azania wakikusanya vifaa mbalimbali baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti Mtenmdaji wa Kampuni ya IPP, Renginar Mengi Dar es Salaam jana.(Picha na Rjabu Mhamila)
MWENYEKITI mtendaji wa Kampuni za IPP, Regnald Mengi jana, alikabidhi vifaa vya michezo kwa shule ya Sekondari ya Azania kwa ajili ya maashindano mbalimbali yakiwemo mashindano ya Shule za Sekondari ya UMISETA.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa mkuu wa shule hiyo Benald Ngozye, alisema anatambua umuhimu wa michezo katika mashule kwani humsaidia mwanafunzi kujijenga kiakili na afya na kwamba vifaa hivyo vitaifanya shule hiyo kufanya vizuri katika mashindano ya
UMISETA.
"Vifaa hivi vitumieni vizuri kwani vitawasaidia kunyanyua viwango vya michezo mkiwa hapa shuleni ambapo mnaweza kuwa wachezaji wa kutegemewa na Taifa hapo baadaye,"alisema mengi.
Vifaa alivyoikabidhi shule hiyo ni pamoja na mipira 10 ya soka, mipira ya mchezo wa kikapu mitatu na mipira miwili ya mchezo wa wavu.
Vifaa vingine ni jezi seti 10 za mpira wa miguu, jezi za mpira wa kikapu, jezi za mpira wa wavu na jezi za mchezo wa riadha zote zikiwa ni seti tatu kwa kila mchezo na trakisuti 16 kwa ajili ya waamuzi na makocha wa shule hiyo.
No comments :
Post a Comment