Timu ya Azam Fc imelazimisha sare ya goli 1-1 na timu ya Kagera Suger katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara uliyochezwa katika uwanja wa Uhuru.
Timu ya Azam ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata goli katika dakika ya 48 kipindi cha pili kupitia kwa mchezaji Saidi Sued, wkati goli la kusawazisha kwa Kagera Suger lilifungwa na Saidi Dilunga katika dakika 87 ya mchezo huo.
Kufuatia sare hiyo sasa Azam Fc wanafikisha pointi 22 wakiwa na fasi ya tatu wkati Kagera Suger wanafikisha pointi 13 wakiwa nafasi ya nane katika msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara.
Kiujumla mchezo ulikuwa wa kuvutia kwani walikuwa wakishambuliana kwa zamu, nilimsikkia moja ya mdau akisema ukitaka kulifaidi soka Tanzania usiangalie mechi wakicheza Simba au Yanga mchezo unakuwa wa upande mmoja, uli ufaidi soka inabidi uangalie hizi timu zingine za ligi kuu.
Je wadau kunaukweli wa kauli hii? na kama upo ni kwanini? hebu tusaidieni mawazo hapo!!!
No comments :
Post a Comment