Akizungumza na viwanjani.blogspot.com katibu mkuu wa chama cha kuogelea Tanzania TSA, Noel Kiunsi amesema timu hiyo imefanya vizuri na kufanikiwa kurejea na medali tisa katika michuano hiyo.
Lakini wadau sasa hapa najiuliza huko katika mashindano hivi hawa walikuwa wanasema wanatoka wapi? Tanzania kweli? mbona wote wanaonekana ni wazungu! inamaana kweli hakuna mzawa kabisa anayeweza kuogelea? ni kwanini wazawa wenyewe hatushiriki na badala yake nafasi inachukuliwa na wenzetu ambao wengi ukiwauliza utasikia ni watoto wa mabalozi ama wazungu wanaofanya kazi nchini na baada ya muda wanaondoka.
Hatukatai kuwa wazungu kuwakilisha Tanzania lakini sasa ndiyo timu nzima jamani?
No comments :
Post a Comment