Kamanda wa Polisi Mkoa
Kanda Maalum ya Polisi
DAR-ES-SALAAM
KUMPONGEZA NA KUMZAWADIA ASKARI WAKO WP……………. KWA UJASIRI
Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) linayo heshima kutambua na kuenzi ujasiri wa kiwango cha juu uliooneshwa na askari wako wote walioshiriki katika operesheni ya kukamata majambazi juzi jijini Dar Aidha tunampongeza binafsi na kumzawadia askari wa kike Constebo Mwachumu Haji kwa ujasiri wake unaostahiki kuigwa na wanawake wengine nchini. Kitendo kilichooneshwa na askari huyu ni cha kupongezwa na wanajamii wote, lakini ujasiri wake akiwa kama mwanamke ni wa kupigiwa mfano.
Taifa letu limekumbwa na vitendo vya ujambazi na mauaji kwa muda mrefu, jambo ambalo ni la kusikitisha na linalotakiwa kulaaniwa. TBF kama taasisi katika jamii, kwanza inakerwa sana na kuwepo kwa vitendo hivi, lakini pia tunaunga mkono na kupongeza juhudi zozote toka kwa jeshi la Polisi pamoja na wananchi kwa ujumla katika kupambana na kuutokomeza ujambazi na mauaji nchini.
TBF imeona ni vyema kupongeza ujasiri wa askari Polisi wote waliohusika katika operesheni ile lakini hasa ushupavu wa askari yule wa kike na kuwataka wanawake wengine nchini waige mfano ule katika nyanja zote, ikiwa ni pamoja na MICHEZONI.
Majeshi nchini, hasa jeshi la POLISI, ULINZI na JKT ni wadau wakubwa wa MCHEZO WA MPIRA WA KIKAPU, kwani wamekuwa wakishiriki vizuri katika ngazi zote tangu mikoa hadi taifa. Ni kwa heshima hii basi ndio nasi Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) tumeona tushiriki kuenzi na kupongeza juhudi hizo za wenzetu katika kutekeleza wajibu wao kwa jamii.
TBF inamzawadia Constebo Mwachumu Haji fedha taslimu Sh. 100,000.00 ikiwa kama ni kichocheo cha kuongeza bidii katika majukumu yake.
HEKO JESHI LA POLISI, HEKO MAJESHI.
UDUMU ULINZI SHIRIKISHI, TUDUMISHE MICHEZO
Mussa Mziya
RAIS
SHIRIKISHO LA MPIRA WA KIKAPU TANZANIA (TBF)
7 JANUARI, 2010
Nakala:
- Mhe. Jaji Augustino Ramadhani - Jaji Mkuu (Mlezi wa Shirikisho)
- Mkuu wa Jeshi la Polisi
- Vyombo vya Habari
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment