Edson Joel na Zaituni Kibwana wakiangalia kava ya Super D Boxing Coach leo
Saturday, April 30, 2011
DVD YA SUPER D BOXING COACH KUPATIKANA KIURAISI KESHO PTA
Edson Joel na Zaituni Kibwana wakiangalia kava ya Super D Boxing Coach leo
MTOTO WA MFALME, WILLIAM AFANYA KUFURU KWA KUFUNGA NDOA YA KIFAHARI ILIYOGHARIMU MABILIONI YA PESA
Mwana mfalme William akifungishwa ndoa na Aksofu Rowan William katika kanisa la Westminster Abbey jijini London.
Takriban wageni 1,900 walishuhudia tukio hilo ndani ya kanisa, na mamilioni wakifuatilia majumbani mwao kwa njia ya televisheni.
Maharusi hao walishangiliwa na maelfu ya watu waliojipanga barabarani kuelekea kasri ya Buckingham Palace ambako Malkia amewaandalia karamu wageni 650.
Wana ndoa hao wapya walitumia gari liliovutwa na farasi la muundo wa mwaka 1902 ambalo lilitumiwa na wazazi wake Prince William wakati wa ndoa yao mwaka 1981.
Maharusi hao baadaye walijitokeza kwenye roshani ya kasri ya Buckingham na kuwasalimu maelfu ya watu waliokwenda kuwasherehekea.
Baada ya kulishana viapo vya ndoa Askofu mkuu wa Canterbury, Rowan Williams, aliwanadi rasmi kuwa "mume na mke".
Kuanzia sasa maharusi hao watajulikana kama Duke na Duchess wa Cambridge.
MAPACHA WATATU NA WANAUME TMK KUTUMBUIZA IKWETA GRILL LEO
SHINDANO LA MISS TANZANIA LAZINDULIWA RASMI KILIMANJARO KEMPINSKI DAR ES SALAAM
Wadau hawa wakifuatilia uzinduzi wa mashindano haya ya urembo ambayo yamezinduliwa rasmi.
Mratibu wa Miss Tabata Fred Ogot akiwa na Miss Tabata 2010 Consolata Lukosi.
Mbunifu wa mitindo mbalimbali ya mavazi nchini Ally Rhemtullah.
Muandaaji wa Kituo cha Kurasini Miss Kurasini Bibie Zuhura naye alikuwepo.
Mhariri wa Habari za Michezo na Burudani Suleiman Mbuguni na Khadija Khalili.
Mama wa Bongoweekendblog nikijiegesha nje mara baada ya hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency pia Mratibu wa Miss Tanzania Hashim Lundenga akizungumza kwenye uzinduzi huo uliofanyika katika hoteli ya Kilimanjaro Kempinski Dar es Salaam.
Kampuni ya Viodacom usiku huu imezindua rasmi shindano lake la urembo la Miss Tanzania kwa kipindi cha maka 2011.Hapa Meneja udhamini wa Kampuni hiyo George Rwehumbiza amesema kuwa wao ndiyo wadhamini wakuu wa shindano hilo.Waliosimama nyuma yake ni baadhi ya warembo waliowahi kutwaa taji la Miss Tanzania.
Meneja Udhamini wa Kampuni hiyo ametoa wito kwa wazazi kuwapa ushirikiano vijana wao wenye nia ya kushiriki katika shindano hilo na hivyo kuonyesha vipaji vyao ."Pia nachukua fursa hii kuwaomba wasichana kokote walipo hapa nchini wajitokeze kwa wingi kushiriki katika shindano hili na kuonyesha vipaji vyao mbalimbali katika kuitumikia jamii yetu".
Hawa ni baadhi ya warembo Miss Tanzania ambao walikuwepo katika uzinduzi wa rasmi wa shindano na nembo mpya ya mdhamini wao Kampuni ya simu ya Vodacom waling'ara kwa miaka tofauti na kupeperusha bendera ya Taifa katika mashindano ya dunia .Kutoka kushoto ni Angela Damas Miss Tanzania (2001),Nasreen Karim (Miss Tanzania 2009),Jacqueline Ntuyabaliwe (Miss Tanzania 2000),Genevieve Mpamnaga (Miss Tanzania 2010) na Saida Kessy (Miss Tanzania 1997).
VIMWANA WA TWANGA KUONYESHA NYONGA ZAO LEO USIKU MANGO GARDEN 'TWANGA CITY'
Sugua Kisigino ni mtindo unaotumiwa na Twanga Pepeta na ni moja ya staili zitakazotumika kwenye shindano hilo, hivyo washiriki watatumia fursa hiyo ili kufahamu jinsi ya kucheza staili hiyo.
Washiriki watatumia onyesho hilo ili kusalimu mashabiki wa Mango Garden ukumbi ambao una historia ndefu na Twanga Pepeta.
Onyesho rasmi la utambulisho wa Vimwana wa Twanga Pepeta 2011 unatarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa tarehe 06-05-2011 ndani ya Club ya Sun Cirro iliyoko Sinza na Fainali itakuwa Ijumaa tarehe 03-06-2011.
Burudani ya Utambulisho wa Shindano la Kimwana wa Twanga Pepeta 2011 itatolewa na Wakali wa Dansi Tanzania, African Stars Band “Twanga Pepeta” na Msanii Abbas Kinzasa maarufu kama 20 percent au asilimia ishirini, pamoja na shoo kali ya Nyonga teketeke ya Vimwana wa Twanga Pepeta.
MAIMARTHA JESSE
MRATIBU WA SHINDANO.
WAFANYAKAZI IDARA YA HABARI (MAELEZO) WAMUAGA RASMI MKURUGENZI CLEMENT MSHANA ALIYETEULIWA KUONGOZA TBC
Clement Mshana, akizungumza na wafanyakazi wa Idara hiyo leo jijini Dar es salaam wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyoandaliwa na wafanyakazi hao.
HAPPYBIRTHDAY PRINCESS ASIA MAHMOUD ZUBEIR
Wednesday, April 27, 2011
MBWANA MATUMLA ANOGESHA NGUMI ILALA
BABY IKOTA SUPER D MNYAMWEZI AKISALIMIANA NA HABIBU KINYOGOLI
KANUMBA ATOKA NA Ramsey WA NIGERIA
Monday, April 25, 2011
NGUMI KUPIGWA PANANDIPANANDI ILALA BUNGONI KESHO
MABONDIA wa ngumi za ridhaa wa mkoa wa Ilala wanatarajia kupanda ulingoni kesho katika ukumbi wa Panandipanandi, Ilala Dar es Salaam. ambapo kutakuwa na ngumi kutoka kwa mabondia mbalimbali toka pande zote za mkoa wa DAr es Salaam
Tamasha hilo litakalokuwa likitimua vumbi kila wiki inatarajia kuwakutanisha mabondia wa Ilala na wa sehemu nyingine za Dar es Salaam ili kuweza kujipima nguvu katika kuinua mchezo huo katika mkoa huo.
Katika Tamasha hilo kesho bondia Mbwana Matumla anayejiaandaa kwa ajili ya kushiriki katika kuwania ubingwa wa UBO pambano linalotarajia kufanyika siku ya Mei mosi katika ukumbi wa PTA dhidi ya Mkenya Gabriel Ochieng atachuana na mabonmdia Yohana Robert na Issa Sewa.
Akizungumza Dar es Salaam leo, Mratibu wa Tamasha hilo kupitia Taasisi ya Kinyogoli foundation, Habibu Kinyogoli alisema mapambano yote yatakuwa katika raundi nne huku pambano la Mbwana likiwa katika uzito wa Kg 55 likiwa ni sehemu ya maandalizi ya pambano lake hilo.
Alisema, mkakati huo wa kuanzisha Tamasha akishirikiana na kocha msaidizi wa timu ya mkoa huo Rajabu Mhamila 'Super D' utasaidia kuinua vipaji vipya vya mchezo huo kwa kiasi kikubwa kwani kutawajenga wachezaji kujikita katika mchezo huo na kuufanya kama ndio ajira yao.
Alisema, katika kulifanikisha hilo anawaomba wadau mbalimbali kuwasaidia kuwadhamini ili waweze kufikia malengo yao katika kuinua vipaji hivyo.pia alisema kutakuwa na wageni waalikwa ambao watatoa mada mbalimbali kuhusu kuinua mchezo wa ngumi Tanzania akiwemo mdau wa ngumi.Innocente Melleck na mwingine Benedictor Hulilo ambao watakuwa wageni waalikwa
MASHINDANO YA SAFARI LAGER DARTS AFRIKA MASHARIKI YAMALIZIKA
Sunday, April 24, 2011
MISS KILIMANJARO HUYU HAPA
MISS TABATA MATAMBO YANAENDELEA..!!
Warermbo wakiwa katika pozi wakisubiri siku ya mchuano
Warembo wanaoshiriki shindano la Miss Tabata 2011 wakiwa katika picha za pamoja katika pozi tofauti wakati wa mazoezi yao katika Ukumbi wa Dar West Park Tabata jijini Dar es Salaam. Warembo hawa wanachuana kuwania taji linaloshikiliwa na Miss Tabata 2010 Consolatha Lukosi.