Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam BONANZA la kila Jumapili katika uwanja wa TP uliopo Sinza jijini Dar es Salaam litaendelea pia wiki hii kama ilivyo ada ya timu mbalimbali kuchuana asubuhi katika michezo tofauti kama vile soka, kuvuta kamba, kukimbiza kuku na mingine mingi huku wiki hii kukiwa na burudani ya nguvu. Hasa kwa mashabiki wa muziki kufundishwa staili mpya ya kusugua vocha bila kutumia funguo au kitu chenye ncha kali kama ilivyo kawaida kutoka kwa mkongwe wa dansi nchini, Hamza Kalala ambaye amehaidi kutoa zawadi kwa washindi. Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wake na waandaaji wa bonanza hilo, Media Entertainment Group, alisema amepania kutoa burudani ya nguvu na safari hii ikiwa ni mara ya pili kushiriki katika bonanza hilo, anawaletea mashabiki kitu kipya ambacho ni staili yake mpya ya kusugua vocha. "Hii ni staili yangu mpya, bado watu hawaijui vizuri hivyo nimeona niwape zawadi mashabiki watakaokuja katika bonanza hili pamoja na kutoa zawadi kwa watakaoicheza vema kwani nitawafundisha siku hiyo naamini wataipenda. "Hivyo sitaki kuzungumza mengi, naomba mashabiki waje kwa wingi kukomba zawadi sambamba na kuinoa staili hii mpya ya Bantu Group 'Wana Kasimbagu' ambayo tumewaandalia sambamba na kuwasikilizisha kibao kipya ambacho tutakirekodi mwishoni mwa mwaka huu cha 'Maisha dakika 90," alisema Kalala. Alisema mbali ya staili hiyo ya kusugua vocha pamoja na kibao hicho cha maisha dakika 90, pia atawapagawisha kwa vibao kadhaa kama kile cha Baba Jeni, Vicky, Ngozi ya Kitimoto na vingine vingi.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment