|
Zitto Kabwe |
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo kimesema kimewaandikia barua aliyekuwa
Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Zitto Kabwe na Mjumbe wa kamati Kuu Dk
Kitila Mkumbo ambazo wanapaswa kujieleza kwa siku kumi na moja, kisha
watapata fursa kujieleza mbele ya kamati kuu maalumu kwanini wasifukuzwe
Chama.
Akizungumza katika makao makuu ya chama hicho, Mkurugenzi wa
habari na Uenezi John Mnyika, alisema barua hizo zipo tayari na wahusika
watapatiwa wakati wowote kuanzia leo Novemba 26.
Mnyika alikuwa akitoa taarifa ya kikao cha Utekelezaji cha sekretarieti
ya chama hicho iliyoketi baada ya mkutano wa kamati kuu iliyoketi tarehe
20 – 22 Novemba mwaka huu.
Ni katika Mkutano huo, Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho, Tundu Lissu
alisema kuwa mkutano uliofanywa na Zitto na Dk Kitila mbele ya waandishi
hawajazungumzia tuhuma zinazowakabili, badala yake walichofanya ni
kujitungia tuhuma ambazo kimsingi sizo zilizo wavua nafasi zao.
Lissu alisema, Zitto na Dk Kitila hawakusimamishwa nyadhifa zao kwa
masuala ya PAC, Uchaguzi wa mwaka 2010, wala kutoshiriki kwenye
operesheni za chama au sababu zingine, na walitaja hizo sababu ili
kupotosha tuhuma zinazowakabili kwa jamii.
“Walichokifanya kina Zitto na Kitilla ni "Diversion" (kubadili mwelekeo)
wa mashtaka yao yanatokana na waraka wa kihaini wa mabadiliko ambao ni
kinyume na katiba, kanuni na maadili na itifaki ya Chama. anawaambia
waandishi, "wamevuliwa nafasi zao na kamati kuu kwa sababu ya waraka
wenye nia ovu" alisema Lissu.
Aliongeza kuwa Chadema kina mwongozo wa uchaguzi uliopitishwa na
kamati kuu, Zitto na Kitila wanaufahamu ingawa haijulikani ni kwanini
wao walienda kinyume na mambo yanayojadiliwa katika kamati kuuu
Aidha
Lissu alieleza kuwa Dk Kitilla anapotosha umma na wanachaka kwa kauli
yake kuwa kamati kuu haina mamlaka ya kumvua yeye nafasi yake ya ujumbe
wa kamati kuu maana amechaguliwa na baraza kuu, alimtaka Kitila na Zitto
waangalie vema katiba ya chama hasa majukumu ya kamati kuu, pale
yanaporuhusu Mwanachama yeyote kusimamishwa au kufutiwa uanachama haraka
kama kamati kuu itaona kuna umuhimu wa kufanya vile.
Kigaila alisema, Kamati kuu iliyoketi Novemba 20-22/2013 ilipitisha ratiba ya uchaguzi wa ndani ya chama kama ifuatavyo.
22/11/2013-14/12/2013
ni kukamilisha zoezi la usajili wa wanachama, 15 Desemba hadi 15
Januari uchaguzi ngazi za vitongoji, 16 januari 30 Januari 2014 Rufaa
naukaguzi, ambapo tarehe 01 Februari hadi 15 Februari ni uchaguzi wa
matawi.
Chadema pia ilisema 16 Februari hadi 29 mwezi huo huo ni
kusikiliza rufaa na ukaguzi, ambapo uchaguzi wa majimbo utaanza rasmi 1
Aprili hadi Aprili 10, huku uchaguzi ngazi ya Wilaya ukitarajiwa
kufanyika 25 Aprili hadi mei 5 mwaka 2014, na ngazi ya Mikoa ni 20 Mei
hadi 25 Mei.
Huku uchaguzi wa kanda ukitarajiwa kufanyika Julai
9, na haada ya hapo Julai 23 hadi Julai 30 utakuwa ndio muda wa uchaguzi
ngazi ya Taifa, utakaoanza na baraza la Wazee, Baraza la Vijana, Baraza
la Wanawake kisha uchaguzi wa ndaniya chama.