Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Sunday, September 20, 2009

WADAU WA VIWANJANI TUNAWATAKIA IDDI NJEMA

(toka kushoto AMRI H. MASSARE na RAJABU MHAMILA)
TUNA WASHUKURU WASOMAJI WA VIWANJANI KWA KUTUUNGA MKONO, TUNAWAOMBA MUENDELEE NA MOYO HUO HUO, LAKINI PIA MSISITE KUTUTUMIA MAONI, HABARI NA PICHA MBALI MBALI ZA MICHEZO KUPITIA EMAIL amrymassare@yahoo.com na viwanjani@gmail.com.
TUNWATAKIA KHERI NA BARAKA KATIKA SIKUKUU YA IDDI EL-FITRI

WATOTO WA KITUO CHA NEEMA WAKIPATA MKONO WA IDDI TOKA ZAIN...!!!

IDDI MBARAKA...!!!IDDI MBARAKAMbunge wa Ilala Mussa Azani Zungu (kushoto) akinywa chai ya asubui katika kituo cha kulea watoto cha Neema Maumba Islamick Center kilichopo Buguruni Malapa Dar es Salaam jana wakati wa kusheerekea sikukuu ya Iddi iliyoandariwa na Kampuni ya Zain wa pili kushoto ni Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Zain Bw, Ismail Katuma na Katibu wa Mbunge huyo Bw,Said Sultani.(Picha na Rajabu Mhamila)
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Zain, Bi,Beatrice Mallya, wa pili kulia akinywa chai ya asubui na watoto wa kituo cha Neema Maumba Islamick Center kilichopo Buguruni Malapa Dar es Salaam jana wakati wa sikukuu ya iddi iliyoadhimishwa jana kulia ni Mwalimu wa kituo hicho,Bi,Mariamu Dedes na watoto wanaoishi hapo kushoto ni Yusra Omari na Jasmini Kayanga chai hiyo iliandaliwa na Zain.(Picha na Rajabu Mhamila)
IDDI OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEIDDI OYEEEEEE

Friday, September 18, 2009

COCA COLA YALILETA KOMBE LA DUNIA KUZURU TANZANIA

Tanzania ni miongoni mwa nchi 52 katika Afrika, nchi ambayo inatarajiwa kutembelewa na Kombe la Dunia litakalokaa kwa muda wa siku mbili ikiwa ni jitihada za kuitangaza nchi yetu kwenye ramani ya soka.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi zaa Tff Rais wa shirikisho hilo la soka hapa Tanzania Leodga Chilla Tenga amesema kuwepo kwa uwanja mpya wa Kimataifa ituwezesha kupata wageni wengi kwa kuuwangalia Uwanja kupitia vyombo mbalimbali vya habari kitu kitakachopelekea timu nyingi kuomba uwanja kwaajilim ya kuutumia.
Kampuni ya Coca Cola ndiyo wadhamini wakuu wa safari hiyo ya utarii ambapo siku nne kuanzia leo huko Zurich,Switzerland itazinduliwa rasmi, kabla ya kuja Afrika litakalokaa kwa zaidi ya miezi miwili, ambapo kilele cha safari hiyo ya utarii itamalizikia Septemba 24 mjini Cairo Misri.Waandishi wa habari pamoja na mdau wa viwanjani wakifuatilia kwa makini mkutano.

EDDO SANGA WA SIKINDE ATUA MSONDO


Wanamuziki wa Msondo music bandi wakiimba wakati wa utambulisho wao wa kujiunga na kundi hilo Dar es Salaam jana, kushoto ni Juma Katundu na Eddo Sanga.(Picha na Rajabu Mhamila)
Na Rajabu Mhamila Super D Mnyamwezi

Kundi la Msondo ngoma music band leo limetangaza wanamziki wake wapya watakaolitumikia kundi hilo kuwa ni Juma Katundu ambae aliondoka na kurudi,Eddo Sanga, Aliyetimukia Sikinde na sasa karudi tena pamoja na Rashidi Mwezingo "Silver Boy" aliyetokea T Respect ambao watashiliki vema katika shamra shamra za sikukuu ya IDDi,inayotaraji kufanyika siku ya jumapili au jumatatu inategemea na muandamo wa mwezi.
Aidha Mkurungenzi wa bendi hiyo Muhidini Gurumo amesema kwa sasa wamejipanga vema kukabiliana na wimbi la ushindani wa muziki, nchini amesema wanatarajia kuzindua albamu yao mpya ijulikanayo kama Huna Shuklani itakayoingia mitaani kuanzia mwezi ujao.

Thursday, September 17, 2009

ZAIN WAWAAAAA... SASA KUONGEZA PUNGUZO LA BEI

Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa Zain Tanzania, Kelvin Twissa (katikati) akiwa na Meneja Mawasiliano wa Zain Tanzania, Beatrice Singano Mallya (kushoto) na Mratibu wa programu ya Zain Zawadi, Mwangaza Matotola (kulia) wakionesha kadi na vipeperushi vya programu ya Zawadi kwa Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam baada ya kutangaza kuongeza idadi ya makampuni nchini yatakayotoa zawadi na punguzo la bei kwa huduma na bidhaa mbali mbali nchi nzima kwa wateja wa Zain katika program yake ya Zain Zawadi.Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa Zain Tanzania, Kelvin Twissa (katikati) akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam kuhusu Zain kuongeza idadi ya makampuni yanayotoa zawadi na punguzo la bei kwa huduma na bidhaa mbali mbali nchi nzima kwa wateja wa Zain katika programu yake ya Zain Zawadi. Kulia ni Meneja Mawasiliano wa Zain Tanzania, Beatrice Singano Mallya na Mratibu wa Programu ya Zain Zawadi, Mwangaza Matotola (kushoto).

WAZEE WA VIWANJANI NA IVO MAPUNDA

Baadhi ya wadau wakuu wa glob ya Viwanjani wakiwa katika picha ya pamoja na Bwana Harusi mtarajiwa na Golikipa Maarufu nchini Tanzania Ivo Mapunda,Mara baada ya kutoka katika kipindi cha VIWANJANI kinachorushwa na Radio Times FM kila Jumapili kuanzia saa sita kamili mchana hadi saa saba kamili mchana.Kutoka kushoto ni Rajabu Mhamila,Amri Masare na Zahoro Mlanzi kulia.

KAYA KUPATIWA MLANDIZI KUPATIWA FEDHA NA TASAF


Baadhi ya wazee wa Kijiji cha Kwala Mlandizi Kibaha Pwani wakisubiri kuandikishwa wakati wa uhakiki wa majina kwa ajili ya Mpango wa jamii wa Uwasilishaji fedha kwa kaya masikini na wenye mahitaji maalumu inayofadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)kushoto ni Mwarabu Tengeni, Mlangonde Nyange na Asha Ponanga.(Picha na Rajabu Mhamila)Baadhi ya watoto wa Kijiji cha Kwala Mlandizi Kibaha Pwani wakisubiri kuandikishwa wakati wa uhakiki wa majina kwa ajiri ya Mpango wa jamii wa Uwasilishaji fedha kwa kaya masikini na wenye mahitaji maalumu inayofadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).(Picha na Rajabu Mhamila)

Wednesday, September 16, 2009

ZAMBIA YAALIKWA CECAFA CUP, TANZANIA NDANI...

Zambia imealikwa katika michuano ya kombe la Cecafa ambalo linatarajiwa kufanyika nchini Kenya kuanzia Novemba 28 .
Kenya itaanda mashindano hayo mwaka huu kwa mara ya kwanza katika miaka 17 maofisa wa CECAFA wamesema hii leo.
katibu mkuu wa Cecafa Nicholas Musonye amesema kuwa nchi zingine mbili kutoka kusini mwa Afrika zimeomba kushiriki michuano hiyo.
lakini Zimbabwe na Malawi wameambiwa kuwa kuna nafasi kwa Taifa moja tu kutoka kusini na kati mwa Afrika.
wazambia wamekuwa wakialikwa katika michuano ya CECAFA tangu mwaka 2007 walipolitwaa kombe hilo huko Ethiopia.
zambia wataungana na wenyeji Kenya,Tanzania, Uganda, Ethiopia, Sudan na Somalia, nchi nyingine shiriki ni Rwanda, Burundi, Eritrea, Djibouti na Zanzibar.
makundi mawili ya michuano hiyo yatakua mji mkuu wa Nairobi huku kundi la tatu litakua Mumias karibu na mpaka wa Kenya-Uganda.
jumla ya michezo 26 inatarajiwa kuchezwa katika wiki mbili za michuano ya CECAFA itakayofanyika huko Kenya.

MZIMU WA MAXIMO WAENDELEA KUMTAFUNA CHUJI

Kiungo wa Timu ya Yanga Athuman Iddi Chuji ataendelea tena na adhabu ya kufungiwa miezi mitatu na kutoa faini ya shilingi laki tano baada ya kuonyesha utovu wa nidhamu katika mchezo uliochezwa mjini Songea Septemba 5 kati ya Yanga dhidi ya Majimaji.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Tff Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo Fredrick Mwakalebela amesema kutokana na kamati ya nidhamu iliyokaa jana na kupitia masuala mbalimbali yahusuyo ligi hiyo hivyo kuamua kutoa adhabu kwa wachezaji,vilabu na waamuzi ili kuhakikisha soka la Tanzania linakua.
Kutokana na adhabu hiyo Kiungo huyo kwa sasa ataendelea na adhabu zote mbili ikiwa ile ya kwanza alipewa adhabu kama hiyo katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya African Lyon uliochezwa kwenye dimba la Uhuru Agasti 23 ambapo mpaka sasa ameshatumikia siku 7.
Mbali na adhabu hiyo klabu ya Maji Maji pia imetakiwa kutoa kiasi cha shilingi laki 5 kutokana na mashabiki wake kuonyesha utovu wa nidhamu.
Mwakalebela ameongeza kuwa kamati hiyo pia imewaondoa baadhi Waamuzi katika orodha kutokana na kushindwa kumudu katika kuendesha michezo yao kitu kilichopelekea kupata alama chache walizopewa na makamisaa wao.
Baadhi ya Waamuzi hao ni Peter Mujaya aliyeshindwa kuchezesha mchezo kati ya Simba na Toto African uliochezwa Septemba 5 mwaka huu wakati Athuman Lazi naye ameondolea katika orodha hiyo baada ya kushindwa kumudu mpambano kati ya Azam fc na Moro United uliopigwa Septemba 9.
Hata hivyo waamuzi wote waliochezesha mchezo kati ya Maji Maji na Mtibwa Sukari mchezo uliochezwa Septemba 9 mwaka huu nao wameondolewa katika orodha hiyo ambao ni Othaman Kazi,Omar Miyaya,Omar Mfaume na Kamwanga Tambwe.

SIMBA YAISHANGAA YANGA...!!!

Klabu ya wekundu wa msimbazi Simba imesikitishwa na klabu ya Yanga kudai kwamba wanakata rufaa dhidi ya mchezaji Uhuru Suleimani kumchezesha katika michezo ya ligi kuu hali ya kuwa ni mchezaji wa Mtibwa Sukari.
Msemaji wa Klabu ya Simba Cliford Ndimbo amesema hatua hiyo walioichukua yanga ni kutaka kuamishia matatizo yao katika klabu ya Simba kama timu yao inaporoka waangalie marekebisho lakini wasitape tape kumtafuta mchawi.
Amesema kinachotakiwa Yanga iwaambie ukweli wanachama wao sababu za kuboronga na si kuwatupia mzigo wa lawama Simba.

ZAIN NA MAMBO YA FUTARI

MWEZI WA RAMADHANI RAHA JAMANI, HEBU ONA HAWA WAFANYAKAZI WA ZAIN... FULL KUJICHANABaadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Zain wakipata futari jana jioni jijini Dar es Salaam baada ya Zain kuandaa futari kwa wafanyakazi wake. Zain pia imekuwa ikifuturisha na kutoa vyakula kwa yatima ikiwa ni sehemu ya kampeni yake ya kusaidia yatima nchini katika kipindi hiki cha mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

RAISI MSTAAFU ATOA MSAADA KWA YATIMA TABORA AKISHIRIKIANA NA ZAIN

Rais Mstaafu wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi (watatu mstari wa nyuma) katika picha ya pamoja na watoto yatima wa kituo cha Tabora Yatima Centre na wafanyakazi wa Zain Tanzania baada ya Mwinyi kufuturu pamoja na watoto na kuwakabidhi msaada wa vyakula uliotolewa na Zain. Futari hiyo iliandaliwa na Zain ilifanyika mjini Tabora Jumatatu jioni ikiwa ni sehemu ya kampeni ya Zain kusaidia yatima katika kipindi hiki cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

RAS JIHAD WATERMAN WA CANADA ASAINISHWA MKATABA HEWA WA MADINI NA WABONGO

Mkurugenzi wa Canadian Diamond Traders Inc Jihad Waterman akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusiana na kutapeliwa baada ya kuingia mkataba hewa wa madini na watu wasiyojulikana jijini Dar es Salaam na kumlazimu kufungua kesi ambayo inasikilizwa katika mahakama ya Wilaya ya Temeke. Picha na Rajabu Mhamila a.k.a Super D Mnyamwezi

TRL KERO MPAKA LINI ?

Katibu mkuu wa chama cha wafanyakazi wa Reli Tanzania TRAWU Bw Sylivester Rwegasira akizungumza na waandishi wa habari juu ya msimamo wa wafanyakazi wa shirika hilo na hali halisi ya kampuni dar es Salaam leo, Kulia ni Katibu mkuu wa chama hicho Bw. bakari Kiswala. Picha na Rajabu Mhamila a.k.a Super D Mnyamwezi.

Tuesday, September 15, 2009

MOHAMMED MPAKANJIA AZIKWA LEO MAKABURI YA KISUTU DAR ES SALAAM

Baadhi ya waombolezaji wa Msiba wa Mohammed Mpakanjia wakiswalia jeneza kabla ya kwenda kuzika katika makaburi ya Kisutu Dar es Salaam jana.(Picha na Rajabu Mhamila)
Baadhi ya waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza la marehamu Mohammed Mpakanjia kwa ajiri ya kwenda kuzika katika makaburi ya kisutu Dar es salaam jana.(Picha na Rajabu Mhamila)

MASHINDANO YA KUHIFADHI QUR-ANI YA FANA

Hemed Khamis (kushoto) akipokea Feni kutoka kwa Mgeni Rasmi, Mama Salma Kikwete baada ya kuibuka mshindi wa kwanza wa Juzu tano katika mashindano la kuhifadhi Kuran. Mashindano hayo ambayo yalidhaminiwa na Zain Tanzania yalifikia kilele chake jana katika Shule ya Sekondari ya Al-Haramain jijini Dar es Slaam.Picha na Rajabu Mhamila a.k.a Super DSamira Nasoro: (kushoto) akipokea TV aina ya HITACHI kutoka kwa Mgeni Rasmi, Mama Salma Kikwete baada ya kuibuka mshindi wa kwanza wa Juzu 10 katika mashindano la kuhifadhi Kuran. Mashindano hayo ambayo yalidhaminiwa na Zain Tanzania yalifikia kilele chake jana katika Shule ya Sekondari ya Al-Haramain jijini Dar es Slaam.Picha na Super D Mnyamwezi

GAPCO WAZINDUA UASILI WA MAFUTA

Wasanii wa Kikundi cha Sanaa cha Mawazo Tradition Band wakiwajibika, kushoto ni Tito Adamu na Said Kasimu wakati wa uzinduzi wa Kampuni ya Gapco kuzindua uasili wa mafuta wenye kuaminika jana.(PIcha na Rajabu Mhamila)

SIKINDE KURUDI NA UJIO MPYA

Hassan Rehani Bichuka akiwajibika katika moja ya maonyesho yao jijini Dar es Salaam.Picha zote na Rajabu Mhamila a.k.a Super D Mnyamwezi.
Bendi ya Muziki wa Dansi Tanzania Sikinde Ngoma ya Ukaye kwa sasa ipo kambini ikijipanga kurudi tena katika chati ya muziki huo hapa nchini ambapo wataanza kutoa burudani siku ya Iddi Mosi watatumbuiza katika ukumbi wa DDC Kariakoo (Old Traford) na Iddi Pili watakuwa Max Bar Ilala Bungoni.

Monday, September 14, 2009

MPAKANJIA AFARIKI DUNI

Habari zilizotufikia hivi punde zinasema aliyekuwa mume wa Amina Chifupa Meddy Mpakanjia amefariki dunia muda si mrefu baada ya kuugua kwa muda habari zimeenea jijini na kumekuwepo na mawasiliano mbalimbali ya ujumbe wa maneno kwa njia ya simu unaotumwa kwa wadau mbalimbali
Inasemekana Mohamed Mpakania amefariki katika Hospitali ya Lugalo alikokuwa amelazwa kwa matibabu

Saturday, September 12, 2009

England Premier League

Saturday, 12 September 2009

Blackburn 3-1 Wolverhampton
Diouf 19
Roberts 56
Dunn 64
Maierhofer 88


Liverpool 4-0 Burnley R
Benayoun 27
Kuyt 41
Benayoun 61
Benayoun 82

Man City 4-2 Arsenal
Almunia o.g. 20 van Persie 62
Bellamy 74 Rosicky 88
Adebayor 80
Wright-Phillips 84

Portsmouth 2-3 Bolton
Kaboul 25 Cohen 13
Boateng 63 Taylor (pen) 41
Cahill 89


Stoke 1-2 Chelsea R
Ab Faye 32 Drogba 45+3
Malouda 90+4

Sunderland 4-1 Hull R
Bent (pen) 13 Zayatte 44
Reid 49
Bent 66
Zayatte o.g. 75
Tottenham 1 - 3 Man Utd
Defoe (1) Giggs (25)
Anderson (41)
Rooney (78)


Sent off:
Scholes (59)

Friday, September 11, 2009

GARI LA MISS TANZANIA LAANIKWA, WAREMBO VICHEKO !!!

Baadhi ya washiriki wa Shindano la Urembo la Vodacom Miss Tanzania wakiwa mbele ya gari ambaro mshindi wa mashindano hayo atakabidhiwa waandaaji wa walipoonesha mbele ya waandishi wa habari Dar es salaam jana.(Picha na Rajabu Mhamila)
Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wanaowania gari hilo ni
Glory Chuwa kutoka Tanga
Slvia Shally Ilala
Miliam Gerald Mwanza
Jacqueline Nitwa Dodoma
Shani Anton Temeke
Wagala Shungu Higher lerning instite
Ivony William Kinondoni
Juliet william Ilala
Sabina Budodi Mara
Atera Chidodo Singida
Easter Gao Higher lerning instite
Doris Deonatus Higher lerning instite
Sandra Malembesa Kinondoni
Sia Ndasoki Temeke
Mary Lucas SWouthern highlands
Suzan Emanuel Arusha
Aloycia Immocent Kinondoni
Gladdies Shao Ilala
Precious Donald Pwani
Maria Daniel Arusha
Gloria Mayowa LIndi
Kuku Ibrahimu Ilala
Beatrce Lukindo Higher learning Institute
Evelyn Lujamasa Ilala
Glory Wiliam Ilala
Catherine Letara Southern highlands
Torry Oscar Morogoro
Mary JOseph Mara
Warembo ambapo wanasimamiwa na Miss Tanzania 2008, Nasreem Karimu na mkufuzi wa warembo kutoka ujerumani Tanja Rohrbacha

SEMENYA ANA JINSIA MBILI ???

Vipimo kwa bingwa wa Dunia katika mbio za mita 800 raia wa Afrika Kusini Caster Semenya hadi sasa bado vinautata lakini baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiandika kuwa anajinsia mbili ya uke na ume.
Semenya, mwenye umri wa miaka 18, ambaye aliombwa kufanyiwa vipimo ili kubaini jinsia yake kufuatia kuwashangaza watu katika michuano ya Dunia ya riadha mwaka huu na masaa machache kabla ya kushinda huko Berlin.
Magazeti ya Australia yamedai kwamba Semenya ni mtu mwenye jinsia moja lakini anahisia za jinsia nyingine ama ana jinsia zote mbili kitaalamu wanaita hermaphrodite.
Waziri wa Michezo Makhenkesi Stofile amesisitiza mapema leo kwamba "Caster is a woman, she remains our heroine. We must protect her."
Naye Raisi wa Riadha wa Afrika Kusini Leonard Chuene ameliambia gazeti la Star: kwamba IAAF wamewaambia matokeo ya vipimo yanatatanisha hivyo hawawezi kuwapataia.
Mwenyekiti wa Baraza la taifa la michezo, Butana Komphela ameongeza kuwa "Someone is guilty of leaking her confidential medical information to Australian newspapers."
IAAF imethibitisha kuwa kwa sasa haitatoa kauli yeyote kuhusu Semenya hadi wakati mkutano wa kamati ya utendaji ya IAAF itakapokutana Monaco Novemba 20-21.
Semenya alitwaa uchampion wa Dunia wa mita 800 mjini Berlin mwezi August kwa kuweka rekodi ya kukimbia dakika 55.45, akiwa mbele kwa dakika 2.5 dhidi ya bingwa wa mwaka 2007 Mkenya Janeth Jepkosgei.

ALLY KIBA NA PRETTY POET KUWANIA TUZO YA BEFFTA

Watanzania Ali Kiba, Pretty Poet( Jacqueline Kweka Kibacha) na kampuni ya Bongo UK ni miongoni mwa watu waliochaguliwa kuwania Tuzo za BEFFTA (Black Entertainment,Film,Fashion,Television and Arts Awards) zinazotarajiwa kufanyikia jijini London tarehe 17 October mwaka huu ndani ya London Hilton Metropole.
Ali Kiba amechaguliwa kuwania tuzo hizo katika kipengele cha Best International Act huku Pretty Poet akichaguliwa kuwania tuzo hizo katika kipengele cha Best Spoken Word Artist/Poets. Kampuni ya Bongo UK imechaguliwa kuwania tuzo hizo katika kipengele cha Best Event Promoters.
Kama ilivyo kawaida ya tuzo siku hizi,kura zinapigwa na wananchi.Wakati ukiwadia kwa zoezi hilo, VIWAJANI itakujulisha.Kwa sasa tunapenda tu kuwapongeza Ali Kiba,Pretty Poet na Bongo UK for the nomination.
Ally Kiba anachuana na Beyonce, Akon na 2face Idibia kuwania tuzo ya Best International Act.

Thursday, September 10, 2009

SIMBA KWENYE KONA SHAAAAAAA...!!!

Mnyama Simba amezidi kujikita kileleni katika msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara baada ya kuizamisha Kagera Suger kwa magoli 2-0.
Goli la kwanza la Simba lilifungwa na mchezaji Haruna Moshi "Boban" katika dakika ya 17 na goli la pili lilifungwa Mohammed Kijuso katika dakika ya 77.
Kufuatia ushindi huo Simba sasa inafikisha jumla ya pointi 12, ikifuatiwa na Mtibwa yenye pointi 9, huku ikiwaacha wapinzani wao Yanga waliyo nafasi ya tano kwa tofauti ya pointi 7.

JE HUU NI USAWA...???


Je huu ni usawa? picha hii inamuonesha mwanaume wa kizungu akiwa ametangulia mbele na kinywaji cha kupooza koo na mwamvuli wa kujikinga na jua huku nyuma mkewe akiwa amebeba mzigo wa kreti za vinywaji.

NYOTA WA VODACOM NA GSS AENDA UBELGIJI


Mkuu wa Kitengo cha udhamini wa Kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom, Ibrahim Kaude (kushoto) akimsindikiza mchezaji mwenye kipaji aliyechaguliwa kwa ushirikiano wa Vodacom na Global Soccer Star,Francis Casto,kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julias Nyerere,Dar es salaam wakati wa safari yake ya kwenda Ubelgiji,kuendeleza kipaji chake katika timu ya Cecle Brugge.(Picha na Rajabu Mhamila)