Umoja wa mchezo wa Kriketi Tanzania (TCA) pamoja na Umoja wa Kriketi wa mkoa wa Arusha “Arusha Region Cricket Committee” (ARCC) kwa kushirikiana na Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo umeandaa mashindano ya Kriketi yanayoendelea mkoani Arusha.
Mashindano haya yanakutanisha Klabu za mchezo wa Kriketi zipatazo tisa ambazo zimegawanywa katika makundi mawili yaani A na B. Hameed Sharif ambaye ni mmoja wa viongozi wa ARCC alisema kuwa kikundi A kinajumuisha Annadil Ezzi, Kilimeru pamoja na L/Kings wakati kikundi cha pili kimejumuisha AMMA Tigers, Expats, Swamibapa, Telugu Vaani pamoja na Wanderers.
Mashindano haya yameanza tarehe 22 January mwaka huu na yanatarajiwa kuendelea hadi mwisho wa mwezi huu kabla ya nusu fainali na finali zitakazofanyika tarehe 4 na 11 ya mwezi February. Udhamini huu mnono wa Tigo unafuatia Arusha kuwa moja ya mikoa inayofuatilia na kuendeleza mchezo wa Kriketi ndani na nje ya nchi.
ARCC ilianzishwa toka mwaka 1970 kusaidia kukuza mchezo wa kriketi jijini Arusha na Tanzania kwa Ujumla.
No comments :
Post a Comment