Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Sunday, January 1, 2012

UZINDUZI WA KIWANJA KIPYA CHA DAR LIVE

Kiwanja kipya cha michezo mbalimbali ya watoto kinachojulikana kama Dar Live kimezinduliwa leo huko Mbagala Zakhem jijini Dar es salaam , kiwanja hiki ni moja ya viwanja vizuri vinavyolifanya jiji la Dar es salaam kuwa na burudani katika maeneo mbalimbali hivyo kupunguza adha ya wakazi wa maeneo husika, kufuata burudani mbali kama ilivyokuwa mwanzo ambapo walikuwa wakienda Kunduchi Wet in Wild, South Beach Kigamboni au Beach Comber, jambo lililokuwa linawapa wakati mgumu kidogo watu wanaoishi maeneo ya Mbagala na Temeke kwa ujumla wake lakini sasa wamepata kiwanja cha kupeleka watoto kucheza. Katika kiwanja hicho pia kuna ukumbi wa Burudani na jukwaa kubwa la kisasa kabisa ambapo leo katika kuzindua kutakuwa na burudani kutoka kwa Juma Nature, Mh. Temba, Ali Choki na Extra Bongo pamoja na kundi zima la muziki wa Taarab la Jahazi Morden Taarab. Mimi leo nilijimuvuzisha na warembo wangu wapendwa Ivon kulia na Diana ili nao wajisikie kidogo katika siku hii ya kusherehekea mwaka mpya wa 2012, lakini mama Mkurugenzi yeye amesema ngoja apumzike baada ya kujumuika na wezake katika mkesha wa kuombea taifa kwenye uwanja wa Taifa usiku wa kuamkia leo hivyo tukasema sawa mama mkurugenzi pumzika.
Hapa ni vifaa mbalimbali vya michezo ya watoto vilivyopo katika kiwanja hicho cha Dar Live.
Hii ni moja wa toi la ndege ambalo watoto wamekuwa waakipenda kucheza humo pia katika kiwanja hicho.
Watu mbalimbali wakipumzika na kupata kinywaji na chakula katika kiwanja hicho.
Watoto wakicheza
Watoto wakicheza katika bembea.
Watu wakipishana kuingia na kutoka ni wazi kwamba watu wengi watafika ili kujionea mambo mbalimbali hapo Dar Live leo.
Picha za wasanii mbalimbali zimepambwa katika kuta za Dar Live yote hii ni kupendezesha kiwanja hicho.

No comments :

Post a Comment