Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, November 26, 2014

KITUO CHA KIMATAIFA CHA MICHEZO KUJENGWA MSOGA MKOANI PWANI


Mratibu wa Uhurumarathon Innocent Melleck kulia akizungumza na waandishi habari jijini Dar Es Salaam juu ya Mbio za uhuru kuanzisha mpango wa kuzindua kituo cha michezo eneo la Msoga linalijulikana kwa jina la Jakaya Kikwete Uhuru Sport Accademy ambapo kituo hicho kitagarimu jumla ya shilingi 4.8Bil ambapo kitashirikisha jumla ya michezo kumi na moja na madarasa kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha sita,Kulia ni Katibu mkuu wa chama cha riadha Tanzania Selemani Nyambui.


WAKATI usajili kwa watu wanaotaka kushiriki mbio ndefu za Uhuru, maarufu kama Uhuru Marathon, zinazotarajiwa kufanyika Desemba 7, mwaka huu jijini Dar es Salaam ukiendelea kwa kasi kubwa waandaaji wa mbio hizo wamezindua mpango wa kujenga kituo cha michezo eneo la msoga Mkoani Pwani.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa Kamati ya mbio hizo, Innocent Melleck alisema,kamati ya Uhuru Marathon imeona umuhimu wa kuanzisha kituo hicho ambapo jumla ya shilingi bil.4.8 zinatarajiwa kutumika katika kukamilisha mpango huo.
“Tunapenda kutangaza rasmi kwamba Uhuru Marathon imenunua shamba eneo la Msoga Mkoani Pwani lenye ukubwa wa ekari 25 kwa lengo la kujenga kituo kikubwa cha kukuza vipaji vya wanamichezo mbalimbali mkoani pwani eneo la msoga na kitajulikana kwa jina la Jakaya Kikwete Uhuru Sports Accademy na jumla ya michezo 11 itahusishwa katika mkakati huo.
Tunatarajia kumkabidhi mheshimiwa Rais Kikwete mpango huu wenye lengo la kuleta mafanikio makubwa ya michezo nchini ambapo watoto wenye vipaji watapata nafasi ya kusoma na kukuzwa katika utaratibu wa michezo na tunaamini kuwa baada ya miaka mitano hadi kumi tutaweza kuanza kupata mafanikio.
Kituo hiki ndicho kituo pekee katika ukanda wan chi za Afrika Mashariki na Kati ambapo jumla ya wanamichezo 2300 wataweza kuwa katika mpango wa awali.
Tunatarajia kupata nguvu toka katika wahisani mbalimbali wa ndani na nje ya nchi kwa kuwa wapo wanaohitaji kuona Tanzania ikipata mafanikio kupitia michezo.
Wakati huo huo zaidi ya wakimbiaji 2700 wameshachukua fomu kwaajili ya kushiriki mbio za mwaka huu huku malengo makuu yakiwa ni kuhitaji kushirikisha zaidi ya wakimbiaji 15,000.

Vituo vitakavyokuwa vikiuza fomu za ushiriki ni Tripple seven Mikocheni, Maduka ya TSN na Uchumi Supermarket,  Uwanja wa Leaderds Club,Ofisi za RT Taifa,Stendi kuu ya mabasi Moshi Mjini, Arusha pia kwa kutumia tovuti ya www.uhurumarathon.com

No comments :

Post a Comment