Mwenyekiti
Mtendaji wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) , Dkt.
Fatma Mrisho akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu Kauli Mbiu
ya Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani isemayo, Tanzania Bila
Maambukizi Mapya ya VVU, Vifo vitokanavyo na Ukimwi na Ubaguzi na
Unyanyapaa inawezekana inayolenga kupunguza maambukizi Mapya ya Ukimwi,
kupunguza vifo vitokanavyo na Ukimwi na kukomesha vitendo vya unyanyapaa
kwa asilimia Sifuri.
Mkurugenzi
wa ufuatiliaji wa Tathmini wa Ofisi ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi
Tanzania (TACAIDS) Dkt. Jerome Kamwela akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa
habari kuhusu utoaji wa huduma na upatikanaji wa dawa za kufubaza
makali ya Virusi vya Ukimwi kwa watu wanaoishi na VVU katika maeneo
mbalimbali nchini.
Mkurugenzi
wa Sera na Mipango wa TACAIDS akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo
pichani) mbinu na elimu inayotolewa na TACAIDS katika maeneo mbalimbali
ikiwemo matumizi ya mipira ya kike kwa wanawake ili kuzuia maambukizi
mapya ya VVU. Picha na Aron Msigwa - MAELEZO
Maadhimisho
ya siku ya UKIMWI Duniani kwa mwaka 2014 kitaifa yanatarajiwa kufanyika
mkoani Njombe kuanzia tarehe 24 mwezi huu hadi tarehe moja Desemba.
Hayo
yamesemwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya kudhibiti
UKIMWI (TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho wakati akiongea na waandishi wa
habari katika ukumbi wa mikutano uliopo makao makuu ya tume hiyo jijini
Dar es Salaam.
Dkt.
Mrisho amesema kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Tanzania bila
maambukizo mapya ya Virusi Vya Ukimwi (VVU), Vifo vitokanavyo na UKIMWI,
Ubaguzi na unyanyapaa inawezekana.
“Kauli
mbiu hii inalenga kutoa msukumo wa utekelezaji wa mikakati mbalimbali
ya kudhibiti UKIMWI kitaifa na kimataifa ili kufikia azma ya sifuri tatu
zinazomaanisha maambukizi mapya sifuri, vifo vitokanavyo na UKIMWI
sifuri na unyanyapaa sifuri ifikapo mwaka 2018”.
Kauli
mbiu hii pia inahimiza utekelezaji wa dhati wa malengo ya Maendeleo ya
Milenia na maazimio yaliyowekwa kwenye mkutano maalumu wa Umoja wa
Mataifa kuhusu UKIMWI uliofanyika mwaka 2001 nchini Marekani”, alisema
Dkt. Mrisho.
Amesema
kipaumbele cha maadhimisho ya mwaka huu ni upimaji wa hiari wa VVU na
ushauri nasaha, na kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi ili
wapate huduma hii muhimu.
Aidha
Mkurugenzi huyo amewataka wananchi kuadhimisha siku hiyo kwa njia ya
makongamano, kumbukumbu za waliofariki kwa UKIMWI, midahalo, mikutano ya
wazi, vipindi kupitia vyombo vya habari, kutembelea na kutoa misaada
kwa watoto yatima na wanaougua ugonjwa huo na kutoa elimu inayohusu
kujikinga na maambukizi.
Akizungumzia
kuhusu upatikanaji wa dawa za kupunguza makali ya ugonjwa wa UKIMWI
Mkurugenzi wa Sera, Mipango na Utafiti wa TACAIDS Dkt. Raphael Kalinga
amesema dawa hizo hutolewa bila malipo kwa wahitaji wanaostahili
kuzipata hii ni kulingana na mfumo wa utoaji kwa wahitaji.
Na Beatrice Lyimo na Aron Msigwa- MAELEZO
No comments :
Post a Comment