Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Thursday, November 13, 2014

Super Nyamwela amaliza Yangele


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgww4S1uEB1voeW70BdiFKYBrEQqAdJmgCQZ4D_JCvQ4KxFt3mdc9CLM_yNSxQakuGGQV6l-qPXv-VEQBpcFfnkkdD_aEWKmg0mXiVcC0uS9HF23WbjCFK8itrnnUUTM5DHGL73eF8ogJM/s1600/Nyamwela+2.jpgDANSA kiongozi wa bendi ya Extra Bongo, Hassan Mussa 'Super 'Nyawela' amekamilisha 'audio' na video ya wimbo wake mpya uitwao 'Yangele Yangele' anaojiandaa kuutambulisha kwa mashabiki wakati wowote kuanza sasa.
Akizungumza na MICHARAZO jana, Nyamwela alisema wimbo huo umetengezwa kwenye studio za C9 Records  na vuideo yake imefanywa na Mkenya anayefahamika kwa jina la Yfeel.
Nyamwela alisema amechelewa kuitambulisha 'ngoma' yake hiyo kutokana na kuwa kwenye majonzi mazito ya kuondokewa na mama Mlezi wao, Mama Shuu, aliyekuwa Mke wa Mkurugenzi wa bendi yao, Ally Choki.
"Tumetoka kumaliza 40 ya Mama Shuu jana (juzi), tuliamua kupumzika kabisa masuala ya muziki kuomboleza kifo cha mama yetu na sasa tumerejea upya, nikiwataka mashabiki wangu wajiandae kuipokea kazi yangu mpya ya 'Yangele Yangele' ambayo imekamilika 'audio' na video yake," alisema Nyamwela.
Kabla ya kazi hiyo, dansa huyo wa zamani wa bendi ya African Star, alikuwa akitamba na nyuimbo kama 'Duvele Duvele', 'Tumechete', Maneno Maneno' na nyingine zilizokuwa katika albamu zake mbili za awali za 'Master of the Tample' na 'Afrika Kilomondo'.

No comments :

Post a Comment