
Hatimaye Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar mchana huu ,imewaachia kwa dhamana Miss Tanzania 2009/10 Miriam Gerald na mpenzi wake Kennedy Victor 'Kanny'. Kufanikiwa kwa dhamana hiyo kumetokana na harakati za Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga ‘Ankal’ pamoja na ndugu wa kijana Keny ambao tokea Ijumaa iliyopita walikuwa wakihaha mahakamani hapo kuwawekea dhamana.
Watuhumiwa hao walipandishwa kizimbani hivi karibuni katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni wakikabiliwa na mashtaka mawili ya kujeruhi na kuharibu mali katika ukumbi wa TPDC uliopo Mikocheni jijini Dar.

Picha kwa hisani kubwa ya GPL
No comments :
Post a Comment