Mwamuzi wa Benin Bonaventure Koffi Codjia amefungiwa na shirikisho la kandanda barani Afrika.
Hatua hiyo imekuja kufuatia kutomchukulia hatua yeyote golikipa wa timu ya taifa ya Algeria Fawzi Chaouchi, ambaye alimpiga kichwa katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya Misri.
Golikipa huyo alipewa kadi ya njano licha ya kufanya kosa hilo kubwa mchezoni.
Codjia, ambaye ni moja ya waamuzi ambao watachezesha michuano ya fainali za Dunia, hakuliandika kosa hilo la kupigwa kichwa na golikipa katika ripoti ya mchezo ambao Algeria walilala kwa magoli 4-0.
Golikipa Chaouchi katika mchezo huo baada ya kufungwa kwa goli la Penati alimkimbilia mwamuzi na kumgeuza mwamuzi Codjia na kumpiga kichwa huku akilalamikia penati hiyo.
Lakini baadae Chaouchi alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumpiga kwanja mchezaji na kupewa kadi ya pili ya njano.
Caf imesema kamati ya nidhamu itasema baadae nini hatua zitachukuliwa kwa wachezaji Belhadj na Chaouchi hapo baadae.
Wachezaji hao wawili huenda wakakibiliwa na adhabu ya kufungiwa na kukosa fainali za Dunia.
RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN ATOA POLE AJALI YA KARIAKOO
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
akitoa salamu za pole kwa waathirika wa ajali ya kudondokewa na gorofa
Kariakoo Jij...
6 days ago
No comments :
Post a Comment