
kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mwanariadha anayeshikilia rekodi ya Dunia yam bio za marathon Paul Tergat, amesema Lelei, 39 na Tanui, 45, walikuwa wakiendesha gari toka Nairobi wakielekea nyumbani kwao Eldoret hapo jana na kkuligonga kilomita chache nje ya Nakuru, Mji wa nne kwa ukubwa nchini Kenya ikiwa na kilomita za mraba 200 magharibi mwa Nairobi.

Akiongea kwa maaseikitiko anakiri kwamba wamempoteza Lelei, lakini Tanui amenusurika na amelazwa Nairobi Hospital.
Lelei alishinda medali ya shaba katika mbio za mita 1,500 mwaka 1999 katika michuano ya All African Games iliyofanyika Johannesburg, mwaka huo huo alimaliza akishika nafasi ya saba katika mbio za Dunia zilizofanyika Seville. Inakumbukwa alimaliza akiwa wa nne katika mbo za mita 800 mwaka 2001 katika michuano ya ndani ya Dunia huko Lisbon.
Tanui alishinda mbio za mita 10,000 na kutwaa ubingwa wa Dunia mwaka 1991 katika michuano iliyofanyika Tokyo. lakini pia alishinda mbio za marathon 1996 na 1998 zilizofanyika Boston.
No comments :
Post a Comment