KAMATI ya Michezo ya Wilaya ya Ilala, imeiagiza klabu ya Simba ifanye uchaguzi wake mkuu ndani ya Machi 3 mwaka huu, vinginevyo Serikali itaingilia kati.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam Mwenyekiti wa kamati hiyo, Prisca Kissila amesema, Kamati ya Michezo inauagiza uongozi wa klabu hiyo uhakikishe lazima unafanya uchaguzi ndani ya siku 90 kutoka Desemba 3 mwaka jana.
Amesema kwa hiyo watalazimka kufanya uchaguzi kabla ya Machi 3 mwaka huu, sera ya maendeleo ya michezo inawalazimisha kifungu namba sita lazima waheshimu kipindi cha uongozi.
Kissila amesema , katika kikao walichokaa juzi (jana) maagizo yaliyotolewa na Mkuu wa Wilaya kwa Kamati hiyo yafuate katiba ya Simba pamoja na sheria namba 12 ya mwaka 1967 na marekebisho yake namba 6 mwaka 1971 ya Baraza la Michezo la Taifa na kanuni za usajili namba 442 za mwaka 1999.
Aidha ameongeza kwamba uongozi wa Simba uliomaliza muda wake, ulitakiwa kuitisha mkutano simu 30 kabla ya kumaliza kipindi cha uongozi au baada ya siku 30, lakini uongozi haukufanya hivyo.
Kissila amesema, uongozi wa Simba umekiuka katiba ya chama chao pamoja na kanuni za Baraza la Michezo la Taifa, uliitisha mkutano mkuu ndani ya siku 46.
Aidha amesema muhtasari wa kikao haukuletwa kwa msajili tangu wamalize kikao chao, katiba yao inasema Kamati ya Utendaji itapanga tarehe ya Uchaguzi Mkuu na si Mkutano Mkuu, lakini uongozi wa Simba ulidai mkutano utapanga tarehe ya uchaguzi ni kinyume na katiba yenye ridhaa yao.
Hata hivyo kabla ya ofisi ya msajili haijatoa ufafanuzi kundi la baadhi ya wanachama wa Simba wakiongozana na aliyekuwa katibu Mwenezi, Said Rubeya 'Seydou' lilivamia ofisi ya msajili huyo huku wakiwasonga viongozi waliowakuta kwa kuwalalamikia kuwa ndio wanaokwamisha uchaguzi.
Hata hivyo Kissila amesema, viongozi wa Simba jana waliitwa na Mkuu wa Wilaya lakini wamekaidi agizo hilo, hivyo Mkuu huyo ameahidi kuwatafuta ili waweze kutoa tamko la terehe ya uchaguzi kama walivyoamuliwa.
RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN ATOA POLE AJALI YA KARIAKOO
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
akitoa salamu za pole kwa waathirika wa ajali ya kudondokewa na gorofa
Kariakoo Jij...
6 days ago
No comments :
Post a Comment