
Hivi karibuni nilipoletewa kazi mpya na kuambiwa kwamba wasanii waliomo katika kazi hiyo ni TID(Top in Dar) na Chid Benz, nilikuwa na uhakika kwamba kazi hiyo itakuwa imesimama.TID na Chid ni miongoni mwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya ambao binafsi nawaheshimu na sioni noma kusema kwamba nazipenda nyingi kati ya kazi zao.Habari nzuri ni kwamba hawakuniangusha katika kazi hii ya hivi karibuni inayokwenda kwa jina Huyu.
Kama zilivyo kazi nyingi za wasanii wetu siku hizi,hii pia ni hadithi ya mapenzi (bado natamani wigo wa yaliyomo(content) za kazi za wasanii upanuke zaidi na kugusa maeneo mengine yanayoizunguka jamii).Kinachoufanya wimbo huu uwe tofauti ni uwezo binafsi wa wasanii husika na hadithi yenyewe.
Kazi hii imepikwa pale Tetemesha Records(kule kule alikoibukia Hussein Machozi) chini ya George Mpanda au maarufu kama Kid Bwoy.
No comments :
Post a Comment