Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara na wawakilishi katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrka Yanga wameahidi kubuka na ushindi katika mchezo wa marudiano dhidi ya FC Lupopo, mchezo utakaopigwa Lubumbashi, DR Congo.
Akizungumza kwa njia ya simu Luis Sendeu amesema, maandalizi yote yamekamilika, licha ya leo wakati wakifanya mazoezi kuvamiwa na watu wa Lupopo ambao waliwataka kuacha mazoezi na kuwapisha kuufanyia usafi uwanja ikkiwa ni pamoja na kukata majani.
Hata hivyo Sendeu amesema malalamiko ya kuzuiliwa kufanya mazoezi wameyawasilisha kwa ujumbe wa CAF na wameahidi kuyafanyia kazi.
Aidha hapo jana walikumbwa na kizaza cha kupotelewa na mabegi katika uwanja wa ndege wa Nairobi nchini Kenya wakati wakibadilisha ndege kuelekea Lubumbashi, Congo tayari kuwavaa FC Lupopo.
Akizungumza na viwanjani hapo jana katibu wa kamati ya mashindano ya Yanga, Emanuel Mpangala mara baada ya kuwasili Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, amethibitisha hilo na kusema takriban wachezaji wanne wamepoteza mabegi yao akiwemo Jerison Tegete, Boniface Ambani na Godfrey Bony.
Kikosi cha Yanga kimeondoka na Jumla ya wachezaji 18 na Viongozi wa nane, ambapo waliondoka majira ya saa kumi Alfajiri kwa ndege ya shiraka la ndege la Kenya KQ.
Msafara huo uko chini ya Kitwana Manara kutoka shirikisho la soka Tanzania TFF, Kocha mkuu wa Yanga Kotadin Papic, Daktari wa Timu Shecky Mngazija, Katibu Mkuu Laurence Mwalusako, Luis Sendeu Afisa habari wa Yanga, Meneja wa Timu Kenneth Mkapa, Emmanuel Mpangala na Mhasibu wa Timu Godfrey Mwenje.
Kwa upande wa wachezaji, ni Magolikipa ni Obren Cuckovic na Yaw Berko, wengine ni Fred MBuna, Shadrack Nsajigwa, Nurdin Bakari, Athumani Iddi “Chuji”, Shamte Ally, Nadir Haroub “Canavaro”, Jerison Tegete, Amir Maftah, Abdi KAssim, George Owino, Mrisho Khalfani Ngassa, Steven Bengo, John Njoroge, Boniface Ambani, Wisdom NDlovu na Kigi Makasi.
Utakumbuka msikilizaji katika mchezo wa kwanza Yanga walizabwa nyumbani katika uwanja bora Afrika Mashariki na kati, Uwanja wa mpya wa Taifa 3-2.
Ili kuweza kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, Yanga wanalazimika kuifunga Fc Lupopo magoli 2-0.
Wakati Yanga wakiwa wamecheza mchezo mmoja wa kirafiki na Zesco ya Zambia na kutoka sare ya bao moja kwa moja, FC Lupopo yenyewe iliondoka Lumbumbashi siku ya JUmatatu na kupiga Kambi katika mkoa wa Copperbelt nchini Zambia ikiwa ni maandalizi ya mchezo wa Jumamosi dhidi ya Yanga.
Lupopo walicheza mchezo wa kirafiki siku ya Jumapili na klabu ya Raon United na kuzabwa 2-1 kwenye uwanja wa Kabufu mjini Luanshya.
wafungaji wakiwa Ben Mwanza na Perry Sinkala wa Roan katika dakika ya 35 na 37, huku bao la kufutia machozi la Lupopo likifungwa na Junior Mubende katika dakika ya 14.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment