
katibu Mkuu wa TBF Alexander Msoffe amesema kozi hiyo itakuwa na manufaa makubwa kwa waamnuzi wa kikapu kwani wengi hawajapata nafasi ya kupandishwa madaraja na kutambuliwa na FIBA
Ametaja mikoa inayounda kanda hiyo kuwa ni Kilimanjaro, Tanga , Manyara na wenyeji Mkoa wa Arusha mbako Mafunzo hayo yatafanyika licha ya waamuzi wengine katika mikoa mingine wanayo nafasi ya kushiriki.
Katibu Mkuu amesema Mafunzo hayo ya siku Nne yamelenga waliowahi kucheza au wanacheza kikapu na
Walimu wa ngazi zote kuanzia Shule za Msingi nawatalazimika kujigharamia.
Kufuatia hali hiyo amewatolewa wito maafisa michezo nchini kutoa ushirikiano kwa kushirikiana na makatibu wa TBF wa Mikoa kuhakikisha wanatoa washiriki kadri wawezavyo.
Msoffe amesema licha ya kutambuliwa na FIBA itawapa Fursa nzuri waamuzi wa Tanzania kutambuliwa kimataifa zaidi hivyo ni vema kuitumia badala ya kuchezesha bila kutambuliwa wakati ni waamuzi wazuri.
Mzuka mzee wa viwanja mambo yako tunayakubali, upo juu
ReplyDelete