Chuo Kikuu cha Arusha cha peperusha Bendera ya Tanzania katika Zain Africa Challenge
Dar es Salaam, Jumatatu Machi 8, 2010
Chuo Kikuu cha Arusha, cha Tanzania ambacho ni chuo kikuu kichanga kimepeperusha bendera ya Taifa na kuitoa kimasomaso Tanzania katika mashindano yanayoendelea ya mtoano ya Zain Africa Challenge, chemsha bongo ya mtoano ya kimataifa ya Vyuo Vikuu.
Chuo Kikuu cha Arusha kimeshiriki kwa mara ya kwanza katika mashindano ya ZAC kikuchuana na Chuo Kikuu kikongwe cha Ghana na kilivibwaga vyuo vikuu vilivyozoeleka nchini Tanzania ambavyo vimekuwa vikishiriki katika mtoano huo wa kimataifa ; Vyuo vilivyotolewa na havikufika fainali ni pamoja na ; Chuo Kikuu cha Hubert Kairuki Memorial, Saint Augustine, Chuo Kikuu cha Mzumbe na Chuo Kikuu cha Muhimbili.
Programu ya Zain Afrika Challenge ni sehemu ya juhudi za Zain inayolenga kuboresha sekta ya elimu na inadhihirisha dhamira ya Zain ya kuleta Ulimwengu Maridhawa kwa wateja wa Zain.
Zain imewekeza zaidi ya dola za Marekani 1000,000 katika mashindano ya ZAC ilikutoa fursa kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu barani Afrika kukuza vipaji vyao.
Vyuo vikuu 32 kutoka nchi nane za Afrika ambazo ni Ghana, Kenya, Malawi, Nigeria, Sierra Leone, Tanzania, Uganda na Zambia vinachuana kuwania kombe la Zain pamoja na zawadi kubwa ya dola za Marekani 50,000 ambayo ndiyo zawadi ya mabingwa watakaoshinda katika fainali ya mashindano haya ya kimataifa.
Zawadi hizo ni sehemu ya zawadi za thamani ya dola za Marekani 1000,000 ambazo zitatolewa kwa washiriki wa ZAC mwaka huu. Zawadi hizo ni pamoja na fedha taslim, pamoja na vifaa vya kielemu kwa ajili ya vyuo vikuu vinavyoshiriki.
Tanzania mwaka huu inawakilishwa na Vyuo Vikuu viwili ambavyo ni Chuo Kikuu cha Tumaini pamoja na Chuo Kikuu cha Arusha. John Sibi-Okumu, maarufu kama Mwalimu ndiye anayeratibu shoo hii tena kwa mara ya nne mfululizo.
Mwaka huu pia watazamaji wa Zain Afrika Challenge wanafursa ya kushiriki katika mchezo wa Zain kupitia SMS. Wateja wa mitandao yote nchini safari hii wataweza kujibu maswali yanayoulizwa wakati na mtoano na kujishindia zawadi nono ambazo ni pamoja na simu mpya za mkononi aina ya Nokia N97 zenye thamani ya zaidi ya shilingi laki nane. Kushiriki katika mchezo wa ZAC watu wenye simu za mkononi watatuma majibu ya swali litakaloulizwa kwenda 15315. Zawadi hizi zitatolewa kila wiki ambapo watachaguliwa washindi watatu kila wiki.
Timu 100 kutoka Vyuo Vikuu vinavyoongoza kutoka nchi nchi hizo nane za Afrika zilichuana katika mashindano ya awali ya kitaifa ili kutafuta nafasi ya kuwakilisha nchi zao katika mtoano wa kimataifa na kujipatia fursa ya kujishindia sehemu ya zawadi zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja (Dola za Marekani 1,000,000).
Kati ya timu hizo 100, timu 32 zilizoongoza zimefuzu kushiriki katika mashindano ya kimataifa yanayofanyika nchini Uganda katika ushindani wa hali ya juu ili kuwania nafasi ya kushiriki fainali ya mashindano ambayo yatarushwa na luninga katika nchi zote nane zinazoshiriki na pia kwa mara ya kwanza, mashindano haya yatarushwa Afrika nzima kupitia satellite ya DSTV na yatatazamwa na zaidi ya watu milioni 700 kila Jumatatu saa moja na nusu usiku kuanzia Machi 1, 2010 kwenye kituo cha Africa Magic.
Akitangaza progamu ya ZAC inayoanza Jumapili iliyopita , Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zain Africa , Chris Gabriel alisema, ‘’ Zain Afrika Challenge ni ushuhuda wa dhamira ya Zain ya kuendeleza vipaji vya vijana kupitia misaada tunayotoa katika elimu pamoja na juhudi nyingine za kijamii. Na haya ndio mambo yanayodhihirisha Ulimwengu wetu Maridhwa wa Zain,’’.
Wizara za Elimu katika kila nchi pamoja na Tume ya Vyuo Vikuu ni wabia wakuu katika programu hii.
Katika msimu wa tatu wa Zain Africa Challenge uliofanyika mwaka jana Chuo Kikuu cha Ibadan cha Nigeria kiliibua na ushindi katika mtoano huo wa chemsha bongo na kujinyakulia zaidi ya milioni 60 (USD 50, 000) kutoka Zain, wakati kila mshiriki alijipatia kitita cha dola za Marekani 5000 kila mmoja. Nafasi ya pili ilichukuliwa na Chuo Kikuu cha Kenyatta ambacho kiliondoka na dola za Marekani 35,000, na kila mshiriki dola 3,500. Vyuo vingine vyote vilivyoshiriki vilipata zawadi zenye thamani kati ya dola 5000 na dola 25,000.
Maswali katika mtoano wa ZAC yanagusa maeneo mbali mbali ikiwemo, historia, sayansi, utamaduni wa Africa, Jiographia, literature, muziki ya matukio ya wakati huo. Kadhalika ZAC huonyesha fursa zilizopo za kielemu katika Vyuo Vikuu vya Afrika kupitia video na wasifu wa wanafunzi.
Yatakayojiri ZAC Msimu wa nne
.
•Kwa mara ya kwanza kutakuwa na mshindano kwa njia ya mtandao kupitia ; twww.facebook.com/ILoveZainAfricaChallenge na kutakuwa na zawadi za kila wiki za dola 100 katika muda wa maongezi na zawadi ya juu itakuwa Laptop.
• Kila wiki watu watapiga kura Barani Afrika kuchagua Mchezaji wa Wiki wa Mchezo na zawadi yake ni dola za Marekani 1000.
• Watazamaji watajishindia zawadi za juu ambazo ni pamoja na simu mpya aina ya Nokia zenye intaneti, muziki na video kwa kutuma majibu ya maswali yatakayoulizwa kwenda namba 15315.
• Zain Africa Challenge sasa inajumuisha watu wengi zaidi licha ya wachezaji, watu wa Idara ya Utawala katika Vyuo Vikuu na wanavyuo kwa sababu sasa taarifa zake zinapatikana kwenye Facebook na Twitter.
Vyuo vikuu ambavyo vimefuzu kushiriki mashindano haya ya kimataifa ni pamoja na: -
Tanzania
Tumaini University
University of Arusha
Ghana
Kwame Nkrumah University of Science & Technology University for Development Studies University of Ghana Valley View University
Kenya
Africa Nazarene University
Egerton University
Jomo Kenyatta University of Agriculture & Technology Kenya Methodist University Maseno University **
Malawi
Malawi Adventist University
Mzuzu University
University of Malawi
Nigeria
University of Ibadan
University of Abuja
University of Jos
University of Maiduguri
University of Nigeria
Sierra Leone
Njala University
University of Sierra Leone
Uganda
Makerere University
Uganda Martyrs University
Uganda Christian University
Kyambogo University
Mbarara University
Zambia
Copperbelt University
University of Zambia
Zambia Adventist University
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
9 hours ago
No comments :
Post a Comment