Timu ya Bussiness Times Limited maarufu The Bize ikiwa ni wamiliki wa gazeti la majira, Dar Leo, Spoti Starehe, Bussines Times na Radio Times FM leo wamefanikiwa kutnga hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la NSSF.
The Bize imefanikiwa kutinga robo fainali baada ya kuizaba Radio Kheri kwa magoli 2-0.
Mchezaji Rehure Nyaulawa ambaye ni mkurugenzi wa Radio Times FM ndiyo alikuwa wa kwanza kuwanyanyua mashabiki wa The Bize baada ya kufunga goli kwanza katika dakika ya 60 kipindi cha pili.
Kama haitoshi mchezaji Sande George alifunga goli la pili na la ushindi katika dakika ya 75 ya mchezo.
Ushindi huo mnono wa The Bize ulitokana na namna ambavyo walilisakama lango la radio Kheri na kuhakikisha wizara ya Ulinzi haitoi nafasi ya mchezaji yeyote kukutana wala kusalimiana na golikipa wa The Bize.
baada ya ushindi huo wa The Bize sasa watakutana na timu ya NSSF ambao ni wenyeji wa mashindano hayo katika mchezo wa robo fainali hapo siku ya Jumatatu ya tarehe 15 mwezi Machi, 2010.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
9 hours ago
No comments :
Post a Comment