Klabu ya Kenya, Ulinzi Stars, ambayo haijapoteza mchezo hata mmoja tangu kuanza kwa msimu wa ligi kuanza, sasa inaongoza ligi kuu ya Kenya (Kenya Premier league) ikiwa na jumla ya pointi 10, ikiwa pointi moja mbele dhidi ya KCB ambayo imefanikiwa kushinda michezo mitatu na kupoteza mchezo mmoja.
Klabu ya Western Stima inashika nafasi ya tatu ikiwa na jumla ya pointi 8, moja zaidi ya timu inayoshika nafasi ya nne klabu ya Sher Karuturi na pointi mbili mbele ya klabu kongwe ya Tusker na kukamilisha klabu tano ambazo zimekuwa na matokeo mazuri tangu kuanza kwa ligi.
Mathare United ilipata ushindi wake wa kwanza msimu huu katika mchezo wa jumapili kwa kuifunga Posta Rangers 2-1 na kujikuta ikilala nafasi ya sita ikilingana pointi na Tusker pamoja na Nairobi City Stars, Sony Sugar na AFC Leopards ambao wanashika nafasi ya 7 hadi 9 katika msimamo.
Mabingwa watetezi, klabu ya Sofapaka, ambao walipata pointi katika mchezo wa jumatatu dhidi ya Mahakama, sasa inashika nafasi ya 10 katika msimamo ikiwa na pointi nne.
Nafasi ya 11-13 inashikiliwa na Mahakama, Gor Mahia na Thika United ambazo zinapointi tatu kila moja, wakati Chemilil Sugar na Posta Rangers zinapointi moja moja na kushika nafasi ya 14 na 15.
Klabu ya Red Berets inashikilia mkia wa ligi kuu ya Kenya wakiwa na pointi moja mkononi.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
9 hours ago
No comments :
Post a Comment