Wachezaji wa vilabu vikongwe nchini vya Simba na Yanga wameendelea kulia njaa kufuatia kutopatiwa mishahara yao mpaka leo.
wachezaji hao kwa nyakati tofauti wamelalamika kuwa wamekuwa wakiishi kwa shida kutokana na kutopata mishahara yao inayowawezesha kujikimu wao pamoja na familia zao.
Kwa uapnde wa Yanga Afisa Habari wa Yanga Luis Sendeu akizungumzia madai hayo amekiri kutopatiwa mishahara kwa wachezaji na kusema haoni ajabu yeyote katika suala la kuchelewa kwa mishahara.
Kwa upande wa wekundu wa Msimbazi Simba, nako hadithi ni ile ile ambapo mhazini wa kuajiriwa wa klabu hiyo Chano Almasi amesema mcehzaji anayelalamikia kutopata mshahara wake akaangalie kwenye account yake ya benki.Chano Almasi amesema yeye ndiyo anyetunza na kutoa fedha hivyo anaamini fika tayari fedha wamekwishapeleka benki na kuwataka wachezaji hao kwenda kuchukua benki.
Klabu ya Simba kwa sasa imeweka kambi visiwani Zanzibar kujiwinda na mchezo wao wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Azam FC utakaochezwa katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam siku ya Jumapili.
lakini pia kambi hiyo ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wao wa kimataifa wa kombe la shirikisho barani Afrika.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
9 hours ago
No comments :
Post a Comment